Tetesi: Operation KAKUCHA yazaliwa Arusha baada ya UKUTA kuyeyuka

Status
Not open for further replies.
1472843421885.jpg
 
W
Ndugu Wanachadema Mkoa wa Arusha, sisi ni vijana wenye uchungu na chama chetu ndio maana tuko tayari kuipigania hata kuifia ili tupate ukombozi. Ni sisi tulikesha nje ya mahabusu alipowekwa ndani Kamanda Godbless Lema. Alivyoshinda siku tatu bila kula na sisi tulishinda naye bila kula.

Ndugu wanaChadema chama hiki kimejengwa kwa nguvu za umma yani sisi ndio maana CCM imefutika hapa Arusha. Hakipo.
Tuna uchungu sana. Hapa Arusha tumeshapigwa sana na Policcm tukitetea ukombozi. Wenzetu wameshatangulia mbele za haki. Mungu awarehemu. Yote ni kupigania ukombozi.

Ndugu zetu wanaChadema na Watanzania, hivi karibuni Kamati Kuu chini ya Kamanda Mbowe iliazimia tuandamane nchi nzima na mikutano kupinga Udikteta wa Serikali ya maCCM isiyotaka demolrasia, UKUTA ya Sept Mosi.

Vijana wa Arusha tulijiandaa vilivyo kupambana na Policcm endapo wangetuzuia hadi tone la mwisho la damu yetu. Tuko tayari kuifia haki na demokrasia. Dunia nzima ilijua ni siku ya ukombozi Tanzania.

Ndugu wanaChadema tumesikitishwa sana, tumeumizwa sana, tumefedheheshwa sana na kitendo cha Mbowe kwa hiari yake kusitisha maandamano hayo kwa madai eti ameombwa na viongozi wa dini na Lowassa naye ameombwa na familia ya Nyerere tuache kuandamana.

Ndugu wanaChadema, popote mlipo hata nje ya nchi tumechunguza hata kuongea na baadhi ya viongozi wa dini aliowataja Mbowe wamekataa hawakuongea naye hivyo Mbowe ni mwongo. Hata familia ya baba wa Taifa wamekataa hawakuongea chochote kuhusu Ukuta.

Tunatambua heshima ya Lowassa kwa chama. Lakini ni dhahiri Mbowe anamwogopa Lowassa. Lowassa bado ana maslahi binafsi na CCM ndio maana hapendi uharakati ambayo ndiyo asili ya Chadema na chama chochote cha upinzani. Tazameni Garbon.
Lowassa anatuletea siasa za Ccm. Anataka tufanane nao mafisadi. Arudi alikotoka.

Maandalizi ya UKUTA Sept 1 imegharimu chama mamilioni ya shilingi ilhali wilaya kibao hatuna ofisi, tumepanga na tunadaiwa kodi. Nani atarusisha fedha hizi?

Mbowe amelewa madaraka ya Uenyekiti wa Chadema. Sisi vijana kwa umoja wetu tunamtaka Mbowe na Lowassa wakae pembeni ili kamanda Lissu atuongoze. Hatuwezi kubembeleza haki yetu.
Tunamtaka aondoke na Lowassa wake atuachie chama. Kinyume cha hapo tumeamua kujichangisha fedha tutaenda kwa Msajili Dar es salaam atusajili kama CHADEMA-ASILI.

Akiondoka hata leo hatutafikia huko. Tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu. Vijana wengine wa mikoa mingine mtuunge mkono kama Singida na Kagera ambao nao Wako mbioni kutoa matamko.

Ahsanteni
John Ole Kaparo
Mwenyekiti wa Muda
Kamati ya Kudai Chadema Asili (KAKUCHA)
Jina lako hata ndani ya chadema tawi hautambuliki, nenda kwa maccm wenzako usijifanye wewe ni chadema
 
Labda aanzishe KADOLE na sio KAKUCHA

KADOLE kamati ya dodoma leo

Kamati hii kazi yake kubwa ni kusema uongo pale makao makuu sisiemu
 
Mnaanzaga hivihivi kugawanyika..endeleeni tu[emoji16]
 
Mkuu hivi unaaamini kabisa chadema kuna watu wenye think tank kubwa kweli

"kuna watu wenye think tank kubwa"

Hicho nini sasa? Kwani unafikiri think tank ni kama litanki likubwa linalokaa ndani ya kichwa? Alafu hapo nana wewe ndio kiongozi ndani ya chichiemu yenu hiyo? chaa! Hili taifa jamani, ni huzuni sana...
 
Ndugu Wanachadema Mkoa wa Arusha, sisi ni vijana wenye uchungu na chama chetu ndio maana tuko tayari kuipigania hata kuifia ili tupate ukombozi. Ni sisi tulikesha nje ya mahabusu alipowekwa ndani Kamanda Godbless Lema. Alivyoshinda siku tatu bila kula na sisi tulishinda naye bila kula.

Ndugu wanaChadema chama hiki kimejengwa kwa nguvu za umma yani sisi ndio maana CCM imefutika hapa Arusha. Hakipo.
Tuna uchungu sana. Hapa Arusha tumeshapigwa sana na Policcm tukitetea ukombozi. Wenzetu wameshatangulia mbele za haki. Mungu awarehemu. Yote ni kupigania ukombozi.

Ndugu zetu wanaChadema na Watanzania, hivi karibuni Kamati Kuu chini ya Kamanda Mbowe iliazimia tuandamane nchi nzima na mikutano kupinga Udikteta wa Serikali ya maCCM isiyotaka demolrasia, UKUTA ya Sept Mosi.

