Elections 2015 Operesheni Zinduka: Uamuzi Sahihi 2015

Huna maana,tatizo lako unafikiri bado una.ushawishi wako kama zamani. Kwa sasa tuna MZEE TUPATUPA WA LUMUMBA.
 

Na ndio hofu yangu kubwa kwamba huenda hata matokeo tayari wanayo mkononi kwa sababu safari hii ku coordinate fraud ni kazi sana na huenda isiwezekane. kinachoweza kutokea ni mtafaruku na mkanganyiko utakaopelekea watu kukubali yaishe tu. Huwezi kuamini hadi sasa hivi bado wataalam wa IT wanafanyia kazi hiyo system sasa sijui muda uliobaki utatosha kufanyia majaribio na kujiridhisha kama utakua unatimiza vigezo na masharti ikiwemo uwezo wa kuhudumia hiyo siku ya uchaguzi?

Nnachokifaham hawatakubali kushindwa kutoa matokeo kisa mitambo imegoma au mchakato haujaenda sawa, matokeo ni lazima yatoke kwa vyovyote vile yawe ya kupikwa, ya ukweli au ya ukweli kuchanganya na ya kupikwa. Tusubiri
 
u-salva rweyimumu
hukummbuki yeye salva alikipataje cheo chake?
 
 
Nitalijibu hili swali vile vile... stay tuned. Hatari sasa hivi ni zaidi ya CCM!

Nitasubiri jibu lako..pia utalazimika kuniambia kwa nini hatari hii unaizungumza baada ya Lowassa kuja kuwa mgombea wa UKAWA na haukuizungumza pale tu alipochukua fomu ya kugombea kupitia CCM ama alipoanza harakati alipokuwa CCM.Na je hatari hii ni akiwa UKAWA tu?
 



Nani ambae hayupo kwenye payroll ya CCM now?
CCM wanazidi onesha walivyo na uthubutu wa kumkamata yeyote 'ahamie' kwao
kuna thread ilisema Yericko nae kapewa milioni 72 ahamie CCM....it could be uwongo but you can imagine
 
Uchaguzi utakuwaje wa huru na haki wakati tume nzima imeundwa na mwenyekiti wa CCM ambaye chama chake pia kitashiriki huo uchaguzi?

Waache kutusi akili za watu.

Mkuu Uteuzi Kufanywa na Mwenyekiti Wa Chama Haiharalishi Uwepo wa Mbinu Za kupora Ushindi. Kumbuka Licha ya makamishinda Kuteuliwa na Mwenyekiti wa Chama lakini katika Mioyo Yao Inawezekana Kukawa na Utofauti Wa Kimsimamo na Rais. Siku Zote Kutanguliza neno kushindwa Katika Mapambano ni kujikatisha tamaa mapema.... Time will tell
 
Uchaguzi utakuwaje wa huru na haki wakati tume nzima imeundwa na mwenyekiti wa CCM ambaye chama chake pia kitashiriki huo uchaguzi?

Waache kutusi akili za watu.

Mimi kila wakati nakwambia NN Laiti kama CDM ndo ingekuwa CCM Kwanza kusingekuwa na chama cha siasa cha upinzani kinafanya siasa kwa UHURU kama ilivyo leo.Pili Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi angetoka Tengeru na angekuwa ndugu wa Mtei.Makamishina wote wa tume wangetoka moshi na kilimanjaro.CCM ni mbovu lakini kwa Tanzania CDM ni chama cha kizuzu na kibogus kuwahi kutokea.God forbid
 
Nani ambae hayupo kwenye payroll ya CCM now?
CCM wanazidi onesha walivyo na uthubutu wa kumkamata yeyote 'ahamie' kwao
kuna thread ilisema Yericko nae kapewa milioni 72 ahamie CCM....it could be uwongo but you can imagine

Naelewa kabisa.

Na hata kama siyo kweli, watu wanapata hiyo 'impression' hususan mtu kama Mwanakijiji anapokiri [albeit, indirectly] kwamba naye anapiga propaganda dhidi ya Lowassa na UKAWA kwa ujumla wake.

Yeye anaweza kudai kuwa anasimamia kanuni [jambo ambalo linaweza kuwa kweli au si kweli], lakini mbele ya watu wengine ataonekana ni kibaraka wa CCM.

But such is politics......
 

Unachosema ni kweli.

Lakini ni kweli pia kuwa, mwenyekiti wa CCM kuunda tume ya taifa ya uchaguzi halafu CCM nayo ni mshiriki wa chaguzi kunaleta mgongano mkubwa sana wa kimaslahi.

Na mtu huhitaji kuwa jiniasi kuuona huo mgongano.

Pia, hata ingekuwa mimi ndo mwenye mamlaka ya kuunda hiyo tume, ni wazi ningeweka watu ambao naamini watakuwa wanashabihiana nami kimtazamo na ambao wataweza kulinda maslahi yangu/ ya chama changu.

Ndo maana sehemu zingine wameamua kuwa na tume huru za uchaguzi.
 
Ameen!

Kuna mambo mengi natofautiana na Mwanakijiji, lakini katika hili, nakubaliana nae moja kwa moja. Ni hvibaya kuona ndugu zetu walikuwa brain washed in the name of mabadiliko, bila kujali mabadiliko wanayoahidiwa na hasi au chanya.

Acheni upotoshaji.... mabadiliko ni mabadiliko...
Ni ajabu kuendelea kutukuza nguo chakavu zinawaacha uchi na kuwadhalilisha ilhali mnao uwezo wa kujinunulia nguo mpya...!
Kipya kipya tu..!!
 
Hiyo contradiction wao hawaioni kabisa na hawawezi kuiona kwa sababu zilizo wazi. Na mimi hapa bado sijasema "mpigieni kura Magufuli". Miye ninachosema ni kile kile nilichokisema miaka nane sasa. Lakini naonekana nimebadilika!

Wazee wengi busara zikianza kuwaishia wanakuwa na hulka kama hizi za kwako... Wala si shangai!!
 

Na hilo ndio linalotakiwa kuwepo hapa Tanzania, lakini bila kubadili katiba ya Jamhuri ya Muangano wa Tanzania Hilo la tume huru litabaki kuwa Hadithi na Hata kama likikamilika bado Wateuliwa watakuwa na mapenzi na Vyama Husika na hilo litakuwa Tatizo Jingine..Bila Kubadili mfumo mzima wa kiutawala na Uongozi ni Hadithi kuwa na Tume huru na Hili linanipa ukakasi wa Kutilia mashaka matokeo ya Uchaguzi wa Oktoba 25.. Muda utatuambia
 
NN kuna jambo umesema kuhusiana na tume nitaandika baadaye kidogo uone kwanini bapo awali nilosema safari hii tume ni kisingizio siyo sababu ya upinzani kushindwa.
 

Haina kuremba, ungesikiliza huku ukitafuna big gii.
 
Usilete pumba hapa watu wameshaamua mabadiliko Mimi na umri wangu wote nmekua kada wa ccm nmekubali mabadiliko nakushangaa ww kijana

kazi kweli kweli. sijui hao vijana wa huko wako vepe! oops nimekosea.
 

du! mpelekeni mwenzenu muhimbili kuna kitengo cha moyo.
 
NN kuna jambo umesema kuhusiana na tume nitaandika baadaye kidogo uone kwanini bapo awali nilosema safari hii tume ni kisingizio siyo sababu ya upinzani kushindwa.

Daah we unadhan tume iko huru mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…