The most useless thing I know to date
Mwanakijiji nakuhakikishia, hata utushawishi vipi, ushawishi wako ni bure kabisa. Sisi tunaoelewa hila na janja zako tumeshazielewa na hatubabaishwi na harakati zako za kipuuzi. Mimi nimeamua kwamba Oktoba 25 2015, alfajiri na mapema kama ilivyokuwa mwaka 2010 nitakuwa wa kwanza kumpigia mgombea wa upinzani na safari hii ni Edward Lowassa. Hata upinzani ungekuwa umesimamisha JIWE BADO NINGECHAGUA JIWE.
Wewe unaishi Marekani lkn bado uelewa wako mdogo sana, hukuona katika chaguzi wa Marekani katika majimbo ya Blue (Democrats) na Nyekundu (Republicans) wanachagua chama tuuuuu hawachagui chama pinzani. Sasa unayetaka kutuhujumu sisi ukiwa ugaibuni unataka kutuambia nini?
Mwaka 2010, nilimchagua Dr Slaa, kwa dhati kabisa kwa sababu mimi ni mwana mageuzi na nilikuwa mtu wa kwanza kupiga kura ktk kituo changu. Na mwaka huu Mungu anipe nguvu na uhai bado nitajihimu asubuhi na mapema ili kumpigia Ndugu Edward Lowassa na madiwani na wabunge wa UKAWA (yaani CHADEMA, CUF NCCR na NLD).
Wewe huna maana ya kuwaghilibu watanzania kwa kununuliwa na CCM. Tuache sisi na Lowassa wetu na hata ukikazana sana bado hutamweza. Kumbuka Watanzania wa mabadiliko toka jana, leo na hata kesho watachagua mabadiiko tu. Si vinginevyo.
Tunataka tuachane na ghiliba za CCM kwa gharama yoyote na Lowassa ni njia tu ya kufika huko. Kwa hivyo hatudanganyiki. Kama wewe umenunulika basi lakini tunaoelewa maana ya siasa ya ushindani hatuwezi kudanganyika kirahisi kihivyo.
MIMI nilitegemea utatupa uzoefu na ujanja wa nchi za magharibi kama Marekani unayoishi kumbe lengo lako ni kutaka kutuhadaa Watanzania kutoka kwenye agenda ya uchaguzi na kutuletea maneno ya mtaani.
Kumbuka Watanzania hatuchagua MALAIKA awe rais wa Tanzania. Tunachagua binaamu awe rais wa Tanzania. Na binadamu huyo aweza kuwa Ndg. Lowassa au Magufuli. Hakuna katika hao au hata ningekuwa mimi atakayekosa dosari. Au chukulia uwe wewe ndio mgombea wetu bado ungekuwa na dosari nyingi tu. Kwa hiyo, suala la kutuambia kuwa eti Magufuli ni nafuu halina maana halina nafasi hapa.
Kama wewe umem-feel sana Magufuli mchague wewe na ukoo wako. Waache watanzania wachague Tanzania wanayotaka. Wewe umechagua Marekani lakini sisi tumechagua mama Tanzania. Tunaipenda sana kwa dhati kabisa.
Munu ibariki mama Tanzania na Mungu umtie nguvu na uwape mioyo wa ushindi Ndugu Edward Lowassa na Watanzania wote wa mabadiliko.