Wauzaji wa dawa feki hapa TZ ni wengi ajabu. Ni muhimu kutafuta mtu wa kutoa ushuhuda ingawa lazima ukubali disclaimer kwa Tiba mbadala! Si kila dawa inayomtibu A itamtibu B, C, D etc. Nina Mfano wangu mwenyewe. Kuna dawa za kichina zilimtibu rafiki yangu 2018 na mpaka anatwaliwa mwaka jana, tatizo lilikuwa limeisha.
Mimi 2025 mwanzoni likanibana, nikachukua dose ni miezi Minne (Gharama $6,000) nikapambana nalo, kweli vipimo vikaonesha tatizo limepata muafaka.
Huwezi amini mwaka huu mwanzoni, bila hili wala lile, kwenye annual full body checkup, kipimo juu. Wachina wakanieleza pengine ni mabadiliko ya hali ya hewa, bla bla. Nikarudi baada ya miezi miwili kupima kitu kinazidi kupaa. Ikabidi sasa niachane na Tiba mbadala, nuclear medicine ndiyo imerejesha matumaini.
Hivyo si kila dawa inamfaa kila mtu katika Tiba Mbadala. Ila mwanadamu lazima ujaribu kila kitu. A very Good morning