Tetesi: Operation KAKUCHA yazaliwa Arusha baada ya UKUTA kuyeyuka

Tetesi: Operation KAKUCHA yazaliwa Arusha baada ya UKUTA kuyeyuka

Status
Not open for further replies.
Juzi tu mlileta habari kuwa vijana wa arusha wanaupinga UKUTA, Leo tena watu wale wale mnaleta habari kuwa vijana wa Arusha wanalalamika UKUTA kuhairishwa.

Hivi nyie uvccm mnadhani watu wote ni vichwa maji kama nyie?
Hawana tofauti na wajawazito, leo anakuagiza niletee Samaki, ukileta Samaki anakuambia no!! Ninahamu na pemba, baadae anakuambia au niletee kitimoto roast!
 
Mimi sijahakikisha ila ni taarifa toka Ra chuga huyo mwenye ametoa sina no yake kuhakikisha ndio maana nineweka tetesi
Mimi sijahakikisha ila ni taarifa toka Ra chuga huyo mwenye ametoa sina no yake kuhakikisha ndio maana nineweka tetesi
Naomba nikuulize, maswali mawili matatu, hivi shule umeishia la ngapi comrade, jamii forum umejiunga lini, unatumia akili au matope?
Wewe umeleta made hujaweka haya change, hata kama ni Tetesi ungeweka change, mf rafiki wa karibu.
Tambua kwamba jf we go with facts sio umbea wa uvccm, au bavicha, wengine humu hatuna vyama ila ni wazalendo halisi.
Next time kijana think beyond your nose, sawa kijana wa uv?
 
Juzi tu mlileta habari kuwa vijana wa arusha wanaupinga UKUTA, Leo tena watu wale wale mnaleta habari kuwa vijana wa Arusha wanalalamika UKUTA kuhairishwa.

Hivi nyie uvccm mnadhani watu wote ni vichwa maji kama nyie?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] hawa watu aliyewaroga kafa
 
Huyo kijana akawaulize vijana wa masaburi,kichapo tulochowapa pale Ubungo mwaka Jana,hatutaki upuuzi,kama hawaitaki CHADEMA waanzishe chama chao kingine,ujinga wa maccm kutumia jina la CHADEMA tumeuchoka,time hii hatutawapa kichapo tu tutawaua kabisa
 
Kwenu
JamiiForums
Invisible
Paw

Uzi huu umewekwa kama taarifa iliyokamilika, inasikitisha bila kuwa viambatanisho wala chanzo chake hakijulikani na wala hakuna kitu kinachoitwa KAKUCHA ndani au nje CHADEMA hapa mkoani Arusha na Tanzania kwa ujumla. Hivyo basi Kwa manufaa ya Jukwaa na wale wanaopenda kuona jukwa likiwa katika hali ya ushindani wa hoja kwa hoja na si majungu wala vijembe, ni afadhali uzi huu uondolewa / kufichwa hadi pale ukweli utakapobainika.
 
Ndugu Wanachadema Mkoa wa Arusha, sisi ni vijana wenye uchungu na chama chetu ndio maana tuko tayari kuipigania hata kuifia ili tupate ukombozi. Ni sisi tulikesha nje ya mahabusu alipowekwa ndani Kamanda Godbless Lema. Alivyoshinda siku tatu bila kula na sisi tulishinda naye bila kula.

Ndugu wanaChadema chama hiki kimejengwa kwa nguvu za umma yani sisi ndio maana CCM imefutika hapa Arusha. Hakipo.
Tuna uchungu sana. Hapa Arusha tumeshapigwa sana na Policcm tukitetea ukombozi. Wenzetu wameshatangulia mbele za haki. Mungu awarehemu. Yote ni kupigania ukombozi.

Ndugu zetu wanaChadema na Watanzania, hivi karibuni Kamati Kuu chini ya Kamanda Mbowe iliazimia tuandamane nchi nzima na mikutano kupinga Udikteta wa Serikali ya maCCM isiyotaka demolrasia, UKUTA ya Sept Mosi.

Vijana wa Arusha tulijiandaa vilivyo kupambana na Policcm endapo wangetuzuia hadi tone la mwisho la damu yetu. Tuko tayari kuifia haki na demokrasia. Dunia nzima ilijua ni siku ya ukombozi Tanzania.

Ndugu wanaChadema tumesikitishwa sana, tumeumizwa sana, tumefedheheshwa sana na kitendo cha Mbowe kwa hiari yake kusitisha maandamano hayo kwa madai eti ameombwa na viongozi wa dini na Lowassa naye ameombwa na familia ya Nyerere tuache kuandamana.

Ndugu wanaChadema, popote mlipo hata nje ya nchi tumechunguza hata kuongea na baadhi ya viongozi wa dini aliowataja Mbowe wamekataa hawakuongea naye hivyo Mbowe ni mwongo. Hata familia ya baba wa Taifa wamekataa hawakuongea chochote kuhusu Ukuta.

Tunatambua heshima ya Lowassa kwa chama. Lakini ni dhahiri Mbowe anamwogopa Lowassa. Lowassa bado ana maslahi binafsi na CCM ndio maana hapendi uharakati ambayo ndiyo asili ya Chadema na chama chochote cha upinzani. Tazameni Garbon.
Lowassa anatuletea siasa za Ccm. Anataka tufanane nao mafisadi. Arudi alikotoka.

Maandalizi ya UKUTA Sept 1 imegharimu chama mamilioni ya shilingi ilhali wilaya kibao hatuna ofisi, tumepanga na tunadaiwa kodi. Nani atarusisha fedha hizi?

Mbowe amelewa madaraka ya Uenyekiti wa Chadema. Sisi vijana kwa umoja wetu tunamtaka Mbowe na Lowassa wakae pembeni ili kamanda Lissu atuongoze. Hatuwezi kubembeleza haki yetu.
Tunamtaka aondoke na Lowassa wake atuachie chama. Kinyume cha hapo tumeamua kujichangisha fedha tutaenda kwa Msajili Dar es salaam atusajili kama CHADEMA-ASILI.

Akiondoka hata leo hatutafikia huko. Tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu. Vijana wengine wa mikoa mingine mtuunge mkono kama Singida na Kagera ambao nao Wako mbioni kutoa matamko.

Ahsanteni
John Ole Kaparo
Mwenyekiti wa Muda
Kamati ya Kudai Chadema Asili (KAKUCHA)
Nakubaliana sana na habari ya Lissu kuwa kiongozi mkuu wa CHADEMA lakini hayo mengine ya chadema asili ni upuuzi, Mbowe ameshatoa mchango wake inatosha, tujaribu akili nyingine na hiyo akili ni Tundu Lissu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom