ORLANDO PYRATES: Walivyochezewa nusu uwanja hata nyumbani kwao Afrika ya kusini waliona. Porojo za hujuma hazina nafasi.

ORLANDO PYRATES: Walivyochezewa nusu uwanja hata nyumbani kwao Afrika ya kusini waliona. Porojo za hujuma hazina nafasi.

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Katika ulimwengu wa soka wa Leo Kila mmoja anajionea mwenyewe mambo yalivyokuwa uwanjani. Nafasi ya kudanganya watu kujitafutia huruma haipo.

Kusema kweli Orlando washukuru Sana kuishia kufungwa goli moja tu kwa jinsi walivyokuwa wamezidiwa! Hiyo penati ilikuwa ya wazi Sana, BM alipigwa ngwala ya kizamani!
 
Hivi una habari kuwa kati ya timu 8 zilizoingia robo fainali SIMBA ndiyo Ina matokeo mazuri zaidi baada ya mechi ya Kwanza?
Si vibaya ukipongeza!
Tatizo ni utopolo kufikiri hii ni ligi ya NBC yenye timu za Mbeya kwanza. Huku ni kwa wanaume.
 
Hivi una habari kuwa kati ya timu 8 zilizoingia robo fainali SIMBA ndiyo Ina matokeo mazuri zaidi baada ya mechi ya Kwanza?
Si vibaya ukipongeza!
Sijui hii inachukuliwaje! Lakini kuna somo kubwa sana Simba kwa timu zilizocheza away.
 
Vipi zile dk 20 za mwisho bado waliendelea kuchezewa nusu uwanja
Zile dk 20 za mwisho wala zisikutishe. Simba waliamua kuwekeza nguvu kwenye kushambulia wakaacha kiungo mkabaji mmoja ndio maana wale jamaa walionekana bora. Kwenye mechi ijayo usidhani Simba wataingia kizembe. Subiri tuone.
 
Katika ulimwengu wa soka wa Leo Kila mmoja anajionea mwenyewe mambo yalivyokuwa uwanjani. Nafasi ya kudanganya watu kujitafutia huruma haipo.

Kusema kweli Orlando washukuru Sana kuishia kufungwa goli moja tu kwa jinsi walivyokuwa wamezidiwa! Hiyo penati ilikuwa ya wazi Sana, BM alipigwa ngwala ya kizamani!
Cha kusikitisha huyu naye unaweza kuambiwa ni mchambuzi wa mpira kwenye viredio vyetu vinavyoishia magomeni.
 
Cha kusikitisha huyu naye unaweza kuambiwa ni mchambuzi wa mpira kwenye viredio vyetu vinavyoishia magomeni.
Na posho ya uchambuzi analipwa! Kuna maajabu mengi nchi hii tumekomalia ripoti ya CAG wakati kuna vulaza wanaharibu sifa za wachambuzi.

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Jeff Lea anasema Simba ilishinda kwa kutumia dark arts, sijui ndio uchawi ?🐒
 
wewe uchambuzi wako uko wapi tuusome
Nitakwenda kukuchambulia kinachokwenda kutokea Soweto, baada ya kutolewa kule mtamkuta Mayele ameshapaka vumbi la Congo, baada ya mechi hiyo na Mayele kutetema ndio akili zitawarudia na kuusikia uchungu wa gap ya point 16, shughuri kwishney.
 
Nitakwenda kukuchambulia kinachokwenda kutokea Soweto, baada ya kutolewa kule mtamkuta Mayeke ameshapaka vumbi la Congo, baada ya mechi hiyo na Mayele kutetema ndio akili zitawarudia na kuusikia uchungu wa gap ya point 16, shughuri kwishney.
Wewe ni Yanga tu 🤣🤣🤣🤣
 
Nitakwenda kukuchambulia kinachokwenda kutokea Soweto, baada ya kutolewa kule mtamkuta Mayele ameshapaka vumbi la Congo, baada ya mechi hiyo na Mayele kutetema ndio akili zitawarudia na kuusikia uchungu wa gap ya point 16, shughuri kwishney.
HAHA safi sana
 
Vipi zile dk 20 za mwisho bado waliendelea kuchezewa nusu uwanja
Tunatumia takwimu/statistics za dakika zote 90! Mchezo wa kandanda ni dk 90. Ndiyo maana timu ya wiki ya CAF karibuni nusu yake ni wachezaji wa Simba!! Kati ya 11 Simba imeingiza wachezaji 5!
 
Vipi zile dk 20 za mwisho bado waliendelea kuchezewa nusu uwanja
Angalia mabadiliko yaliyofanyika pia kwenye kikosi cha Simba, walitolewa viungo wakabaji kisha wakaingizwa washambuliaji ni lazima mchezo ungebadilika tu pale kati.

Kwakua nyinyi sio watu wa mpira hilo huamuwezi hamuwezi kuliona.
 
Back
Top Bottom