Oreshnik: Silaha mpya tishio iliyotumiwa na Urusi. Hakuna mfumo unaweza kuzuia duniani, isipokuwa S550 wa Urusi wenyewe

Oreshnik: Silaha mpya tishio iliyotumiwa na Urusi. Hakuna mfumo unaweza kuzuia duniani, isipokuwa S550 wa Urusi wenyewe

Mbona Ukraine wamepoa hawajaendelea tena kutumia silaha zao za masafa marefu baada ya jaribio hilo moja tu?
Bado wanaandaa mashambulizi, unajua vita ya siku hizi mpaka aambiwe USA, ndio wanapiga. Iran ilipotaka kurusha yale ma baloon kule Israel walimjulisha USA kwanza kisha wakarusha, na Israel naye alipotaka kulipiza walijadiliana na USA kwanza na wakaelekezwa apige wapi na atumie nini kupiga.

Hivyo naamini hata hawa Ukraene naona wanatafuta line USA bado bussy, unreachable. Wakiipata mawasiliano utasikia wanatoa taarifa za kujibu.

Nilitaka kukutoa wasiwasi tu kwamba watajibu uwe na subira.
 
Nami nikutoe wasiwasi tu nayajua yote hayo, tena pengine katika kiwango cha kukuzidi.

Na maamuzi yote yatafanyika baada ya kikao cha dharura cha NATO hiyo Jumanne ambacho kitajadili majaribio ya silaha mpya kutokea Urusi.
Good Day
 
Kwahio zile carrier zinazamishika
Carrier sio kisiwa kwamba kipo sehemu moja. Ziko majini zinatembea muda wote inabidi uwe na CEP ndogo sana uweze kuzipiga. Sasa kutokana na speed kubwa inayokuwa kwa hypersonic missile, kuna joto kubwa sana linakuwa generated kwa skin ya kombora hadi ukitumia aluminium au steel inayeyuka. Joto lile haliruhusu electronics ndani. Hivyo hypersonic missile sio accurate enough kupiga moving target.
 
Putin katawala Urusi kwa miaka 24 sasa ila hajafanya mambo makubwa hata 30% ya aliyofanya Hitler ndani ya miaka yake 12 Ujerumani.
Ndio utuambie Hitler kafanya nini cha akili? ,unajua Putin alikuta Russia kwenye hali gani? Mpaka sasa Russia imekuwa nchi yenye uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi kushinda hata German?
 
Yaani mpaka Leo Urusi imeshindwa kufumua hako kainchi, iemishiwa na makombora hadi Sasa imehamia ICBM ambazo ni gharama sana na hupaswa kutumika pale nchi imeshindwa namna yote, Sasa hizo ICBM zikidunguliwa ndio basi hakutakua na kete nyingine.
Makobaz sijui mtahamia kwa nani maana Iran nayo ilifanyiwa aibu juzi
 
Kisayansi hamuna kitu kama hicho
Someni Newtons Laws of Motion
He! we bado uko kwenye Newtons laws of motion! Vijana wamevuka huko. Habari ya mjini ni AI na uchafu mwingine.
Any way we baki huko bado.
 
Ndio utuambie Hitler kafanya nini cha akili? ,unajua Putin alikuta Russia kwenye hali gani? Mpaka sasa Russia imekuwa nchi yenye uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi kushinda hata German?
Ukimlinganisha Putin na viongozi wengi wa Ulaya kawaacha mbali sana.

Tangu kuanguka kwa Soviet Union Putin ndiye raisi ambaye amekuja kuinyanyua sana kiuchumi Russia
 
Carrier sio kisiwa kwamba kipo sehemu moja. Ziko majini zinatembea muda wote inabidi uwe na CEP ndogo sana uweze kuzipiga. Sasa kutokana na speed kubwa inayokuwa kwa hypersonic missile, kuna joto kubwa sana linakuwa generated kwa skin ya kombora hadi ukitumia aluminium au steel inayeyuka. Joto lile haliruhusu electronics ndani. Hivyo hypersonic missile sio accurate enough kupiga moving target.
Jidanganye, ndiyo maana wazungu wameshangazwa na silaha mpya,tech Ina surprises nyingi
 
