Elections 2015 Operesheni Zinduka: Uamuzi Sahihi 2015

Elections 2015 Operesheni Zinduka: Uamuzi Sahihi 2015

Duh Mzee Mwanakijiji what a waste of time....mbona hukuenda direct to the point? 12 minutes na hujaongea lolote bado. Dah!

Hivi ni lini wewe uliwahi kuwa upinzani...lini? Ni lini wewe ulitaka mabadiliko?

Dakia 5:24 "wengi ambao hawajui, miaka 20 sasa nimekuwa kwenye harakati hizi..."

Dakika 5:51, "..tuliunga upinzani wakati ule na tumeendelea kufanya hivyo. Pamoja na kwamba tuliamini kwamba labda kwa kufanya hivyo chama ambacho kilikuwa kimeleta uhuru Tanzania kingeweza kubadilika lakini hakijabadilika jinsi ambavyo tulikuwa tumetarajia. Labda safari hii kinaweza kikabadilika…"

- Mzee wangu, kwa miaka zaidi ya 50 tumekuwa tukisema hayo hayo unayoyaongea, "labda safari hii kinaweza kikabadilika..." labda..labda..labda...na hakuna siku wamewahi kubadilika!

- Ubaya wa Lowassa ni upi huo ambao mlipokuwa naye mlimuunga mkono kuliko watangaza nia wote waliokuwa kwenye kinyang'anyiro ila sasa amekuwa mbaya kuko Hashim Rungwe (no offence intended)?

- Unataka tena kuja hapa baada ya miaka mitano kutueleza ni kwa namna gani tumejaribu jaribu kuleta upinzani na mwaka 2015 tuliona LABDA watabadilika?

MWISHO: kwenye video zako zitakazofuata tafadhali tafuta mtaalamu akusaidie kwenye speech yako..punguza maneno yasiyo na mantiki. hizi ""eeh" "aaah"! Ninaamini ulijiandaa na uliiandaa speech kabla ya ku-rekodi. Inapoteza ladha kusikiliza! Inakaa kama unawaza kwa kadri unavyozidi kuongea. Go straight to YOUR point..!

Nashukuru.

Last edited by a moderator:
hahahahahahhaahhahaahahahhahahahaahahahahha.....Comedy of the century
 
Unapoamua kufanya hii operesheni Zinduka ili kuwashawishi watu wasimpigie kura Lowassa pia kumbuka kuwaambia wampigie nani...ili at least tujue umesimana wapi.

Mimi nilidhani kwa sasa tungejaribu kudiscuss issues na sio mtu mmojammoja.

Lowassa ni "Issue"...sio mtu "mmoja mmoja"
 
Wadau mlipaswa kuping/kujibu hoja..wengi humu wameanza kujihami kabla hata ya kusikiliza hoja...inasikitisha sana
 
Usilete pumba hapa watu wameshaamua mabadiliko Mimi na umri wangu wote nmekua kada wa ccm nmekubali mabadiliko nakushangaa ww kijana
 
Naona kama MMKJ anaanza kuchanganyikiwa, watu wako wako field yeye yuko Marekani anajirekodi chumbani halafu anategemea watu wa Loliondo kijijini wazinduke kwa video.
 
Umechelewa sana,, hauna jipya la kushawishi watanzania. Usifikiri watanzania ni mazuzu. Yapo mengi ya kudiscuss kuleta maendeleo Tz sio huu unafiki wako tena.

Ni bora CCM ikaondoka sasa hv hata kwa miaka mitano tu. Lakini mfumo uvurugike kabisa tuwe na mfumo mpya wa uongozi Tanzania.

Hamna mabadiliko yoyote tutakayopata ndani CCM. Sielewi nini ambacho unashawishi watanzania. Na kama si Lowasa ummeseme kiongozi mwingine tofauti na CCM. Tofauti na hapo wewe utakuwa msaliti mkubwa wa mageuzi ndani ya nchi yetu.
 
