Opportunity ya kazi kwa wabongo wanaoishi Afrika Kusini

Opportunity ya kazi kwa wabongo wanaoishi Afrika Kusini

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Habari zenu ndugu zangu, ama baada ya salam ningependa kujielekeza kwenye mada husika. Mimi ni mbongo ninaeishi hapa Afrika Kusini, kuna salon nimefungua, so nahitaji vinyozi watatu wenye sifa tatu.

1) sifa ya kwanza kinyozi awe na uzoefu wa kutosha wa kazi hii, na awe anajua kunyoa style mbali mbali.

2) sifa ya pili kinyozi awe mcheshi na mwenye kujua kuongea vizuri na wateja ( hapa haijalishi lugha) lkn pia unaweza kuwa haujui lugha ila ukawa unaonesha sura ya bashasha (tabasamu) kwa wateja wakakufurahia na kukupenda.

3) tatu kinyozi awe msafi muda wote, yan kuanzia kwake yeye mpaka kwa sehemu anayofanyia kazi.

Saluni ipo Fuller Street namba 2, Betrams (karibu na Spar) Johannesburg. Saluni bado mpya na tunaendelea na matengenezo, kwahiyo kama mtu yupo tayari ani PM.

Kama nikikosa wa hapa karibu basi hata wa mbali kutoka Tanzania, Burundi, Rwanda au Congo mnakaribishwa, lkn gharama zote za kufika hapa utafanya mwenyewe.

Mi nitachofanya (kama hauna mwenyeji) ni kukupokea na kukupa sehem ya kuanzia maisha. Karibuni

IMG-20210526-WA0005.jpg


IMG-20210526-WA0001.jpg
 
Ungekuwa Chaka huku Cape town Vinyozi wazuri kibao,Labda ungeshindana nao kwa Masharti hasa hilo la usafi.
Hahaha.. usafi huwa ni changamoto kubwa kwa vijana wengi wa saluni. Ila wakiwa kwang watajifunza tu.
 
Kwani nauli ngap mpaka south
Kabla ya corona ilikuwa Dar to Harare ni sh 1,30000, na kutoka Harare to J'burg ni Rand 350 ambapo ilikuwa sawa na sh 50,000. Ila kwa sasa sifahamu labda kama unaishi Dar uende pale k'koo yanapopatikana mabasi ya kuelekea Zimbabwe uulize. Kuhusu nauli ya kutoka Harare to J'burg pia unaweza kuulizia hapo hapo maana stand yao ni moja kwahiyo madereva wengi wanafaham na wanaweza kukusaidia kwa safari. Kikubwa uwe na document za kueleweka zikiwemo kadi za vipimo vya magonjwa nk.
 
Kaka hiyo ndio saloon ya kujisifia unasema mpya haina ubora kabisa Dah ww wacha tu Mungu akusaidie.
Nimesema bado ipo katika matengenezo mkuu, haijaanza kazi ndo maana bado nahitaji watu. Pia hamna sehem niliyojisifu zaidi ya kusema nahitaji wafanya kazi wa saloni, hasa kwa wabongo wanaoishi hapa. Au kuzungumzia swala la usafi wa sehem ya kufanyia kazi nako ni kujisifia?
 
Malipo tunaelewana mkuu. Ila utaratibu wa malipo huwa ni wa kiti. Nakupa kiti kimoja unanilipa kwa wiki.
Ha ha ha. Hapo haijalishi Kuna wateja au la? Hapo huitaji wafanyakazi bali business partner.
NB: Mfanyakazi means Mshahara
 
Kabla ya corona ilikuwa Dar to Harare ni sh 1,30000, na kutoka Harare to J'burg ni Rand 350 ambapo ilikuwa sawa na sh 50,000. Ila kwa sasa sifahamu labda kama unaishi Dar uende pale k'koo yanapopatikana mabasi ya kuelekea Zimbabwe uulize. Kuhusu nauli ya kutoka Harare to J'burg pia unaweza kuulizia hapo hapo maana stand yao ni moja kwahiyo madereva wengi wanafaham na wanaweza kukusaidia kwa safari. Kikubwa uwe na document za kueleweka zikiwemo kadi za vipimo vya magonjwa nk.
+ COVID test = 50 USD [123,500 TZS] ndani ya masaa 72 kabla ya Safari. Kama unasafr na basi itabd upime Tena njian maana safari ya Dar-joburg Ni zaidi ya masaa 72.
 
Ha ha ha. Hapo haijalishi Kuna wateja au la? Hapo huitaji wafanyakazi bali business partner.
NB: Mfanyakazi means Mshahara
Mkuu mbona salon nyingi watu wanafanya kazi kwa mfumo huu. Fikiria mfano unaingiza sh elf 25 kwa siku, ina maana kwa wiki una 175000. Mimi ukinilipa elf 50 ya kiti ww ukibaki na 125000 tatizo liko wapi, na kwa style hii unafikiri ni nani atakuwa katengeneza pesa ndefu zaidi ya mwenzake kati ya boss na mfanyakazi. Kuhusu wateja kazi yoyote ukiwa na uzoefu nayo plus usafi na uchangamfu basi nakuhakikishia kuwa utapata wateja tu tena kutoka sehem mbali mbali.
 
Ila **** mijitu ina roho mbaya uko hata sijawahi kujua ni kwanini!!!!

Yanachagua kazi za kufanya halafu wabongo wakiwa wanazifanya kazi ambayo wao hawazipendi wanawajengea chuki na kuchoma maduka[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom