Orodha ya raisi wafuatano wanaweza kuingiza dunia kwenye vita kwasababu wana tatizo la wenge

Orodha ya raisi wafuatano wanaweza kuingiza dunia kwenye vita kwasababu wana tatizo la wenge

Pakome

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2024
Posts
1,651
Reaction score
1,129
Donald Trump

Ni raisi mwenye chokochoko hana tofauti na kidawa mpenda kufunua Makaburi na vyungu vya sumu ambavyo havikutakiwa kufunuliwa, kesha funua vyungu vingi vipo wazi vinatema sumu na sasa dunia nzima inakohoa

Kim Jong Un

Ni raisi mwenye mikono inayowasha sana anapenda kuchezea moto mwisho wake utachoma dunia ( Anapenda kucheza na Mabomu hatarishi amedhibitiwa tu na Sheria kinyume na hapo angelikuwa ameshalipua dunia )

Vladimir Putin

Ni raisi mwenye hasira za haraka ni kama anatumia sana pilipili kichaa, kosa la kuchapwa fimbo yeye anachapa na bunduki ni raisi mzuri kama hatachokozwa

Volodymyr Zelenskyy

Raisi wa Ukraine huyu amejawa na msongo wa mawazo ni raisi mzuri sana kinachomfanya aonekane mbaya ni uchokozi
Ni raisi anayetakiwa kuachwa apate muda wa kupumzika hapendi vita inamlazimu lakini inapomlazimu anaweza kuharibu dunia

Isaac Herzog

Raisi wa Israel huyu anatumia mgongo wa nchi Takatifu kusumbua watu akiamini nchi yake ina historia kubwa kwahiyo anaishi kwa kudeka akiamini lolote atakalofanya hata kama ni ovu ataogopwa kwani kwa historia ya Israel wana wake wanaamini kuwa wanaishi katika nchi Takatifu yenye historia kubwa

Endapo raisi hawa watadhibitiwa au kunyang'anywa mamlaka basi dunia itapona matatizo yake kwa zaidi ya asilimia 90%
 
Back
Top Bottom