Habari ya kwenu jamani,
Naomba ushauri juu ya suala hili, nina rafiki yangu wa kike yeye anasema mara kwa mara amekua akiota anafanya mapenzi na wanawake tofauti tofauti, yani anaweza akaota anafanya romance na huyo mwanamke, lakini sura haionekani.
Pia amekua anaota anataka kufanya mapenzi na wanaume ila sura hawaoni ila anauwezo wa kushuka uume wao na anaota kama vile yuko nao live. Sometimes hao wanaume huwa wanakuja kwa sura ya kaka yake.
Je, inawezekana akawa ikawa ndio jini mahaba? Au ni kitu gani na je nimpe ushauri gani juu ya suala hili?
Na pia anasema katika maisha ya kawaida hata akifanya mapenzi na mwanaume hajawahi kusikia raha yoyote, je inawezekana ni hilo jini ndio limemshikilia.
Naombeni maoni yenu wadau nijue tunamsaidiaje mdada huyu.
Asanteni.