mtwa mkulu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2013
- 8,586
- 11,227
Umeshindwa kumtaja aliyeanzisha mradiUwe na adabu na heshima kwa Mheshimiwa Rais. Haitwi huyu Mama . Anaitwa Mheshimiwa Rais Dkt Mama Samia Suluhu Hasssan.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeshindwa kumtaja aliyeanzisha mradiUwe na adabu na heshima kwa Mheshimiwa Rais. Haitwi huyu Mama . Anaitwa Mheshimiwa Rais Dkt Mama Samia Suluhu Hasssan.
Sio watanzania, sema mazombieWatanzania wanatambua ya kuwa ni CCM Pekee iliyo na uwezo wa kuiongoza Tanzania
ANC ndio ina historia ya kujuvunia, sio hiki Cha majizi.chama cha mapanyarodi chadema kina historia fupi ajabu aise dah 😀
ukitaja mbowe tu, basi ndio historia ya chama cha mapanya rodi imeishia apo 😀
mapanyarodi na manyumbu haikua inawahusu sana japo si mbaya mkaelewa historia hiyo mujarabu sana😎Sio watanzania, sema mazombie
nadhani uMKHONTO WESIZWE ya J.ZUMA ina historia ndefu kuliko chama cha mapanyarodi na nyumbu- chadema dah😀ANC ndio ina historia ya kujuvunia, sio hiki Cha majizi.
Kwa uKatibu Mkuu CCM, kusini wanatisha inabdi tuwape maua yao ya maadili mema. Ni kama wanavyotisha Arusha na Moshi (Kaskazini) kwa nafasi ya Waziri Mkuu: SOKOINE, EDWARD LOWASSA, FREDRICK SUMAYE, CLEOPA MSUYA. Huyu MSUYA pamoja na Sokoine waliwahi kushika mara mbili kila mmojaNdugu zangu watanzania,
Leo nimeona niwaletee makatibu wakuu wa CCM tangia kuasisiwa kwa CCM Mwaka 1977. Nitaweka uchambuzi wangu binafsi kidogo kuwaonyesha waliohudumu kwa muda mrefu na wale waliohudumu kwa muda mfupi sana na sababu zake .orodha ni kama ifuatavyo.
1977-1981=Pius Msekwa .huyu ndiye
katibu mkuu wa kwanza
Tangia CCM
ilipoasisiwa
baada ya kuunganisha
chama cha TANU na
ASP (5-2_1977)
1981-1982= Ndugu Balozi Daudi
Mwakawago.
1982-1990=Ndugu Rashidi Kawawa.
1990-1995= Ndugu Horrace
Kolimba.
1995-1997= Ndugu Laurence Gama.
1997-2007= Ndugu Philip Mangula.
2007-2011= Ndugu Yusuphu
Makamba.
2011-2012= Ndugu Dr Willson
Mukama.
2012-2018=Ndugu Abrahamani
Kinana.
2018-2021=Ndugu Dr Bashiru Ally
2021-2023=Ndugu Daniel Chongolo.
2024 Ni Ndugu Dr Emmanuel Nchimbi.
Sasa ndugu zangu ukiangalia katika orodha hiyo na miaka yake utagundua ya kuwa mzee Philipo Mangula ndiye katibu mkuu aliyedumu na kuhudumu kwa muda mrefu katika nafasi hiyo tokea kuasisiwa kwa CCM .Ambapo Alikaa kwa takribani miaka kumi .katika kufanya uchambuzi wangu na tathmini yangu binafsi nimegundua kuwa kwanza alihudumu kipindi cha Hayati Mzee Benjamini Mkapa,Ambapo nikabaini ya kuwa ni kiongozi ambaye katika nafasi nyeti na kubwa serikalini na chamani alikuwa hapendi kubadilisha badilisha watu.yaani ilikuwa kama kakuamini na kukupitisha basi alitamani na kuwa na dhamira ya kufanya kazi na wewe mpaka mwisho wa uongozi au utawala wake wa miaka kumi unapokoma kikatiba.
Hii nimefanya na kufika hitimisho hilo baada ya kuangalia pia katika nafasi ya waziri mkuu wake ambapo alifanya kazi na waziri mkuu mmoja tu kwa miaka yake yote kumi uongozini .ambapo alifanya kazi na mheshimiwa Frederick Sumaye anayeshikilia rekodi hiyo mpaka sasa ya kukaa miaka mingi kama waziri mkuu.
Pili ni katika nafasi ya waziri wa mambo ya nje ambapo pia katika miaka yake yote kumi ya Urais wake alifanya kazi na Mheshimiwa Dr Jakaya Mrisho Kikwete ,ambaye pia ndiye mpaka sasa anayeshikilia rekodi ya kuwa waziri wa mambo ya nje aliyehudumu kwa muda mrefu sana wa miaka kumi.ambapo mpaka sasa hakuna aliyefanikiwa kufikia rekodi yake hata kwa nusu tu ya miaka yake.
