Kwakweli Shinyanga kwa sasa imefunguka imeamka, kasi ya maendeleo nikubwa mno. Kwa waliotembelea Shy kuanzia 2020 kurudi nyuma na sasa nadhani wameona mabadiliko makubwa sana. Mji umefunguka umeanza kuchangamka. Pia wengi wanapita barabara kuu wanajua ndio mjini kati hapo ila hapo wanapopita ni pembeni, mji umefunguka sasa CBD inakimbilia lubaga na mpaka bushushu uelekeo wa oldshy,mahotel yanajengwa kwa kasi na biashara zinafunguliwa kwa kasi. Pongezi za dhati kwa mkurugenzi aliepita bwana jomari satura hakika alikua na juhudi za dhati kuubadilisha mji walau sasa mji unaonekana.