ToniXrated
JF-Expert Member
- Sep 21, 2022
- 1,134
- 2,993
Igweeee igweeee!!
Nimekaa nikitafakari jinsi gani tunakosa mawakala wa kuwavusha wachezaji wetu kwenda kucheza soka la kulipwa barani Ulaya na Marekani. Nchi yetu imebarikiwa kuwa na mchezaji mahiri sana katika soka la wanawake naye si mwingine bali ni muwindaji wa magoli, Oppah Clement.
Huyu binti hastahili kucheza soka la kulipwa hapa barani Afrika. Anastahili kuzitumikia timu kubwa duniani katika upande wa soka la wanawake kama vile Bayern Munich, Barcelona,Chelsea,Lyon,PSG au Real Madrid.
Swali langu ni kwa Mawakala wa wanamichezo, hivi hamuoni hii lulu inayozagaa matopeni? Oppa angekuwa anatokea nchi za Afrika Magharibi sasa hivi tungekuwa tunazungumzia mengine! Huenda angekuwa anacheza katika mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya, UEFA kwa upande wa soka la wanawake.