Orijino Komedi wanapokashifu afya ya Lowassa, wamesahau ya mwenzao VENGU?

Orijino Komedi wanapokashifu afya ya Lowassa, wamesahau ya mwenzao VENGU?

Hii nchi watu wapuuzi... hata kama wasingekuwa na mwenzao kitandani, suala la kufanya mzaha na afya ya mtu ni ujinga uliopitiliza! Ila ndugu yangu Chinga One ndo maana sie wengine hizi siasa zenu tunajionea ujinga mtupu! OK wanafahamika tangu hapo ni wapuuzi tu! Lakini hata wale ambao hatukuwadhani kwamba nao ni wapuuzi nao wanaendesha upuuzi ule ule! Lakini kwa vile siasa zenu zenyewe hizi zimeshamiri maji taka, basi hata huyo Lowassa angesimama kwa tiketi ya CCM, upuuzi huu unaofanywa sasa na CCM dhidi ya afya ya Lowassa ungefanywa na UKAWA dhidi ya huyo huyo EL au mwingine yeyote endapo angekuwa na matatizo sawa na EL na yupo upande wa CCM!

Nakumbuka Mrema kakashifiwa sana hususani hapa JF kutokana na maradhi yake na waliokuwa wanamkashifu majority ni wana-CHADEMA! Nakumbuka enzi zile ni mashabiki wa CCM ndio waliokuwa wanajifanya kumjua Mungu na kuwaona mashabiki wa upinzani wanakufuru kumnyanyapaa Mrema kwa ajili ya afya yake!!! Yaani nyinyi watu wa siasa na wafuasi wenu ni tatizo kweli kweli nchi hii!

Nimekuelewa sana mkuu.. Thumbs up! Thumbs up! Thumbs up!
 
Kama Magufuri ni mzima,loliondo kwa babu alienda kufanya nini,amekunywa kikombe
 
Tumeshudia mtu anaanguka jukwaani,tumeshuhudia magufuli anakunywa kikombe kwa babu
 
mtu kama Massanja ndio nimebaki kumshangaa ata kama ni njaa zingine zimezidi. Huyu jamaa si naskia ni mchungaji? huwa anaubiri nini akiwa na waumini wake?
 
Wakati Mrema akiendelea na Kampeni zake huko Vunjo, aliyekua akimuigizia afya yake(Vengu leo hii Mwaka wa 3 na nusu yupo kitandani.
 
Wakati Mrema akiendelea na Kampeni zake huko Vunjo, aliyekua akimuigizia afya yake(Vengu leo hii Mwaka wa 3 na nusu yupo kitandani.

ImageUploadedByJamiiForums1442042150.944418.jpg
 
Suala la afya ya mtu sio chambo la kufanyia maigizo hata kidogo.
Orijino Komedy imebaki jina tu lakini ni kikundi ambacho kwa sasa hakina tena mvuto wowote na wala hakina ushawishi wa namna yoyote ile kwenye kampeni hizi za Uchaguzi.
Mkuu umekasirika hasa,mpk wanakufanya uchapie!
 
Back
Top Bottom