Vijana wa Arusha tulijiandaa vilivyo kupambana na Policcm endapo wangetuzuia hadi tone la mwisho la damu yetu. Tuko tayari kuifia haki na demokrasia. Dunia nzima ilijua ni siku ya ukombozi Tanzania.

Ndugu wanaChadema tumesikitishwa sana, tumeumizwa sana, tumefedheheshwa sana na kitendo cha Mbowe kwa hiari yake kusitisha maandamano hayo kwa madai eti ameombwa na viongozi wa dini na Lowassa naye ameombwa na familia ya Nyerere tuache kuandamana.

Ndugu wanaChadema, popote mlipo hata nje ya nchi tumechunguza hata kuongea na baadhi ya viongozi wa dini aliowataja Mbowe wamekataa hawakuongea naye hivyo Mbowe ni mwongo. Hata familia ya baba wa Taifa wamekataa hawakuongea chochote kuhusu Ukuta.

Tunatambua heshima ya Lowassa kwa chama. Lakini ni dhahiri Mbowe anamwogopa Lowassa. Lowassa bado ana maslahi binafsi na CCM ndio maana hapendi uharakati ambayo ndiyo asili ya Chadema na chama chochote cha upinzani. Tazameni Garbon.
Lowassa anatuletea siasa za Ccm. Anataka tufanane nao mafisadi. Arudi alikotoka.

Maandalizi ya UKUTA Sept 1 imegharimu chama mamilioni ya shilingi ilhali wilaya kibao hatuna ofisi, tumepanga na tunadaiwa kodi. Nani atarusisha fedha hizi?

Mbowe amelewa madaraka ya Uenyekiti wa Chadema. Sisi vijana kwa umoja wetu tunamtaka Mbowe na Lowassa wakae pembeni ili kamanda Lissu atuongoze. Hatuwezi kubembeleza haki yetu.
Tunamtaka aondoke na Lowassa wake atuachie chama. Kinyume cha hapo tumeamua kujichangisha fedha tutaenda kwa Msajili Dar es salaam atusajili kama CHADEMA-ASILI.

Akiondoka hata leo hatutafikia huko. Tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu. Vijana wengine wa mikoa mingine mtuunge mkono kama Singida na Kagera ambao nao Wako mbioni kutoa matamko.

Ahsanteni
John Ole Kaparo
Mwenyekiti wa Muda
Kamati ya Kudai Chadema Asili (KAKUCHA)
Upuuzi....ila poah wafu zikaneni!!!!
 
Hivi mmeshajua kiingereza au bado mnaleta ujinga humu??

To do you do you you say I do me

Huhuhuuu
 
Kwa nini ccm wamekuwa waoga kiasi hiki kwa ajili ya Lowasa Mbowe na CHADEMA. Je walishinda kweli hawa?
 
Uchochezi.
Uchochezi
Uchochezi.
Uchochezi.
Uchochezi.
Uchochezi huoooooooo.

Hatua kali zichukuliwe.
Hatutaki watu wa kuwashawishi watu matumizi ya nguvu wakati hii ni nchi ya amani na kuna vyombo vya sheria.
Uongozi wa Chadema na Jeshi la polisi wamtafuye huyu mchochezi ili iwe fundisho.
Awamu hii sio ya ile ya maandamano waliozoea Arusha.
Arusha ni kaeneo kadogo tu kasisababishe amani ya nchi ikatoweka.
Nasema huyu ni mchochezi. Rais wetu kama kweli hajaribiwi waanze na huyu mleta mada.
Amani ya nchi ni pamoja na kuwatia gerezani hawa wanaovuruga amani kwenye vyama vya siasa kwa kutoa matamko ya kichochezi.
 
Shairi ngonjera au
 
Hueleweki
Punbguza japo kidogo UPUUZI wa ki CCM hapa
Tunahitaji mjadala mkubwa kuhusu CHADEMA yetu lkn sio kutoka kwa wana UVCCM kama ww
Ona saa unavyo aibika tu
Ingekuwa ile JF ya zamani ww ungefukuzwa hapa kwa uongo
Wewe ni mwana UVCCM unaleta uchonganishi kwa habari za CHADEMA
 
[emoji23][emoji23][emoji23] hivi nyie vijana huwa mnapewa nini pale Lumumba?
Sio kwa kujitoa huku akili!

Wewe sio Mwanachadema,acha kutuharibia amani iliyopo ndani ya chama chetu.
CDM ilishafariki siku alipofanyiwa uhuni Dr Slaa!
 
Wanajamvi mpoooooo ....

Baada ya FUKUTO la kile kilichoitwa UKUTA kuingia mdudu .... baadhi ya wajiitao "Makamanda asili" wameanza VUGUVUGU la kudai chadema ileeeeeeeeeee ya miaka flani ambayo UFISADI ulipingwa kwa ngumi hadi mateke ..... kiasi cha MAJINA YA MAFISADI kuwekwa ktk tovuti .....

Kumekucha ngoja niagize BISI niendelee kuicheki hii SERIES EPISODE YA PILI
 
Kweli njaa inawaharibu akili vijana unaandika uzi viungo vyote umeviachia huku ukiagiza bisi ukisubiri matokeo ya umbea ulioupeleka nyumba ya pili utakuwaje...cha ajabu huyo msajili wa vyama hajui kama kuna kitu kinaitwa Chadema asilia
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom