Orodha ya wabunge bubu bungeni yawekwa hadharani

Orodha ya wabunge bubu bungeni yawekwa hadharani

Vipi likianzishwa bunge la mabubu na RA awe Spika wao?
 
Sasa unategemea waziri mkuu au waziri wa fedha apige kelele za nini bungeni? Na haya leo tunayaona pia kwa Mramba ambaye akiwa waziri wa fedha amepeleka miradi ya ujenzi wa barabara jimboni kwake pesa ambazo zilitakiwa zitumike kujenga barabara sehemu nyingine.

Alafu njoo sasa kwa Waziri Mkuu wa sasa Mizengo Kayanza Pinda amepiga route mara ngapi kwa wapiga kura wake kule ...dah usipime mkuu anataka Sumbawanga iwe juu kama Mbeya sehemu za Lindi na Ntwara mtaendelea kusubili maendeleo na nyie pigeni debe Mdhihiri awe waziri mkubwa mwakani.
 
Inavyoelekea ni kwa kiasi gani wabunge ambao wapo hawajui maana halisi ya ubunge ndio maana wapo hapo kwa hisia zao za kupata wapi hela kupitia miradi yao na sio kuwatumikia wananchi kama walivyoahidi.

Inawezekana mtandao wa JF unaweza kuwa-brush ili wajue nini cha kufanya ninawashauri wausome ili waone wako wapi? wanakwenda wapi?
 
Niliwahi kusema kuhusu RA na Bungeni, sio tuu hajawahi kuchangia, bali kipindi anachohudhuria kikao cha Bunge, akikaa sana ni siku 3 tuu. Sijawahi kumuona zaidi ya siku 3 mfululizo. Yeye na mkono, huja Dodoma na ndege zao. ya Mkono huridi Dar kusubiri kuja kumchukua. Ya RA humsubiri hapo Airport ya Dodoma.

RA haulizi swali lolote kwa sababu matatizo yote ya wananchi wake anayamaliza mwenywe kwa fedha yake ya mfukoni.

Pia hachangii hoja yoyote kwa vile kichwani hamna kitu, hata ukimuona kwa macho tuu usoni, hilo utaliona wazi.

Kuna baadhi ya wabunge hawachangii lolote kwa sababu wamesusa baada ya kukatiwa ulaji. Ila pia kuna wasio changia kwa sababu hawaoni umuhimu wowote kuchangia japo vichwani wako fiti, lakini kuna hawa wasiochangia kwa vile vichwani hawana kitu, japo pesa wanazo.
Hivi kweli wananchi wakielimishwa kuhusu majukumu ya mwakilishi wao Bungeni, bado watawachagua mabubu?.

Hii ya kichwani kama hana kitu ndio maana hachangii......mh! mpya.

Remember jamaa ni Oxford Graduate! uliza heshima na entries requirements za wanaotaka kujiunga na Oxford.....

Simtetei ila jamaa upstairs is very bright than you can imagine.

At his late thirties ni very influential and power individual this country has ever had! hii yote inasababishwa na bongo yake kuwa na akili za ziada.

Je kuchangia na kuuliza saana ndo ujiniasi....tupeni takwimu za almarhuum Amina bungeni.
Kingwele.
 
Remember jamaa ni Oxford Graduate! uliza heshima na entries requirements za wanaotaka kujiunga na Oxford.....

Du kali hii, alisoma mwaka gani na kozi gani mkulu, tumtafute ? ama umetengeneza hii muzee?
 
Jamani ee, Inawezekana mbunge haoni matatizo katika jimbo lake au hata katika nchi, hivyo anakuwa hana cha kuuliza wala cha kuchangia. Ila kubwa nadhani wamezoea shida hivy kuziona kama raha, otherwisw hawafai
 
Bhagosha,

Duh nimewasoma wote na hoja zenu zote ni nzito ful ful, nanyi ni wanaharakati kweli wa mapinduzi na ni wazalendo ful ful,ila kuna kitu kimoja tu ndio sijakipata toka kwenu:

Maoni yenu kwa watanzania wazalendo wenzenu

wafanye nini kwa uchaguzi ujao esp kwa wale wasomao JF na kuwashauli wale wasio kuwa na access na JF?

