Orijino Comedi - Sasa Kwisha

Orijino Comedi - Sasa Kwisha

mwana akililia wembe, we mkate nao maana ukimpa atakukata wewe.
Cha msingi ni kujua kwamba ufisadi una nguvu kubwa ambapo ni budi tuwe na nia thabiti ya kujitolea kuutokomeza.
 
Ni kweli komedi hawana jipya tena,

haivutii tena

sasa naangalia mama kayai, ojwang na kobra squard

TBC naangalia tu kile kikundi cha fataki wale wanaoongea kwa mashairi/ngonjera. Hata taarifa ya habari ya TBC haina coverage sehemu nyingi za Tanzania kama ITV.

Heko ITV
 
Hebu sasa tutafute mambo ya maana ya kufanyia kazi, hilo kundi sasa ni kichefuchefu, wenye akili wote wanajua!
 
ulimbukeni pia tatizo. hawana ladha kabsaaaaaaaaaaaaa siku hizi..........kweli bora mizengwe, they are real hawa orijino ndo feki hamna kitu
 
Ukitaka kufurahi na kucheka sasa hivi cheki FUTUHI ya star TV.mimi siku nyingi sana niliacha kutazama original comedy kwa sababu haina vichekesho.Hata kama wanatetea mafisadi.tatizo lao ni kule kutochekesha!

Komedi haina ladha kama mlengwa hataweza kucheka!Sanaa ya uchekeshaji..ni kutunga stori za kuvunja mbavu na kuziingiza kwenye maigizo!
 
......hivi kuna mtu ameshawahi kuangalia VIMBWANGA TIME? Hili ni kundi jingine la vichekesho linalopatikana Channel 10, siku za Jumamosi kuanzia saa 2 usiku na kurudia Jumapili na Jumanne saa 10 jioni..................hutatamani kuangalia tena hao Orijino Komedi!!!
 
"hivi kuna mtu ameshawahi kuangalia VIMBWANGA TIME? Hili ni kundi jingine la vichekesho linalopatikana Channel 10, siku za Jumamosi kuanzia saa 2 usiku na kurudia Jumapili na Jumanne saa 10 jioni..................hutatamani kuangalia tena hao Orijino Komedi!"

Hapo umenigusa vimbwanga time kweli wanakuja juu....hata mimi nawafagilia sio orijino komedi...... ambao hawajaoa waoe wakatulie makwao na wake zao, sanaa imewashinda.
 
......hivi kuna mtu ameshawahi kuangalia VIMBWANGA TIME? Hili ni kundi jingine la vichekesho linalopatikana Channel 10, siku za Jumamosi kuanzia saa 2 usiku na kurudia Jumapili na Jumanne saa 10 jioni..................hutatamani kuangalia tena hao Orijino Komedi!!!
Channel Ten wengi hatuioni, inaonekena maeneo fulani ya mji kwingine tabu kuona.
 
Tukubaliane tu kwamba, chembilecho Mzee Mwinyi a.k.a ruxa, Kila Zama na Kitabu chake. Tulijazana kwenye kumbi kuangalia mpambano wa taarabu kati ya Muungano 'Taarabu iko Huku' na TOT '. Wako wapi? Tukatoka Mbagala Mabomu hadi iliyokuwa Silent Inn Mwenge kuifuata ile Band gani ile ilitingisha sana miaka ileee! Iko Wapi? Ni wazi kuwa hata hawa Orijino Comedi kitabu chao kiko kurasa za mwisho mwisho. Wanaojaribu kuwabeba wamawadanganya. Tusikitike tu kwamba Kitabu chao hakikuchukua muda sana...!!! Kuna mahali hawajachanga karata zao vyema. Tuwaambie kweli badala ya kuwabeba tu kusikowasaidia.
 
Nadhani ze comedy hawajui maana ya comedy ndiyo maana wamejikuta katika matatizo na watu mbali mbali. Wao wanachofanya ni kejeli "satire" na si vichekesho "comedy". Comedy inapaswa imfurahishe hata unayemuigiza na huangaliwa na watu wa umri na rika zote, lakini kwa hawa ze komedi kuna baadhi ya sehemu wanazoigiza ni kinyaa kutazama ukiwa na watu wa heshima. Mi nilishaacha kuwatazama siku nyingi tu they are redoubling their efforts when they have forgotten their aims.
 
Ni kweli inawezekana kwamba jamaa sasa hivi wamepunguza makali ila mimi naona jamaa bado kicheko kwangu hasa MPOKI hehehe.....Bill...why?????? Kwaniniiiiii?

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=3QQlMh-g--c"]YouTube - Dar-Moro Komedi[/ame]
 
Inaonekana kuna uhusiano wa karibu ssana kati ya wanamtandao na mafisadi... Tido Mhando ni mwanamtandao aliesaidia sana kampeni za "JUMA KILAZA" (JK) alipokuwa BBC na akazawadiwa ukurugenzi kama asante toka kwa JUMA KILAZA.

He!........
Hii Kali, ndo naiskia!
 
Channel Ten wengi hatuioni, inaonekena maeneo fulani ya mji kwingine tabu kuona.

Kwa wale wanaotumia free-to-air dishes, fanyeni consultation na mafundi wenu maana wamebadilisha frequency zao. Na hutawapata kwa jina la Channel 10 tena.Nadhani Mipango ya ununuzi imeshakamilishwa na Fisadi RA.
 
upande wa kuigiza miziki ya bendi mbalimbali ni wazuri. sometimes they perform better than the original music. they are good, wanahitaji mtu mwenye uwezo ili awaongoze
 
Haya ni maono au mtizamo wa watu mlio kuwa mnapenda Ze commedy wawe wanarusha EAT au chanel 5 mbona vijana wapo juu na wanakula maisha na kuchekesha kama kawa mtaani wanakamata sana vichwa...nyie endeleeni na hoja zenu zaifu.

Usisahau na wewe pia ni mtazamo wako ndo unauwakilisha. Hawa jamaa wamekwisha kimtindo. Hawana jipya
Mwanzo wa mwisho wao ndo huooooooooooooooooooooo! Jipe moyo kaka hata mie bado nawakumbuka Pwagu na Pwaguzi pia mahoka, ulikuwepo?
 
Nadhani ze comedy hawajui maana ya comedy ndiyo maana wamejikuta katika matatizo na watu mbali mbali. Wao wanachofanya ni kejeli "satire" na si vichekesho "comedy". Comedy inapaswa imfurahishe hata unayemuigiza na huangaliwa na watu wa umri na rika zote, lakini kwa hawa ze komedi kuna baadhi ya sehemu wanazoigiza ni kinyaa kutazama ukiwa na watu wa heshima. Mi nilishaacha kuwatazama siku nyingi tu they are redoubling their efforts when they have forgotten their aims.
Waache wajiandalie kifo kwa tamaa zao.Huwezi kukaa kwa kuwatete watu kwenye Luninga halafu useme ni vichekesho bali ni wizi mtupu.
 
Nafikiri hadithi ya komedi haitofautiani sana na hadithi ya ndoa wakati wa fungate na mwaka mmoja au mitatu au mitano baadaye depending na intensity ya mapenzi na available challenges in between!
 
Back
Top Bottom