Elections 2015 Operesheni Zinduka: Uamuzi Sahihi 2015

CCM hata wangemsimamisha Amina Salum Ali wangetangazwa washindi tu.

Hivi watu wanadhani haya mabadiliko ya [uteuzi wa makamishna] ya tume ya uchaguzi yaliyofanywa na mwenyekiti wa CCM ni ya bure tu?

Huo uteuzi hata mimi ulinipa mashaka, kwanza aliyekua mkurugenzi alipelekwa kwa majaji, msaidizi wake akapandishwa juu. Nasikia kwenye IT nako yamefanyika mabadiliko, kana kwamba haitoshi mwenyekiti anaaminihsa watu wauamini mfumo wa uchaguzi kwamba utakua wa haki na huru kwa kuwaahidi kwamba matokeo yatabandikwa vituoni.

Nahisi kuna kitu kikubwa sana kipo nyuma ya huu mpango mzima, suala la ushindi ni zaidi ya kura zitakazopigwa na wananchi.
 

Faza,

Mimi najihesabu kuwa ni mmoja wa anti-CCM wakubwa.

Na naombea washindwe vibaya mno hiyo tarehe 25, Oktoba.

Moyo wangu unataka CCM washindwe [na UKAWA washinde] lakini kichwa changu/ akili yangu inaniambia kwa jinsi mazingira ya sasa yalivyo, hilo tamanio langu kutimizika itakuwa vigumu sana.

Kwa hiyo natumaini unachokisema ni sahihi na kwamba CCM itabwagwa.

Lakini kila nikikishirikisha kichwa changu bado sioni hilo likitokea kwa sasa.

Sipendi kukosea ila kwenye hili nikikosea basi nitafurahi sana.

Yangu macho na subira tu kwa sasa.
 
Uchaguzi utakuwaje wa huru na haki wakati tume nzima imeundwa na mwenyekiti wa CCM ambaye chama chake pia kitashiriki huo uchaguzi?

Waache kutusi akili za watu.

Watu ndio kwanza ajira bado mpya na wanataka waonyeshe umashuhuri na nafasi yenyewe ndio hii kisha wapoteze? Huku wakijua kabisa hatma yao na bosi wao aliyewateua iko mikononi mwao?....hapo tuombee yatokee makosa ya kiufundi. Usijekushangaa tayari matokeo yapo mkononi watu wanafanya maandalizi ya namna ya kuyatangaza.
 
Waambie wana wa Israel wasonge mbele. Hayo ni maneno ya mungu kwa Musa. UKAWA tutasonga mbele na tutafika moja kwa moja. Eva ana taka kumpa Adam Tunda. Ushindwe.
 
Kaka yangu Mzee Mwanakijiji asante sana kwa moyo huu.Namshukuru Mungu kwa kukupa moyo wakuendelea kusimamia unachokiamini bila ksita japo umekua ukidharauliwa na kutukanwa na wanaodhani wana mapenzi na Tanzania zaidi yako.
Tuko pamoja na nina imani iko siku wanaokutusi iko siku watakuja kukuomba radhi.
Nazisubiri kwa hamu show zinazofuata nikiamini zitafungua macho ya walio wengi na kuiona picha halisi.

Lowassa ni balaa na Laana inayojaribu kuikumba Tanzania.
Roho inaniuma natamani hata kulia ninavyoona ndugu zetu wanavyokitamani kipande cha chupa wakidhani ni almasi.
Inauma kuona mtu aliye mchafu mbele ya Mungu na wanadamu akifikia hadi kupewa majina ya watakatifu na ya mitume watakatifu wa Mungu.
Uchaguzi wa mwaka huu shetani amejiinua na kuja kama malaika wa nuru na wengi wamevutiwa nae.
Eeh Mungu tunahitaji msaada wako tuepukane na hili balaa.
 
Last edited by a moderator:
Kadiri siku zinavyoenda mbele, Mwanakijiji ni kama anakuwa moko!
 

Dr.Mo, dude got paid to start this thread. Very sad.
 


Vuta subira mkuu jambazi anaibiwa na jambazi mwaka huu...

