Matojo Cosatta
JF-Expert Member
- Jul 28, 2017
- 234
- 390
ORODHA YA SHERIA ZINAZOTUMIKA KWENYE UCHAGUZI MKUU WA 2020.
SEHEMU 1: UTANGULI.
Kuna msurululu mrefu wa Sheria za ndani (municipal laws) zinazotumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2020. Sheria za ndani zinazotumika katika Uchaguzi Mkuu zimegawanyika katika aina kuu nne (4) zifuatazo;
(1) Sheria za Kikatiba
Sheria za Kikatiba ni masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kunga za kisheria (legal principles) za kikatiba ambazo zimetengenezwa na Mahakama Andamizi za Kumbukumbu (Superior Courts of Record) ikiwemo Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa katika mchakato wa utoaji haki na kutafsiri Katiba zinazohusu uchaguzi.
(2) Sheria Kuu
Sheria Kuu (Principal Legislation) ni sheria ambazo zimetungwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na mamlaka za kutunga sheria zingine zilizotangulia bunge au sheria za nchi za nje ambazo zimetangazwa na bunge kutumika Tanzania.
(3) Sheria Ndogo Ndogo.
Sheria Ndogo Ndogo ni sheria ambazo zimetungwa na taasisi ya umma au Kiongozi wa umma au mtumishi wa umma aliyekasimishwa (delegated) na bunge au katiba mamlaka ya kutunga sheria ikiwemo sheria za uchaguzi kwa niaba ya bunge. Kwa mfano, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekasimishwa na Bunge mamlaka ya kutunga Kanuni za Uchaguzi na Maelekezo ya Uchaguzi chini ya Kifungu cha 124 na 126 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 ambayo yanatumika katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020.
(4) Sheria Lamzi.
Sheria Lamzi (case law) hizi ni kunga za kisheria (legal principles) ambazo zimetengenezwa na Mahakama Andamizi za Kumbukumbu katika mchakato wa utoaji haki na kutafsiri sheria za uchaguzi .
SEHEMU 2: ORODHA YA SHERIA KIKATIBA.
Zifuatazo ni sheria za kikatiba ambazo zinatumika katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020;
(1) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977
(2) Sheria Lamzi za Kikatiba zinazohusika na uchaguzi.
SEHEMU 3: ORODHA YA SHERIA KUU.
Zifuatazo ni Sheria Kuu ambazo zinatumika katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020;
(1) Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 ( theNational Election Act, Cap. 343)
(2) Sheria ya Gharama za Uchaguzi, Sura 278 ( the Election Expenses Act, Cap. 287
(3) Sheria ya Mamlaka za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani), Sura 292 (the Local Authorities (Elections) Act, Cap. 292)
(4) Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura 258 (the Political Parties Act, Cap. 258)
(5) Sheria ya Makamishna wa Viapo na Wadhibitisha Nyaraka, Sura ya 12. ( the Commissioner for Oaths and Notary Public Act, Cap. 12
(6) Sheria ya Huduma ya Habari, 2016 (Media Service Act, 2016)
(7) Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, 2010 (the Electronic and Postal Communications Act, 2010)
(8) Sheria ya Tafsiri ya Sheria, Sura 1 (the Interpretation of Laws Acr, Cap. 1
(9) Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi, Sura 322 ( the Police Force and Axuxiliary Services Act, Cap. 322)
(10) Sheria ya Pesa za Serikali za Mitaa, Sura 290 ( the Local Government Finance Act, Cap 290)
(11) Sheria ya Siku Kuu, Sura ya 35
(12) Sheria ya Mahakama na Utumikaji wa Sheria, Sura ya 358 ( the Judicature and Application of Laws Act, Cap. 358)
(13) Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura ya 287 [ the Local Government (District Authorities) Act, Cap. 287]
(14) Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288 [the Local Government (Urban Authorities) Act, Cap. 288]
SEHEMU 4: ORODHA YA SHERIA NDOGO NDOGO.
Zifuatazo ni Sheria Ndogo Ndogo ambazo zinatumika katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020;
(1) Kanuni za Uchaguzi wa Taifa (Uchaguzi wa Rais na Wabunge), 2020 (Tangazo la Serikali Na. 401 la 2020).
(2) Kanuni za Mamlaka za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani), 2020 (Tangazo la Serikali Na. 402 la 2020).
(3) Maadili ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020 (Taarifa ya Kawaida Na. 722 ya Gazeti la Serikali, Toleo la 23, Juzuu Na. 101)
(4) Notisi ya Majimbo na Wilaya za Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 2020 (Tangazo la Serikali Na. 599 la 2020).
(5) Amri ya Kutangaza Siku ya Uchaguzi kuwa Siku Kuu, 2020 (Tangazo la Serikali Na. 578 la 2020)
(6) Kanuni za Uchaguzi wa Taifa (Mashauri ya Uchaguzi), 2010 (Tangazo la Serikali Na. 447 la 2010).
(7) Mabadiliko ya Kanuni za Uchaguzi wa Taifa (Mashauri ya Uchaguzi), 2010 (Tangazo la Serikali Na. 106 la 2010).
(8) Kanuni za Mamlaka za Mitaa ( Mashauri ya Uchaguzi ), 2020 (Tangazo la Serikali Na. 448 la 2020).
(9) Kanuni za Gharama za Uchaguzi, 2010 (Tangazo la Serikali Na. 246 la 2020)
(10) Amri ya Gharama za Uchaguzi (Kiwango cha Juu cha Fedha), 2015 (Tangazo la Serikali Na. 325 la 2015).
(11) Fedha za Serikali za Mitaa (Ushuru wa Mabango, Vipeperushi na Fremu za Matangazo), 2019 (Tangazo la Serikali Na. 157 la 2019).
(12) Kanuni za Ushuru wa Huduma za Mahakama, 2018 (Tangazo la Serikali Na. 247 la 2020).
(13) Maelekezo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi, 2020
(14) Maelekezo kwa Vyama vya Siasa na Wagombea, 2020.
(15) Maelekezo ya Mambo Muhimu ya Kuzingatia kwa Wasimamizi wa Uchaguzi kwa Uchaguzi wa Mwaka 2020.
(16) Mwongozo wa Elimu ya Mpiga Kura Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020
(17) Mwongozo wa Watazamaji wa Ndani na wa Kimataifa wa Uchaguzi wa 2020
(18) Kanuni za Vyama vya Siasa (Usajiri na Ufuatiliaji), 2019 (Tangazo la Serikali Na. 953 la 2019).
(19) Maadili ya Vyama vya Siasa, 2019 (Tangazo la Serikali Na. 954 la 2019)
(20) Maadili ya Huduma ya Utangazaji wa Maudhui ya Uchaguzi wa Vyama vya Siasa, 2015 ( Tangazo la Serikali Na. 228 la 2015).
(21) Kanuni za Huduma ya Habari, 2017 (Tangazo la Serikali Na. 18 la 2017).
(22) Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Utangazaji wa Maudhui Katika Redio na Televisheni), 2020 ( Tangazo la Serikali Na. 134 la 2018)
(23) Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ( Maudhui ya Mtandaoni),2020 (Tangazo la Serikali Na. 538 la 2018)
(24) Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Kumlinda Mteja),2020 (Tangazo la Serikali Na. 61 la 2018)
Imeandaliwa na Matojo M. Cosatta.