Najua kweli mumeenda vidato na wengine mna akili kweli zakuzaliwa na wengine tu kwa upeo wa kuona matendo tu ya kisiasa,uongozi wa serikali ilioko madarakani na ahadi zake tu na waweza nyambulisha jambo, sasa je mumejiandikisha kwa kupiga kura 2010? maana hapo ndipo patashika inapo anzia.au twachangia na kuto dukuduku zetu bila fanyia kazi au kuhamasisha?

Lastly, Mwazania lini mapinduzi halisi yatafika au kufanyika lini?, ili hali twajua fika hali halisi ya nchi yetu iendavyo kisiasa,kiuongozi,kimaendeleo,kiuchumi na kadharika.
 
RA ndie anatisha!!! hata wakati sakata la richmond mbali na kuwa implicated hakuongea chochote!!! lol
 
John Komba yeye amewahi kuuliza au kuchangia lini???
Au yeye anachangia kwa nyimbo?????????
 
kwani kuuliza swali sifa?

wananchi wanaowakilishwa kama wanapata maji,dawa, shule,na mengineyo maswali ya nini?

hao wanaoluliza maswali kila kukicha wamefikia wapi?

Na walichaguliwa kwenda Bungeni kufanya nini?kuwa kama betri za magari?
 
..wabunge wengine kazi yao ni kusakama mawaziri tu lakini ukichunguza hakuna chochote cha maana walichokifanya majimboni kwao.
 
kama baba wa taifa angekuwa hai leo hii huyu anaitwa Mh Rostam azizi sijui kama hata ofisi ya kata ya chama cha mapinduzi angezisogelea yetu macho ukisema utaambiwa unabagua rangi sjui udini jaamm ni hatari!! kupita tunavyofikiria
 
Hivi wewe GT ndo Rostam Aziz mwenyewe nini?

Yaani miaka 4 hata kufungua mdomo hakuna! Huyu jamaa yuko bungeni kwa maslahi yake binafsi tu wala hana shida na maendeleo ya wadanganyika. Yeye ni kwenda bungeni kutengeneza chanels zake za kuinyonya hii nchi tu basi. Rostam Aziz ni hatari sana kwa maendeleo ya taifa letu. He is too wicked I can say.
2010 wadanganyika watamrudisha tena.Pesa kweli sabuni ya roho atawapepea na vijisenti then tena huyo bungeni kupiga miayo na miusingizi huku akusubiri posho.
 
haya mambo ya kulazimishana kusema sijui yametokea wapi

Mwakyembe na kelele zake kawapelekea wananchi wa jimbo lake maendeleo gani?

Nadhani tuendelee kufundishana humu JF; Mbunge hapeleki maendeleo jimboni bali anawajibika kusimamia serikali ibuni na kutekelza mipango ya maendeleo jimboni kwake na nchi nzima. Wasomi wa JF vipi? Mwakyembe siyo wa kubeza, ameisimami serikali vilivyo hadi kubomoa njama za wezi wa Richmond/Monduli.
 
Bora ya hao wanaokaa kimya na kuelewa manake hakuna michango zaidi ya 300 isijirudie na kama kila mmoja akitoa pendekezo tofauti hatuna serikali itakayo weza kutekeleza.

Kubwa kuna wabunge wengi wanabofoa kuliko kutoa hoja za maana, wabunge viwango hawafiki 20% (less than 20% kwa ajili ya ku-qualify 80/20 rule), isipokuwa wengi wanauza sura na kuunga mkono hoja pamoja na kupongeza kulikopita kiasi.

Hoja nyingi zinajirudia kila kukicha na maswali mengine majibu wanayo.
 
Back
Top Bottom