Kwa hiyo nikagundua kuwa Hayati Mzee Benjamini Mkapa ni kiongozi ambaye alikuwa akikuamini anakuamini kwelikweli na akifikia uamuzi wa kukupa nafasi basi anakuwa anamatarajio makubwa kutoka kwako ya kusaidiana nawewe mpaka mwisho. Na kwa upande mwingine utaratibu huu ni mzuri kwa kuwa unawapa utulivu wa kazi wasaidizi wako yakufanya kazi kwa kujiamini na pasipo mawazo au hofu ya kuondolewa wakati wowote ule .tofauti na ile kila mtu akilala usiku kucha anawaza kama kesho kutakucha akiwa katika kiti chake au nafasi yake ya uongozi ,yaani anakuwa anafanya kazi kwa presha na kutokujiamini kabisa na wakati mwingine inaweza ikamfanya aamue ajipendekezage tu na kukuabudu tu muda wote kama Mungu ili kujihakikishia uwepo wake katika uongozi uliomteua.
Lakini athari yake kwa upande mwingine ni kuwa mtu akijuwa wewe hunaga tabia ya kubadilisha badilisha au maamuzi magumu ya kumtoa mtu mahali bila kuangalia sura inaweza kupelekea watu kufanya kazi kwa mazoea bila hofu wala uoga wala ubunifu wala kujituma.yaani mtu anakuwa anafanya kazi anavyotaka yeye .anakuwa anadumu katika eneo moja kwa kujitengenezea na kujichimbia mizizi chini ili asitoke na hata akitoka basi aache watu wa kumlinda yeye na maslahi yake na Madudu yake yote aliyoyafanya akiwa katika nafasi husika.
Lakini pia inaweza kupelekea kuwadhoofisha kiuongozi wale wanaoonekana kufanya kazi kwa bidii na kuja na ubunifu mpya utaakaoonekana kufunika utendaji wa yule aliyedumu kwa mda mrefu . hivyo ili kutokuhatarisha nafasi yake inaweza anza kupigwa fitina na Majungu ya kumuondoa yule anayeonekana ni wakuja au mgeni ikiwepo kulazimisha ahamishwe na fitina zingine kibao hadi michezo ya nyuma ya pazia ya kiafrika.
Kwa hiyo yote kwa yote ni lazima uwe kiongozi ambaye wasaidizi wako na watendaji wako wote wafahamu ya kuwa kitakachokubakisha na kukuhakikishia kudumu katika uongozi ni uchapa kazi wako na ubunifu wako unaoleta matokeo chanya,kufanya kazi kwa bidii,kujituma kwa hali ya juu na kutokusubili au kuwa mtu wa kufanya kazi kwa kusukumwa sukumwa tu.
Ni lazima wasaidizi wako na watendaji wote wa serikali wafahamu kuwa ukiharibu kazi unaweza kuondolewa muda na wakati wowote ule hata ndani ya mwezi mmoja tu bila kuangalia sura yako wala ukubwa wa jina lako wala la wazazi wako.ni lazima kila mtu afanye kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu,katiba na miongozo mbalimbali.
Wakati mwingine nitakuja kuwachambulia wale waliodumu kwa muda mfupi na sababu zake kwa maoni yangu hasa kwa mzee Dr Willson Mukama.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.
CHADEMA ni genge la manyumbu na mafisi yenye njaa kali tumboni mwao na ndio maana yanapendekeza kuwa na wabunge wawili katika kila jimbo ili yapate matumaini kiasi ya kushibisha matumbo yao.bila kujali kuwa itamuongezea mwananchi mzigo mkubwa wa gharamachama cha mapanyarodi chadema kina historia fupi ajabu aise dah 😀
ukitaja mbowe tu, basi ndio historia ya chama cha mapanya rodi imeishia apo 😀
Mheshimiwa Hayati Mwalimu Dkt John Pombe Joseph Magufuli Rais wa awamu ya Tano ya jamuhuri wa muungano wa Tanzania.Umeshindwa kumtaja aliyeanzisha mradi
Nakubaliana nawe hapo kwa JK ila ukiangalia msingi wa hoja ya KADA ni kwamba Hayati BWM kwenye kutobadilisha viongozi wake aliowateua alifanya vizuri zaidi. Hivyo ana imply kuna Kiongozi au Viongozi waliofuata hawafanyi kama Hayati BWM.Hapana mkuu Sidhani kama Uko sahihi..
Mimi Ni KADA wa CCM wa Muda mrefu naweza kukuambia kuwa JK hakubadilisha Sana makatibu wakuu Kama unavyosema Maybe Ungemsema Mama na JPM..
Kwa Jk..
Makamba alichomoka Mwenyewe na Sektretariet yote Japo aliongoza kwa jumla ya Miaka 5 kama Katibu Tangu mwaka 2007 mpaka mwaka 2011
Sababu ya kuchomoka ilikuwa Makamba kufail kwenye Strategies Za uchaguzi wa Mwaka 2010 uliopelekea Majimbo mengi ya Uchaguzi kwenda Upinzani..
Mtikisiko ulitokea kwenye Chama hivyo wao waliamua kujitoa kipindi hicho ndo kulikuwa Na ufisadi mwingi kwenye Chama na Serikali..
