Mzee Mwanakijij
Mzee Mwanakijiji hoja zako za kupingana na Lowassa kusimamishwa na chama / vyama ambavyo watanzania wanategemea kuwa ndio nguzo ya kubadili uongozi na think-tank ya uongozi ni nzuri na kiuhalisia binafsi najiuliza maswali kadhaa. Baadhi ni haya
1. Tunaposema Rais hafanyi kazi yake ipasavyo, je huwa ni yeye kama Rais au Taasisi nzima ya urais.
2. Rais na Taasisi ya urais ni vitu viwili vinavyofanya kazi kwa pomoja na kutoa taaswira moja. Je pale Rais anapokuwa na tatizo /dosari ila Taasisi ya urais ikawa imara. Je taaswira ya kazi ya Rais huwa nzuri au mbaya? .
3. Baraza la mawaziri ndilo linalofanya kazi kwa ukaribu na Rais. Uimara wa baraza hili au ubovu wake unaathiri vipi utendaji wa Rais? Assume Rais ni mzuri kiutendaji au mbaya kiutendaji au ana tatizo lingine lelote lile.
4. Chukulia ameshinda Rais toka chama cha Mapinduzi, je baraza Lake la mawaziri litakavyosukwa litakuwa tofauti kwa kiasi gani na baraza /mabaraza yaliyokuwepo kiutendaji kwa kuzingatia wale watakaoteuliwa (individual person) na miongozo iliyokuwepo chini ya serikali inayomaliza muda wake.
Pia Chukulia akashinda Rais kutoka upinzani mathalani Lowassa. Baraza Lake litakuwaje (components) na miongozo itakayotumika bila kusahau think tank itakayohusishwa katika uongozi. Je sio kuwarudia wabunge wale wale ambao unakiri kuwa wamejengwa katika upinzani unaowakubali?
5. Je tuchague Rais mchapakazi na mwenye maamuzi ya kukurupuka atakayekuwa na baraza la mawaziri na think tank ile ile iliyotufikisha hapa kwa milongo kadhaa ambayo utendaji wake hata wewe ulikuwa ukiukosoa au
Tuchague Rais mwenye afya dhaifu (kama wanavyosema Wana CCM) lakini mwenye kuchukua maamuzi yanayofuata sheria na aje na baraza jipya na think tank mpya katika mfumo mpya?
Kwa sasa naomba niishie hapo kwanza.