Mzee Mwanakijij

Mzee Mwanakijiji hoja zako za kupingana na Lowassa kusimamishwa na chama / vyama ambavyo watanzania wanategemea kuwa ndio nguzo ya kubadili uongozi na think-tank ya uongozi ni nzuri na kiuhalisia binafsi najiuliza maswali kadhaa. Baadhi ni haya
1. Tunaposema Rais hafanyi kazi yake ipasavyo, je huwa ni yeye kama Rais au Taasisi nzima ya urais.
2. Rais na Taasisi ya urais ni vitu viwili vinavyofanya kazi kwa pomoja na kutoa taaswira moja. Je pale Rais anapokuwa na tatizo /dosari ila Taasisi ya urais ikawa imara. Je taaswira ya kazi ya Rais huwa nzuri au mbaya? .

3. Baraza la mawaziri ndilo linalofanya kazi kwa ukaribu na Rais. Uimara wa baraza hili au ubovu wake unaathiri vipi utendaji wa Rais? Assume Rais ni mzuri kiutendaji au mbaya kiutendaji au ana tatizo lingine lelote lile.

4. Chukulia ameshinda Rais toka chama cha Mapinduzi, je baraza Lake la mawaziri litakavyosukwa litakuwa tofauti kwa kiasi gani na baraza /mabaraza yaliyokuwepo kiutendaji kwa kuzingatia wale watakaoteuliwa (individual person) na miongozo iliyokuwepo chini ya serikali inayomaliza muda wake.
Pia Chukulia akashinda Rais kutoka upinzani mathalani Lowassa. Baraza Lake litakuwaje (components) na miongozo itakayotumika bila kusahau think tank itakayohusishwa katika uongozi. Je sio kuwarudia wabunge wale wale ambao unakiri kuwa wamejengwa katika upinzani unaowakubali?

5. Je tuchague Rais mchapakazi na mwenye maamuzi ya kukurupuka atakayekuwa na baraza la mawaziri na think tank ile ile iliyotufikisha hapa kwa milongo kadhaa ambayo utendaji wake hata wewe ulikuwa ukiukosoa au
Tuchague Rais mwenye afya dhaifu (kama wanavyosema Wana CCM) lakini mwenye kuchukua maamuzi yanayofuata sheria na aje na baraza jipya na think tank mpya katika mfumo mpya?

Kwa sasa naomba niishie hapo kwanza.
 
Last edited by a moderator:
mzee hatukutishi bali tunakuambia ukweli msijaribu kucheza na mabomu ambayo alarm imeshaanza kutowa mlio!
kama mlikuwa mnasikia kwa majirani sasa alarm inalia hapa kwetu ole wenu ole wenu vijana hatutarudi nyuma na hamtaweza kuturudisha nyuma me mwenyewe moyo wangu unakaribia kupasuka kwakuona unacho jaribu kutaka kutuaminisha kitu ambacho hakina faida na TANZANIA !!
 
Mzee Mwanakijiji usijiche kwenye keyboard. Anza kwa kujitambulisha jina lako halisi, kisha panda jukwaani. Kama una uwezo huo.

Mzee Mwanakijiji yuko nyuma ya keyboard anazindua operation kwa watu walio na uelewa mkubwa mzee kapiga chaka, peleka operatio zinduka na maeneo mengine ambayo hayana access na internet. Bibi yangu kule Dongobesh atapataje mawazo yako na yeye ameamua MABADILIKO!!!!!!

Walengwa hasa wa maudhui yake sijui ni nani, mwishowe hii story lazima iishie kwa kusema msimulizi hakufanikiwa kuleta ujumbe kwa jamii.
 
Kuna kitu ambacho wengi hamkielewi kwa vile si wamoja wetu huku Site waTz wameshaamua wampigie nani kati ya ENL na JPM ni asilimia chache sana almost zero hawajaamua!so don't waste your time and energy MMK. Kama humu JF ndio kabisa sidhani kama kuna mtu utamshawishi
 
Duh Mzee Mwanakijiji what a waste of time....mbona hukuenda direct to the point? 12 minutes na hujaongea lolote bado. Dah!

Hivi ni lini wewe uliwahi kuwa upinzani...lini? Ni lini wewe ulitaka mabadiliko?

Dakia 5:24 "wengi ambao hawajui, miaka 20 sasa nimekuwa kwenye harakati hizi..."

