Orodha ya benki za biashara zilizofungwa 2015-2020

Ile Benki ya Wanawake ndio iliunganishwa na TIB? Alafu kama niliona mahali Twitter benki ya posta hivi sasa ni kama ina upungufu wa ukwasi
 
Orodhesha na ambazo zimefunguliwa ili kuweka mizania sawa, kisha usisahau na zile mbili zilizofunga ndoa na sasa ni benki moja.
 
Tatizo kubwa ni ukwasi ambao umeyumba kutokana na mikopo chefuchefu kuwa mingi ,mfano Twiga bank ilikuwa na matatizo tangu 2011 niliwahi kuona mahesabu yake ya robo mwaka assets na liability zilikuwa hazilinhani ,sema uongozi iliopita ilikuwa unavumilia sana ,pia kwenye hii list yako umeunganisha bank zilizofungwa na zilizoungana au zilizounganishwa,mfano benki za serikali ziliunganishwa ili zilete tija, benki zingine zilizoungana ni nic na cba, nadhani exim walichukua ubn,mwanga community ikachukua hakika na efc microfinance, uchochoro wa mabenki Tanzania ilikuwa unasababishwa na mazingira mazuri ya biashara yaliyokuwepo kipindi cha nyuma pamoja na unyonyaji wa mabenki ,kwani kipindi cha nyuma ilikuwa rahisi sana kwa benki mpya kuanza kutengeneza faida ndani ya miaka miwili tu ya kuanzishwa ,ila kwa Leo benki zinalia sembuse benki mpya? Labda iwe ya kisiasa na haitadumu pia
 
Ile Benki ya Wanawake ndio iliunganishwa na TIB? Alafu kama niliona mahali Twitter benki ya posta hivi sasa ni kama ina upungufu wa ukwasi
Benki ya wanawake iliunganishwa na TPB siyo TIB, pia twiga na TIB ziliunhanishwa TPB ,ni kweli TPB inatatizo la ukwasi has a baada ya kurithi madeni na mitaji ya hizi benki zilizoinganishwa kwakwe,ndio maana now wanafanya promotion ya fixed deposits by 11% per year ,
 

Pesa imekuwa moto kushikangumu,ukiweka benki sana TRA ,TISS,serekali wote wanataka kujua mbona unaingiza au unapata wapi.hii wafanya biashara wengi wameogopa maana
TRA. Siku hizi mpaka pesa yako ya benki hiwe yoyote ufatilia kulinganisha na biashara (malalamiko yapo mengi sana)
TISS .hawa bwana ukiwa na mdomo sana utaishia kupotezewa akaunti zako tunao wengi na wengine wanaogopa hata kuweka wala kutumiwa.wengine wapo jera
N.k

Benki sasa zinachunguzwa mpaka utawaonea huruma
 
Sijui hii miaka mitano hali ya uchumi itakuwaje?
 
Namba 7 sababu za kufungwa si kwamba ni tofauti?
 
Bado shule za private zenye kuonekana zinapiga sana mahela..mjiandae.

Bwanayule mzalendo hataki 'ufisadi'..!
Nguvu kubwa sasa iko kwenye kuboresha shule za serikali ili ziwe shule bora zaidi Tanzania.... sio kufungia shule binafsi🤣🤣🤣
 
10
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…