Orodha ya majiji, miji na wilaya zenye mzunguko mkubwa wa hela Tanzania

Heading na contents haviendani, sio kila mji au wilaya yenye mapato makubwa basi kuna mzunguko mkubwa wa fedha, mapato ya halmashauri hutegemea aina ya vyanzo vilivyomo ndani ya eneo husika, nitolee mfano Chalinze, chalinze sehemu kubwa ya mapato yake yanatokana na ushuru wa kokoto, zile kokoto hazitengenezi money circulation ndani ya lile eneo kwani wamiliki wa machimbo wala sio wakazi wa chalinze, na zile kokoto haziuzwi chalinze, vivyo hivyo kwenye maeneo ya migodi inayomilikiwa na makampuni, hapo mapato yatakuwa mengi kwa upande wa halmashauri lakini sio lazima sana money circulation iwe kubwa katika eneo hilo

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
 
Halmashauri ikishapata mapato inayapeleka wapi?
 
Darasa limeniingia. Asante.
P
 
Darasa limeniingia. Asante.
P
Pasco ukipata wasaa tembelea khm,uone mji ulivyo changanya kibiashara, ufanye mahojiano na mkurugenzi, ili upate undani wa mapato na shughuli za kiuchumi kiujumla.ndo utajua khm ni ndogo au ni kubwa.tamisemi wenyewe wanatambua kahama nikubwa ndo maana kwenye makundi ya halmashauli iko kundi A. mirad ya tactic inayo fadhiliwa na benki ya dunia kahama ipo kundi la kwanza lenye miji 12,na ni wilaya pekee kwenye hili kundi,miji mingine yote ni makao makuu ya mikoa.
 
Kiukweli kuna vitu unanifungua macho sikuwahi kuimagine, kwa kutoijua kwangu Kahama, nikajua mji wa Kahama utajiri wake ni Kahama Gold Mine, nilipita zamani nikaona hali ya mgodini na hali ya nje ya mgodi ni kama mbingu na dunia!. Hivyo nikahesabu maendeleo yote ya Kahama ni Kahama Gold Mine, sasa nikiangalia CSR ya Kahama Gold Mine compared na CSR ya GGM, GGM ndio wanaoongoza kwa CSR sasa iweje Kahama iipite Geita kimapato?. Nikija kuilinganisha na mji wa Moshi, Kinapa na Kia, nikaamini Kahama can't compete!.

Haya mambo ya kusafiria mwewe haya yanatukosesha kuijua vizuri nchi yetu, from time to time we should travel by road tuone maendeleo. Thanks for this na kiukweli ikifanywa documentary ya maendeleo ya Kahama, you never know, they might inspire the rest to follow and do what Kahama does. Naiweka Kahama kwa kuichomekea kwenye mpango kazi wangu kwa mwaka huu, na kiukweli sisi mainstream media hatuwatendei haki Watanzania kwa kutoa habari za mijini tuu na ku neglects habari za vijijini ambako ndiko kwenye wananchi.
P
 
Hakika mkuu yaani ukienda kahama na geita hata innovation ya frem zao za maduka wanavyojenga ni nzuri sana!

Na kwa sasa wafanyakazi wa migodi ya Bulyanhulu ni watu wa kawaida sana kwa kuwa wachimbaji wadogo wana pesa kuliko wafanyakazi wa mgodini au tunawaita watingaji!
Ila kwa miaka ya nyuma ukionekana mfanya kazi wa mgodini ilikuwa issue kubwa ila kwa sasa hakuna kitu kama hicho!

Vijana wanamiliki mamilioni ya kutosha hela ambao mfanyakazi wa mgodini hawezi kuwa nayo
Sema jamii ya huku ya ndugu zetu wasukuma na watu wa kanda hii ya ziwa si watu wenye sifa kwa kifupi hawana kelele!

Ila mi nakili kabisa ukiwa umejifungia Dar utajidanganya sana ila maisha saizi sio kukariri Dar na miji mikubwa utakuwa inajidanganya sana na siku ukitoka ukaingia mkoa utajiona unacheza na hakuna lolote!
Mda mwingine utakuwa unaita watu washamba kumbe wewe ndo huna lolote umebakiza kubwajaja!
 
True, nilikuwa nakosea sana!. Jf ni darasa sasa nafungua macho, nitatinga Kahama!.
P
 
Mikoa yote kiwango kimeshuka sn kwa sababu zifuatazo
1.Covid...hapa watu toka nje ya nchi wengi walisitisha safari while Covid was at its peak..so mzunguko wa dollar tz ulishuka sn.
2.misaada mingi sn ilisimama,kumbuka 90%ya fedha ya TZ we depends na misaada km hii kitu ilikisimama hakuna mzunguko wakutosha.
3.NGO nyingi sn zilikufa tena hapa ndio jana kubwa lilipo
4.vita ya Ukraine. ..ingawa hapa naona kuna siasa nyingi kuliko uhalisia
 
Sijakuelewa hapo ndio umeongea nini?
 
Manispaa ya kwanza kuwa nje ya Makao makuu ya Mkoa Tanzania. Rekodi ya kipekee kabisa kuwekwa na Kahama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…