Dakika 5:51, "..tuliunga upinzani wakati ule na tumeendelea kufanya hivyo. Pamoja na kwamba tuliamini kwamba labda kwa kufanya hivyo chama ambacho kilikuwa kimeleta uhuru Tanzania kingeweza kubadilika lakini hakijabadilika jinsi ambavyo tulikuwa tumetarajia. Labda safari hii kinaweza kikabadilika…"

- Mzee wangu, kwa miaka zaidi ya 50 tumekuwa tukisema hayo hayo unayoyaongea, "labda safari hii kinaweza kikabadilika..." labda..labda..labda...na hakuna siku wamewahi kubadilika!

- Ubaya wa Lowassa ni upi huo ambao mlipokuwa naye mlimuunga mkono kuliko watangaza nia wote waliokuwa kwenye kinyang'anyiro ila sasa amekuwa mbaya kuko Hashim Rungwe (no offence intended)?

- Unataka tena kuja hapa baada ya miaka mitano kutueleza ni kwa namna gani tumejaribu jaribu kuleta upinzani na mwaka 2015 tuliona LABDA watabadilika?

MWISHO: kwenye video zako zitakazofuata tafadhali tafuta mtaalamu akusaidie kwenye speech yako..punguza maneno yasiyo na mantiki. hizi ""eeh" "aaah"! Ninaamini ulijiandaa na uliiandaa speech kabla ya ku-rekodi. Inapoteza ladha kusikiliza! Inakaa kama unawaza kwa kadri unavyozidi kuongea. Go straight to YOUR point..!

Nashukuru.

Huyu mwenzetu nadhani alikuwa anajielewawna anaelewa na kwenda wapi pomoja na watanzania wengine wanaona mfumo unaotuongoza hauja fanya vyema kama inavyostahili lakini ghafla katikati ya safari ameshika bumbuazi na kupoteza muelekeo lakini bado yuko mbele kuongoza safari na pale anapokumbushwa na wenzake kuwa ameshikwa bumbuazi anabisha na kukataa.
Ngoja tuendelee kusikiliza anachotuletea kwani ni haki ya kila mtanzania kusikilizwa
 
Last edited by a moderator:
Nasubiri kwa hamu sana baada ya 2016, naamini Mwanakijiji ndiye atakuwa mllamikaji mkubwa humu kuhusu hilo chaguo unalolipigia debe. Mark my words!!?
 
Sikuwahi kuwa fan wa Lowassa siku za nyuma, lakini kila siku navutika kwake kwa sababu ya watu kama MMM.

Kwanini kila siku ni Lowassa? Hii nguvu kubwa ya kumpinga Lowassa ni ya nini? Hofu ya watu kwa Lowassa ni nini? Is he an immortal being or what? Kwani akiwa rais si kama ilivyokuwa kwa Mwinyi, Mkapa, Kikwete na kwamba atapita kama wengine walivyopita? Kama ndivyo, then what is all this fuss about??
 
KinachoShangaza ni kuwa watu wanataka tuamini watu wengi watamchagua Lowassa. Lakini inaonekana hawaamini hilo ni kweli. Kama ni kweli hoja zangu hazina wasikilizaji na hazimbadili yeyote hivyo ni za kupuuzia. Hampuuzii mnaomtaka Lowassa kwanini?

Nitajibu: kwa sababu hamuamini Lowassa atakubaliwa na wengi kama mnavyotamani.
 
Sikuwahi kuwa fan wa Lowassa siku za nyuma, lakini kila siku navutika kwake kwa sababu ya watu kama MMM.

Kwanini kila siku ni Lowassa? Hii nguvu kubwa ya kumpinga Lowassa ni ya nini? Hofu ya watu kwa Lowassa ni nini? Is he an immortal being or what? Kwani akiwa rais si kama ilivyokuwa kwa Mwinyi, Mkapa, Kikwete na kwamba atapita kama wengine walivyopita? Kama ndivyo, then what is all this fuss about??

Liulize hili swali kivingine..nguvu kubwa ya kumsukumizabLowassabkwa Watanzania ya nini na kwanini? Ukipata jibu la swali hili utapata na jibu lako.
 
Back
Top Bottom