Hii nchi watu wapuuzi... hata kama wasingekuwa na mwenzao kitandani, suala la kufanya mzaha na afya ya mtu ni ujinga uliopitiliza! Ila ndugu yangu
Chinga One ndo maana sie wengine hizi siasa zenu tunajionea ujinga mtupu! OK wanafahamika tangu hapo ni wapuuzi tu! Lakini hata wale ambao hatukuwadhani kwamba nao ni wapuuzi nao wanaendesha upuuzi ule ule! Lakini kwa vile siasa zenu zenyewe hizi zimeshamiri maji taka, basi hata huyo Lowassa angesimama kwa tiketi ya CCM, upuuzi huu unaofanywa sasa na CCM dhidi ya afya ya Lowassa ungefanywa na UKAWA dhidi ya huyo huyo EL au mwingine yeyote endapo angekuwa na matatizo sawa na EL na yupo upande wa CCM!
Nakumbuka Mrema kakashifiwa sana hususani hapa JF kutokana na maradhi yake na waliokuwa wanamkashifu majority ni wana-CHADEMA! Nakumbuka enzi zile ni mashabiki wa CCM ndio waliokuwa wanajifanya kumjua Mungu na kuwaona mashabiki wa upinzani wanakufuru kumnyanyapaa Mrema kwa ajili ya afya yake!!! Yaani nyinyi watu wa siasa na wafuasi wenu ni tatizo kweli kweli nchi hii!