Mach 10 badili kwenda kwenye Km/s.
Nenda Google andika "Convert Mach 10 to km/s".
Wabongo kwa ujuaji na ubishi tupo vizuri.
Anyway, seeing is believing. Jionee mwenyewe. Kasome makala huko BBC, CNN, Forbes, RT, Sputinik, n.k. kuhusu hilo tukio na hiyo speed ya Mach 10.
Watu si wajuaji mkuu kuna kipindi niliwahi mwambia mtu habari za SR-71 Blackbird speed yake akabisha mno tuliingia hadi google hakubadili msimamo akisema habari za kutunga. Nilijisemea tu sisi ndo wakuunda hata capacitor tu ikiwa huyo msomi tu kumbadilishia hiyo mach number kwenda kwenye km/hr anasema hakuna speed kama hiyo.
 
Marekani yapewa taarifa na Russia dakika 30 kabla, Ukraine na washirika wake washindwa kuizuia.

Ina uwezo wa kufika na kuangamiza mahali popote Ulaya nzima.

Hakuna mfumo wa kuizuia.

Ni Hypersonic hivyo inaweza kusafiri kwa kasi ya Mach 10 (kilometa 3 kwa sekunde, huwezi kuiona muenendo wake wa kasi kwa macho).

Inabeba vichwa vingi kwa mara moja ambavyo vikitawanyika huko angani kila kimoja kinaweza kujiongoza kufuata 'target' yake sehemu tofauti na vichwa vingine.

Russia imesema itakuwa inatoa taarifa kabla haijafanya shambulizi, tahadhari kwa raia eneo inalotaka kulishambulia waweze kuondoka lengo likiwa kupunguza maafa kwa raia wasiokuwa na hatia.

Muelekeo wa vita kati ya Ukraine na Russia umechukua sura mpya baada washirika wa Ukraine kuruhusu silaha za masafa marefu walizo wapa Ukraine zitumike kushambulia ndani ya ardhi ya Russia inayotambuliwa kimataifa.

Baada ya Ukraine kuzitumia hivi karibuni Russia amejibu mapigo kwa kuifanyia majaribio silaha yake mpya Oreshnik.

Ni teknolojia mpya ya Hypersonic Intermediate range ballistic missile.

Ina uwezo wa kubeba vichwa vya nyukilia (nuclear payload), kwa sasa imetumia vilipuzi vya kawaida(conventional bomb) lengo kutoa onyo tu. Pentagon wakiri silaha hiyo ni tishio lakini wana amini Ukraine itaweza kuhimili maafa yake.

Naomba wale wadau wa mambo ya silaha waje watoe maoni yao. Narudia, wale wadau wanaojua mambo ya silaha siyo shabiki wa vita vya Ukraine au NATO na Russia.

CC: T14 Armata waite wadau wengine tujadili wengine tujifunze.
Stori za vijiweni hizi
 
Yaani mpaka Leo Urusi imeshindwa kufumua hako kainchi, iemishiwa na makombora hadi Sasa imehamia ICBM ambazo ni gharama sana na hupaswa kutumika pale nchi imeshindwa namna yote, Sasa hizo ICBM zikidunguliwa ndio basi hakutakua na kete nyingine.
Makobaz sijui mtahamia kwa nani maana Iran nayo ilifanyiwa aibu juzi
Zelensky amefanikiwa kukulisha uongo ambao umekanushwa na Pentagon.
Fuatilia press ya Pentagon wamesema ile siyo ICBM bali ni Intermediate Range Ballistic Missile (IRBM).
Umbali toka iliporushwa hadi ilipokusudiwa kupiga ni mfupi hakuna kichaa atatumia ICBM wakati IRBM zipo.
Kwa kukuondoa wasiwasi kuhusu idadi walizonazo Putin kasema zipo nyingi, na walipo ona imefaulu majaribio ya vitani watazalisha nyingi zaidi. Sababu malighafi zimetoka ndani ya nchi hivyo siyo gharama kubwa Sana kuzitengeneza.
 
Kuna makombora mengi Urusi pia hawezi kuzuia pamoja na kuwa na S 550 ambayo hayafiki mach 4
 
Back
Top Bottom