Unaposikia habari za kulishana sumu usidhani mchezo...
 

Ndio maana waliyakataa mapendekeo ya katiba mpya.
 

Kama ni kweli una sali, huna haja ya kuwatahadharisha watu juu ya mgombea, Mungu anajua na atatupatia rais. Ntashangaa sana kama una uwezo wa kujua uchafu wa Lowassa bila kuomba Mungu na ukitaka watu wakubaliane na mawazo yako. kila mamlaka iliyopo huwekwa kutoka juu.
 
Mpaka sasa sijaona mchango wa Mag3 njoo huku
Nianze kwa kukushukuru mwanga lutila kwa kunikumbuka, kumbe kuna watu wanafuatilia michango yangu! Kwa kweli nimefarijika sana kwa hili.

mwanga lutila, mimi nilianza kuipinga CCM tangu mfumo wa chama kimoja kwa imani na sababu kuwa mchawi na adui nambari one wa taifa hili ni CCM na leo, miaka zaidi ya 20 baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, bado naipinga CCM kwa imani na sababu ziile zile. Ajabu ya maajabu ni dai la Mzee Mwanakijiji kwamba ni sisi tumebadilika kimsimamo na sababu pekee ya kudai hivyo ni kukubali kwetu kumpokea Lowassa kuungana nasi katika hayo mapambano dhidi ya CCM.

mwanga lutila, naomba nikupe tu kionjo kwa kurudi nyuma hadi 13th February 2009 mwaka moja baada ya Lowassa kuwajibika na kujiuzul Uwaziri Mkuu kufuatia kashfa ya Richmond...msome kwa makini Mzee Mwanakijiji, nanukuu;

mwanga lutila, huu ndi ulikuwa ni mchango wangu kufuatia mada ya Mzee Mwanakijiji, nanukuu;
mwanga lutila, mwaka 2010 tulikuwa na uchaguzi mkuu na pamoja na kashfa zote na lawama zote kwa serikali ya chama tawala, CCM ilitangazwa kushinda uchaguzi na mgombea wake Jakaya Mrisho Kikwete kuongezewa awamu nyingine ya miaka mitano na leo tuko hapa tena. Mgombea wa Chadema mwaka huo alikuwa ni Dr. W. P. Slaa.

Swali la kujiuliza ni je hilo bonde la kashfa alilokuwa akiongelea Mzee Mwanakijiji bado lipo? Je anayeamua kutoka kwenye hilo bonde na kutafuta hewa safi huko nje ana kosa? Je kutoka kwa mtu moja ama wawili kunalitakasa hilo bonde? Je kwa nini kwa miaka minane baada ya Lowassa kujiuzulu tofauti lolote halikuweza kuonekana bondeni na badala yake kasi ya kashfa ndio ikaongezeka?

Mathalan, hivi kati yangu mimi, Mag3, na Mzee Mwanakijiji nani anaonekana amebadilika kimsimamo? Huyo Lowassa kama angeteuliwa kugombea Uraisi akiwa ndani ya hilo bonde ningempinga kama ninavyompinga Magufuli. Lowassa kaonesha ujasiri mkubwa kwa kulitosa hilo genge na kujiunga na sisi wana mabadiliko na tutamkaribisha mtu yeyote atakayeweza kuongeza nguvu katika hii vita; Tanzania bila CCM yawezekana.

Rejea: Taifa lililopiga kambi kwenye bonde la kashfa!
 

Nyie watu acheni unafki nilini mlianza kujua kuwa Lowasa ni Fisadi mayowe haya mnayopiga Yanatudhihirishia bila shaka mmekwiba sana kwenye hii NCHI sasa mnaona huyo jamaa akiingia madarakani Atawafanya vibaya huyo MM yuko kzn so Lazima atimize wajibu wa waliomtuma lkn asidhani km kuna MTU asietumia Utumbo kufikiri ataweza kuMbadilisha kwa hizo Ngano....zake wengine tulishaikataa CCM tangu 1995 sasa kuja na blah blah kama hizi nikupoteza Muda wengine tunazipitia hizi thread kwaajili yakuona Watu wazima wanavyojitoa ufahamu sababu Njaa.......
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…