Mkuu ni vigumu sana kujua siri ya mafanikio na utajiri mtu!
Ila ni vema ukatofautisha kupata fedha kipindi fulani na kuwa tajiri.
Wengii wanazipata pesa na baada ya muda pesa zinaweza kuwakimbia. Tajiri ni mtu ambaye ana mfumo/mzunguko wa kumuingizia pesa na kuitunza pesa hivyo ana uwezo wa ku maintain hadhi ya kuwa na pesa/mali kwa muda. Kuwa tajiri siyo kazi rahisi.
Note: kupata pesa nyingi kwa mpigo bila kujari chanzo chake ni sababu pekee ya kumfanya mtu kuwa tajiri, hivyo sio guarantee kuwa ukipata pesa tu wewe unakuwa tajiri. Amini nakuambia kuizungusha na kutunza pesa ni jambo gumu sana kuliko kupata pesa kwa mkupuo! Amini hivyo!
Zipo Njia kuu tatu za kupata pesa/mali nyingi.
1. Njia ya kwanza ni haramu: ikijumuisha wizi, uporaji, rushwa, kutoa kafara, kuingia mikataba hasi ya kiimani na kudhurumu. Wapo wapo wachache wakipata mali/pesa kwa njia hii wanaoweza kuzitunza na kuzizungusha na kuwa matajiri.
2. Njia ya pili ya kuwa tajiri ni kubahatika kupitia njia mbalimbali zikiwemo Kamari, kurithi, na kuwa katika strategic location/locality au position (e.g ardhi iliyogundulika kuwa na madini, eneo ulilopo kuwa mkabala na investment inayokufanya uwe katika competitive advantage kibiashara (oposite na aiport/uwanja wa mpira/ serengeti/ ngorongoro n.k).
3. Njia ya tatu ya kupata pesa na baadaye utajiri ni kuwa na uwezo wa kutengeneza ziada, kudunduiza na kuwekeza sehemu sahihi. Ili utoboe kwa njia hii unatakiwa uwe mbele zaidi ya wenzano katika mazingira uliyopo. Kuna njia mbalimbali za kukufanya upate ziada lakini kubwa zaidi ni kuwa na maarifa ya ziada kuliko wenzako. Maarifa ya ziada yanapatika kupitia njia kuu nne ambazo ubunifu, kipaji cha kuzaliwa, elimu na exposure. Njia hii ni ngumu kuliko nyingine kwani ina kupanda na kushuka na inachukua muda kufanikiwa. Itakuhitaji siyo chini ya 10 years kuwa tajiri kupitia njia hii. Njia pekee ya mkato ni kupitia talent za michezo, sanaa n.k.
Note: kuna watu wengi wanaingiza kiasi cha TZS 35,000,000 au zaidi kwa mwezi na wanapata kiasi hicho kwa miaka 5 au zaidi mfululizo lakini wameshindwa kuwa matajiri kwa sababu hawana maarifa ya utajiri, hivyo wanashindwa kudunduiza na kuwekeza sehemu stahili. Wengi wa watu wa aina hii wakitoka tu katika njia za kupata kipato husika ugeuka masikini wa kutupwa.
Pia, watu wanaopata mafanikio ya haraka kwa njia za kafara huwa hawawezi kubainisha njia za mafanikio yao kwa sababu kuna unjustice nyingi wamefanya, na mwisho wao huwa siyo mwema. Huwa wanateseka sana. Ndio maana inashauriwa usitamani kuwa kama mwingine tengeneza njia zako.
Mwisho, kama unataka uwe na utajiri wa halali Muombe Mungu sana, toa sadaka halali na punguza kuvunja amri kuu za Mungu.
Mungu atusaidie bila yeye hatuwezi