Orodha ya magonjwa ambayo ukiyapata hayatibiki kwa hapa Tanzania

Saratani haijawahi kuwa na tiba popote pale duniani, ukiupata huu ugonjwa kinachobakia ni kusogeza siku tu
Saratani inatibiwa; inategemea imeshambulia sehemu gani ya mwili na imegnduliwa ikiwa katika ngazi gani. Nadhani saratani ngumu kutibiwa ni ile ya Ubongo, Mapafu na ya kongosho (pancreatic -kama sikukosea). Nyingine zote zinatibika zikingundulika mapema katika stage 1 au stage 2.

Halafu pia elewa neno kutibu maana yake ni kurefusha maisha, siyo kuzuia kifo. Hakuna kiumbe kitakachoishi bila kuonja mauti.
 
niliwahi kupata tatizo la vidonda vya tumbo Lakini kwasasa imethibitika sinavyo tena πŸ’

sijui nini kiliniponya mpaka wa leo, dawa za hospitali nilitumia kwa wingi sana, tiba mbadala mitishamba na miziziologi nimetumia kwa wingi mno, ibada na maombezi nimeshiriki sana πŸ’

Ile nashukuru zaidi ni Neema na Baraka za Mungu nimepona kabisa baada ya mateso kwa kipindi fulani kirefu πŸ’
 
Asali ni dawa kubwa sn ya vidonda vya tumbo
 
Pili pili ina asidi?
 
Jaundice sio ugonjwa ni dalili ya baadhi ya magonjwa hasa ya ini. But I can assure u magonjwa mengi km sio yote ya ini na yanayosababisha manjano ( jaundice)yanatibika kasoro Hepatitis B, Kansa ya ini au kansa ya kongosho
Asante kwa jibu zuri lenye matumaini, nina kijana wangu ana Jaundice
 
Pia kumbukeni dawa nyingi tunazotumia nchi hii ni za ubora wa chini sana,. Mfano mzuri jaribu kulinganisha ubora wa Amoxiclav hizi za India ( Myclav, and the likes) na Amoxiclav ile original Augmentin ya GSK( European Quality)
Dawa za GSK PRODUCT (UK) Zina Bei juu pia ufanisi wake Ni mkubwa sanaaa...
 
Nipo Mwanza sijui wewe upo wapi au kama una connection na Dr aliopo mkoa niliopo utakua umenisaidia. Kuna baadhi ya hospitals nilisha mpeleka wakaishia kumpa folic acid
 
Ni life style tu inakuepusha na hili janga.

Kama wewe ni mtu unaepitia stress sana mara kwa mara, hasira nyingi unakosewa kidogo unalalamika unahuzunika, unaweka vitu moyoni vinakutuafuna mwenyewe, basi una uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo kwa asilimia 98 %
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…