Mimi nimewahi kuota vita napigana na watu wa mataifa ya nje, nimeota nipo natembea sokoni, ghafla inapigwa ambushi. Ndege za kivita, silaha yani ni vita kabisa. At the end of the day nikapambana sana, wenzangu wengi walikufa kwenye hiyo vita, mwisho wa siku nili survive kwani nilimteka kiongozi wa hao wazungu. Hivyo waka surrender lakini niliumia kwa kupata majeraha kadhaa, at the end of the day nikademand pesa nikapewa dollar kadhaa na kumuachia huyo kiongozi wao.

Hiyo ndoto nilivyoamka nilijihisi kabisa uchovu. Acha tu.
 
Asante pia kwa ufafanuzi mzuri kuna jambo kubwa umeongezea hapo kwenye maana ya hizo alama ambalo lilikuwa alijajumuishwa na imekuwa faida kwetu sote.
 
Mi nishawai kuota kuna uwazi mkubwa (tundu)kwenye mbingu,na pia nishawai kuota kiama
 
Ulikuwa unaangalia movie Gani kabla ya kulala?ya kivita?kiinteligensia?
 
Theory tu, vp kama leo niliota kupanda kesho nikaota kushuka?.

Maisha ni zaidi ya ndoto
Ndoto si nadharia kwa kuwa kuna uthibitisho wa kisayansi kuwa binadamu na viumbe hai wengine uota.

Ubongo wetu ufanya imaginations kibao katika kipindi chote cha maisha yetu kutupa kile tunachokiita experience na katika kufanya hivyo ubongo ujikuta ukiendelea na kazi yake hata pale unapokuwa umelala.

Kile unachokiona katika ndoto ni mchanganyiko wa picha halisi za matukio unayoyafahamu na usiyoyafahamu (ambayo ubongo umejibunia kutokana na uzoefu)

Ndoto zina tafsiri au uwezo wa kubeba ujumbe kwa kuwa akili zetu zimehifadhi experience kubwa kuliko tunayotumia kila siku, kwa wale wanaoamini reincarnation wanafahamu kuwa akili yetu ina-nakili ya kumbukumbu zote za maisha yetu yanayojirudia hapa duniani.

Hivyo endapo jambo litakuwa linajirudia mara kwa mara katika ndoto au fahamu zako ni ishara kuwa ubongo umedetect same data kama za awali ambazo ziliwahi kutumika na hivyo ukizingatia au kuzipa usikivu jambo kama hilo au hilohilo lazima litajirudia tena katika maisha yako,

Hivyo endapo tukishapata uzoefu huu wa kila ubongo unapodisplay kitu fulani katika ufahamu wetu huu wa ndani(kupitia ndoto) na jambo fulani mara kwa mara linatokea automatic kifizikia hapo ndipo tunapofikia maamuzi ya alama na tafsiri ya ndoto hizo.
 
Mi nishawai kuota kuna uwazi mkubwa (tundu)kwenye mbingu,na pia nishawai kuota kiama
Ukielezea vizuri kwa kirefu tunaweza kupata picha japo kidogo ilikuaje ndoto yako na ilikuwa na ujumbe upi, mfano matukio yalivyokuwa mpaka mbingu ukaiona namna hiyo,ilikuwa ni mida gani wakati unaota, vipi hali yako ya Kiimani kwa nyakati hizo je ulikuwa ukimchamungu sana au ulikuwa ukifanya meditation, kuzimu uliona nini n.k
 
Karibu sana kwenye tafsri kuhusu ndoto.
Ndoto na Tafsri yake...
1. Ukiota unaruka kutoka juu MLIMANI,MTINI
👉TAMBUA KUNA WATU,MTU ANAPAMBANA kukushusha
CHINI ILA MWENYEZI MUNGU BADO ANAKULINDA KWAHIYO JITAHADHARI SANA.

2. UKIOTA UNAKULA NYAMA...
👉 (TAMBUA UMELISHWA TIYARI CHAKULA CHA KICHAWI SO UNATAKIWA
(UWAI DOZI MAPEMA)

3. UKIOTA UNAKIMBIZWA( NA UJAKAMATWA TAMBUA KIPINDI UMELALA UKUKUNJA MIGUU NDO MAANA UKUKAMATWA
👉(MAANA YAKE KUNA KITU KIBAYA KINAKARIBIA SO CHUNGA SANA MARAFIKI ZAKO .. UENDA KUNA MWENYE NIA MBAYA NA WEWE.

4. UKIOTA UNAPATA ELA NA UNAAMKA UONI ELA, HAPA HII NDOTO UWAGA INAWATOKEA/INATUTOKEA WENGI...
👉TAFSIDA YAKE NIKWAMBA UNAWEZA KUPOTEZA KITU CHA THAMANI SANA KWAHIYO CHUNGA SANA.