Na ukija kumzungumzia Mukama utakumbuka Maswala ya "Vua Gamba" Enzi hizo kama unafatilia siasa kwahyo JK si wa kulaumiwa
OkNakubaliana nawe hapo kwa JK ila ukiangalia msingi wa hoja ya KADA ni kwamba Hayati BWM kwenye kutobadilisha viongozi wake aliowateua alifanya vizuri zaidi. Hivyo ana imply kuna Kiongozi au Viongozi waliofuata hawafanyi kama Hayati BWM.
KWani kuna ubaya gani kama ungesema tu Hayati JPM au hujui kuwa Mtu haitwi Mheshimiwa Akiwa amefariki Hiyo nayo inahitaji nini kukuelewesha?Mheshimiwa Hayati Mwalimu Dkt John Pombe Joseph Magufuli Rais wa awamu ya Tano ya jamuhuri wa muungano wa Tanzania.
Huwezi kumuita Dkt pia kwa sababu Honorary PhD huwa haiwi adressed kwenye PreffixesUwe na adabu na heshima kwa Mheshimiwa Rais. Haitwi huyu Mama . Anaitwa Mheshimiwa Rais Dkt Mama Samia Suluhu Hasssan.
Hapo sawa japo najua hujapendaMheshimiwa Hayati Mwalimu Dkt John Pombe Joseph Magufuli Rais wa awamu ya Tano ya jamuhuri wa muungano wa Tanzania.
1981-1982= Ndugu Balozi Daudi Mwakawago.
1982-1990=Ndugu Rashidi Kawawa.
1990-1995= Ndugu Horrace Kolimba.
1995-1997= Ndugu Laurence Gama.
1997-2007= Ndugu Philip Mangula.
Asilimia kubwa wana origin ya Kusini Nyanda za Juu2021-2023=Ndugu Daniel Chongolo.
2024 Ni Ndugu Dr Emmanuel Nchimbi.
Acha uongo wako wewe . Usingeweza kunifanyia usaili mimi wakati sikwenda hata hatua ya usaili maana tulikatwa juu kwa juu baada ya mtihani😀😀😀😀 halmashauri watu wabaya sanaa.NIsaidie kumuuliza Vipi ile kazi ya kukusanya Taarifa za makazi aliipataga?😅😅
I was the one assessed him, (From above) Kwa upande wa Juu sana, Japo hanijui na hajawahi kuniona😅😅..
Na wala hatakuja kunijua😅😅
Cc: Lucas mwashambwa
wabunge wanaowaita wa covi-19 asilimia 85 ni wives zao eti wanawafukuza chamani kwao 😀 jamaa kwa maigizo hawa dahCHADEMA ni genge la manyumbu na mafisi yenye njaa kali tumboni mwao na ndio maana yanapendekeza kuwa na wabunge wawili katika kila jimbo ili yapate matumaini kiasi ya kushibisha matumbo yao.bila kujali kuwa itamuongezea mwananchi mzigo mkubwa wa gharama
Yaani CHADEMA ni minyumbu sanaa eti nayo inakubali kweli kuwa wamekubaliana kuwafukuza .wakati wanajuwa fika kuwa ni wake wa viongozi wao na wanatumia madhara huo huo wa wake zao kulishwa matumbo yaowabunge wanaowaita wa covi-19 asilimia 85 ni wives zao eti wanawafukuza chamani kwao 😀 jamaa kwa maigizo hawa dah
Hiyo Halmashauri na nyinginezo si ni sehemu ya mfumo unaoutetea hapa kila siku? Nimebaini sasa kama unakubali kuwa Mifumo inawakata watu juu kwa juu, basi unatetea mambo usiyoyaamini ili tu uonekane na ndio maana unaandika bila kuacha kuweka namba ya simu.Acha uongo wako wewe . Usingeweza kunifanyia usaili mimi wakati sikwenda hata hatua ya usaili maana tulikatwa juu kwa juu baada ya mtihani[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] halmashauri watu wabaya sanaa.
Acha ujinga wewe nani kakwambia kuwa mifumo ni mibovu? Kwani mtu mmoja akiharibu ndio mfumo mzima mbovu? Kuna watu wachache tu ndio wanakuwa wanaharibu taswira nzuri ya serikali yetu.ndio maana hata waziri wa Tamisemi Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa amekuwa akikemea sana masuala ya uonevu katika halmashauriHiyo Halmashauri na nyinginezo si ni sehemu ya mfumo unaoutetea hapa kila siku? Nimebaini sasa kama unakubali kuwa Mifumo inawakata watu juu kwa juu, basi unatetea mambo usiyoyaamini ili tu uonekane na ndio maana unaandika bila kuacha kuweka namba ya simu.
Sasa ndo ujiulize kwwanini Ulikatwa 😅😅😅..Acha uongo wako wewe . Usingeweza kunifanyia usaili mimi wakati sikwenda hata hatua ya usaili maana tulikatwa juu kwa juu baada ya mtihani😀😀😀😀 halmashauri watu wabaya sanaa.