Ntemi_Ntale
Member
- Aug 23, 2026
- 20
- 16
Kwa Ufupi ni Kwamba :
- OpenAI imezindua GPT-6.1 Terra, model ya ukubwa wa kati inayolenga kazi za kawaida za kompyuta kama kuandika, coding na kuendesha programu za kompyuta (computer use).
- Gharama zake zimeshushwa karibia nusu ukilinganisha na GPT-5.6 Terra.
- Inapatikana sasa kwa watumiaji wa Plus, Pro, Enterprise na Edu kupitia ChatGPT Work na Codex.
Jumatatu tarehe 26 .10.2026 , Mkurugenzi Mtendaji wa OpenAI, Sam Altman, alitangaza GPT-6.1 Terra,AI Model yenye kasi zaidi na gharama ndogo iliyoundwa kushughulikia kazi zinazofanyika kwenye kompyuta. Kwa mujibu wa kampuni hiyo, ni model ya ukubwa wa kati inayolenga kazi za kila siku kwenye kompyuta, zikiwemo kuandaa mapendekezo (proposals), kujaza fomu na kuhariri video. OpenAI imeielezea kama hatua kubwa mbele ukilinganisha na GPT-5.6 Terra.
kampuni ilisema inaleta model yenye kasi na yenye ufanisi inayounganisha uwezo wa kina wa kuchambua picha (visual reasoning), matumizi sahihi ya kompyuta, pamoja na uandishi ulio wazi na wa asili zaidi. Pia, inaweza kutafsiri michoro ya kiufundi (technical drawings).
GPT-6.1 Terra inachukua nafasi ya GPT-5.6 Terra, na imekaa katikati ya GPT-6 Luna yenye gharama ndogo na model zenye uwezo mkubwa zaidi, yaani GPT-6.1 Sol na GPT-6 Astra. Inatoa uwezo unaokaribiana na GPT-6.1 Sol huku gharama yake ya uendeshaji ikiwa takriban nusu ya ile ya Sol.
OpenAI imesema GPT-6.1 Terra inakamilisha kazi kwa kasi zaidi ya mara tatu kuliko GPT-6 Astra na GPT-6.1 Sol. Kwa watengeneza programu (developers), bei kwenye API ni dola 1 kwa kila tokeni milioni moja za kuingiza (input) na dola 5 kwa kila tokeni milioni moja za matokeo (output), ambayo ni nusu ya bei za GPT-6.1 Sol. Kwa watumiaji wa ChatGPT, kampuni inasema kiwango kilekile cha matumizi (usage allowance) kinaweza kukamilisha kazi nyingi zaidi kuliko GPT-5.6 Terra, na nyingi zaidi kwa kiasi kikubwa kuliko GPT-6.1 Sol au GPT-6 Astra.
Matokeo ya majaribio (benchmarks)
- Kwenye Agents’ Last Exam, kipimo cha kazi za kitaalamu, Terra iliishinda GPT-5.6 Terra kwa asilimia 15 (percentage points) zote zikitumia kiwango cha kati cha kufikiri (medium reasoning), huku ikigharimu takriban theluthi moja tu. Pia ililingana na GPT-6 Astra kwa bei ya moja ya kumi kwa kila tokeni.
- Kwenye kipimo cha ndani cha maswali yanayolenga kusababisha makosa, kiwango cha makosa cha Terra kilishuka hadi asilimia 16.7, kutoka asilimia 53.6 kwa GPT-5.6 Terra.
- Kwenye Terminal-Bench 4.0, kipimo cha coding kwa kutumia command-line, Terra ilitatua asilimia 50.3 ya kazi, ikilinganishwa na asilimia 21.5 kwa GPT-5.6 Terra.
- Kwenye MMMU-Pro, Terra inaizidi GPT-5.6 Terra katika kila kiwango cha kufikiri, na inakaribia GPT-6 Astra na GPT-6.1 Sol kwa gharama ndogo zaidi.
Hata hivyo, kwa kazi ngumu zaidi za coding, OpenAI inawashauri watumiaji kutumia GPT-6.1 Sol au GPT-6 Astra.
OpenAI ilisema Terra inafikia kiwango cha “Critical” katika usalama wa mtandao (cybersecurity) chini ya Preparedness Framework yake, na inaendelea kutumia kinga zilizotengenezwa kwa ajili ya GPT-6 Astra.
Watumiaji wa Plus, Pro, Enterprise na Edu wanaweza kuitumia modeli hii kwenye ChatGPT Work na Codex, na developers wanaweza kuifikia kupitia API kwa jina gpt-6.1-terra.
=================
source :OpenAI