• ASANTE KWA LEO.... KAMA UNAHITAJI TAFSIR KUHUSU NDOTO COMMENT AFU NITAKUJIBU..
. endelea kushare kulike post zangu zote chanzo cha hii elimu Kimodomsafi
 
inaweza ikawa nje ya msaada lakini kwakua wewe ni mbobezi Nimeona sio mbaya nikiuliza.Imetokea nimeota napiga nyoka ndotoni alafu kesho yake nikamuona nyoka nje ya nyumba yangu nikampiga kweli hii ni ishara ya nini Mkuu?
 
inaweza ikawa nje ya msaada lakini kwakua wewe ni mbobezi Nimeona sio mbaya nikiuliza.Imetokea nimeota napiga nyoka ndotoni alafu kesho yake nikamuona nyoka nje ya nyumba yangu nikampiga kweli hii ni ishara ya nini Mkuu?

Kabla ya kukupa tafsiri ebu pitia mfano huu;

Katika maisha halisi unapomwona nyoka popote pale, cha kwanza unaogopa/kuingiwa na hofu kuwa utang'atwa lakini cha pili unawaza kujihami aidha kwa kukimbia au kumuua.

Alama za ndoto hii na maana zake;

Nyoka=Hisia mbaya

Kung'atwa=Kusalitiwa/kuumizwa

Kukimbia=kushindwa kukabiliana na hisia zako

Sumu= tatizo litakuelemea/kubwa

Kuua=kulikabili tatizo/mwanzo mpya

Nyoka mweusi=Adui

Nyoka wengi= hisia kuwa mahali ulipo si salama

Nyoka mrefu mno= ishara ya maisha marefu n.k

Hivyo kwa tafsiri rahisi katika ndoto uliyoota ulimuua nyoka kisha kesho tena ukamuua nyoka halisi; Mosi uliyoota si ndoto tu bali ni maono (ndoto zenye tafsiri ya wazi kwa mwotaji) Lakini kwa maana ya kiroho ni kuwa umeweza kuishinda hofu yako na sasa una uthubutu mpya katika sehemu fulani ya maisha yako.
 

Huwa sikumbuki kuota ndoto mara kwa mara
Week tatu zimepita nimeota nimejifungua mtoto wa kike mzuri sana,kiukweli hata mimi kwenye ndoto nilikuwa siamini kama ni wangu
Cha kushangaza watu wengi walikuwa wananipa hongera haswa maadui wananipongeza sana watu ambao hata hatuongei ila kwenye ndoto tumeongea
Kiufupi kila mtu alimfurahia huyu mtoto mimi pia
Maana yake inaweza kuwa nini?
 
Juzi nimeota natembea barabarani uchiii kabisa cha ajabu hakuna anaenishangaa na mimi nipo natembea tu hata sijizibi watu wasione....kwamba ndio nitaaibika maana yake???🤔
 
iyo ya kuendesha gari waga inanikumba sana, na si gari tu yani gari,pikpi,trekta ajabu ni kwamba natia gia nakanyaga moto chombo inatembea chakushangaza ni kuwa naendesha hatua kadhaa tu inazima na kugoma hata kuwaka na ndo unakuwa mwisho.

hii imekaaje!!
 
Mkuu kuna ndoto huwa inajirudia dia huwa namuota marehemu Bibi yangu mara kwa mara baadhi ya ndoto ninazozikumbuka ni kama vile (1)nimekutana nae mahali akaniambia huko aliko anaogopa sababu yuko peke yake,na mazingira tuliyokutana ni ya giza
(2)kulikuwa na baridi kali na mm naskia baridi hasa ktk kutembea tembea nikamkuta amekaa mahali chini amevaa koti la suti na aliponiona akavua akanipatia nikavaa huku yeye akiwa mtupu,ila muonekano wake ukiwa wa kisichana mana matiti yake yalikuwa wazi.
Na nyinginezo nyingi ambazo sizikumbuki vizuri,kwa hizo nn maana yake?
 

Mtoto wa kike ni ishara ya haiba/ubini wako wa ndani yaani uzuri wako wa ndani (tabia au roho nzuri)
Na kitendo cha kuzaa ni kufunguka kwa milango ya mafanikio (kuzaa kiumbe kipya) iwe ni kifedha, bahati au afya imara.Ni wazi kuwa utastawi bila vikwazo. (Maadui wanamlaki mwanao nakufurahia pamoja nawe)
 
Inamaanisha katika safari yako ya maisha bado kuna mikwamo kadhaa kila unapojaribu kupiga hatua unakumbana na ugumu.
 
Ni kweli ila kama una Imani ktk Yesu Kristo unaweza badilishaaa kwa maombi ktk Jina la Yesu na hayatatokea ktk Hali ya kifizikia.. Au mwili. La msingi uwahi tu kuomba Mara unapoamka.
 
Juzi nimeota natembea barabarani uchiii kabisa cha ajabu hakuna anaenishangaa na mimi nipo natembea tu hata sijizibi watu wasione....kwamba ndio nitaaibika maana yake???[emoji848]
Fikra za ndani ambazo ndiyo uhalisia wako zinajaribu kukuonesha kuwa upaswi kujali maoni ya watu au kipi wanawaza juu yako, bali ondoa dhana zinazokufanya usiwe huru/kupiga hatua au kubaki msiri kwa kuofia wengine wakati vitendo vyao havina madhara yeyote kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…