Ghiti Milimo
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 4,748
- 7,061
Maana yake?🕊️PSP
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maana yake?🕊️PSP
CDF kaandika mpka kitabu cha dini, kina uzwa huko kwa wakatoliki na pesa zote zinazo patikana ni kwa ajiri ya kanisa, hachukui hata sentTrue
Kwa wakati mmoja Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa na CDF walikuwa Viongozi wa Kanisa!
Polen sana kwa kuwa na ubongo unaotafsir mada zao ni za kidin.ORODHA YA WAKURUGENZI WAKUU WA 'TISS' TANGU UHURU.
Idara ya usalama wa Taifa (TISS) imeundwa kwa sheria ya bunge namba 15 ya mwaka 1996 (Tanzania Intelligence and Security Service act No. 15 of 1996) iliyosainiwa na Rais Benjamin Mkapa tarehe 20 mwezi Januari mwaka 1997. Sheria hiyo ndio inayoipa mamlaka Idara hiyo kufanya kazi zake ndani na nje ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Pamoja na idara hii kusajiliwa kisheria mwaka 1996, lakini ilkuwepo tangu wakati wa utawala wa kikoloni chini ya ofisi ya Gavana wa Tanganyika. Baada ya Uhuru mwaka 1961 ilihamishiwa ofisi ya Rais.
Tangu idara hii kuanzishwa hadi sasa imeongozwa na Wakurugenzi 9 akiwemo Diwani Athumani Msuya aliyepo kwa sasa
Wa kwanza ni mzee Emilio Mzena, huyu aliongoza mwaka 1961 hadi mwaka 1975. Ndiye Mkurugenzi wa TISS aliyeongoza idara hii kwa miaka mingi zaidi kuliko wengine (miaka 14). Aliaminiwa na Mwalimu Nyerere baada ya idara yake kuzima majaribio kadhaa ya kumpindua.
Wa pili ni Dr. Lawrence Gama (PhD). Huyu alipokea kijiti kutoka kwa Mzena. Aliongoza kwa miaka mitatu tangu mwaka 1975 hadi mwaka 1978, kabla ya Mwalimu Nyerere kumuondoa katika nafasi hiyo na kumteua kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma.
Wa tatu ni Dr. Hassy Kitine (PhD) ambaye aliongoza idara hii kwa miaka miwili toka mwaka 1978 hadi 1980. Kitine alichaguliwa kuongoza idara hiyo nyeti akiwa kijana wa miaka 36 tu. Anakumbukwa kwa jinsi alivyoiwezesha TISS kushirikiana na Idara ya Usalama na Utambuzi Jeshini (MI) Chini ya Meja Jenerali Tumainieli Kiwelu, kuiteka nyara ndege ya makomandoo kutoka Libya iliyokuja kumsaidia Idd Amin katika vita ya Kagera.
Mwaka 1980 Mwalimu Nyerere alimteua kijana mwingine mwenye miaka 35 Dr. Agustine Mahiga (PhD) - (Marehemu) ambaye alikuja kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na baadaye Waziri wa Sheria chini ya Hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli - kuwa Kaimu Mkurugenzi mkuu wa TISS. Alikaimu nafasi hiyo hadi mwaka 1983, Nyerere alipomuondoa na kumteua Kaimu Balozi wa Tanzania (Minister Plenipotentiary) nchini Canada.
Baada ya Mahiga kwenda Canada, Mwalimu Nyerere alimteua Luteni Jenerali Imrani Kombe kuwa Mkurugenzi mkuu wa 5 wa TISS mwaka 1983. Nyerere alipong'atuka alimuacha Kombe kwenye idara hiyo na alidumu hadi mwaka 1995.
June 30 mwaka 1996 Jenerali Kombe aliuawa na Jeshi la polisi kwa madai kuwa walifananisha gari lake (Nissan Patrol) na gari iliyokua imeibiwa na mtuhumiwa Ernest Mushi maarufu kama "White".
Alimininiwa risasi 4 kifuani licha ya kushuka kwenye gari na kunyoosha mikono juu kama ishara ya kusurrender. Askari waliohusika na mauaji hayo walihukumiwa kunyongwa lakini Rais Kikwete aliwapunguzia adhabu mwaka 2011. Bado kifo cha Jenerali Kombe kina maswali mengi kuliko majibu.
Baada ya Kombe kuuawa alifuata Kanali Apson Mwang'onda. Huyu aliteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa 6 wa TISS ambaye aliongoza Idara hiyo hadi mwaka 2005 alipostaafu. Kanali Mwang'onda anasifiwa kwa kuifanyia marekebisho makubwa idara ya TISS ya kimfumo na kiutendaji. Ndiye aliyewezesha muswada uliounda sheria ya TISS mwaka 1996.
Mwaka 1980 Mwalimu Nyerere alifanyiwa jaribio kubwa la kutaka kupinduliwa na baadhi askari wa JWTZ (akina Tamin, McGhee na Kepteni Maganga) . Hili lilikua jaribio la 3 kubwa la kumpindua Nyerere, lakini ni jaribio la 7 katika orodha ukijumlisha na mengine madogo. Kanali Apson Mwang'onda akiwa Mkurugenzi wa ndani wa TISS (DOI) alifanikiwa kuzima jaribio hilo. Historia hii ilimuongezea sifa ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi mkuu wa TISS mwaka 1995.
Mwaka 2005 Rais Jakaya Kikwete alimteua Othman Rashid kuongoza Idara hiyo hadi mwaka 2016 alipostaafu. Othmna Rashid alikuwa Mkurugenzi wa 7 wa idara hiyo.
August 24 mwaka 2016 Rais John Magufuli alimteua Mchungaji Dr. Modestus Kipilimba (PhD) wa Kanisa la City Harvest Church la jijini Dar es Salaam kuwa Mkurugenzi Mkuu wa 8 wa TISS. Kabla ya uteuzi huo Kipilimba alikua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya taifa (NIDA).
Mchungaji Dr. Kipilimba amedumu katika nafasi hiyo hadi September 12 mwaka 2019 alipotenguliwa uteuzi wake na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna wa Polisi CP Diwani Athumani Msuya.
Kwenye nchi zetu za Commonwealth Ilikuwa ni "Special Branch", chombo cha Ikulu. Pengine walikuwa na sheria zao huko ndani, lakini formally hakuna kokote ilikuwa inajulikana.Kwa miaka 35 tangu uhuru hadi mwaka 1996 hakukuwa na sheria ya TISS?
Umenikumbusha hili tukio wakati limetokea lilizizima Morogoro ila sikuwa na utambuzi mkubwa. Naomba nikumbushe mkuu kama hutajali.DSTV kuna mpaka Majambazi wa Silaha ambao huo ujambazi ni sehenu ya Kasi zao
Umewahi kupata kuelezwa namna Hayati Prof Nikas Mahinda aliekuwa Mbunge wa Morogoro alivyovamiwa na kuuawa nyumbani kwake?
Mpare pia.Nimesomaaa weeee ila nimeona MHAYA, MNYAKYUSA na mchagga barikiwa wasukuma
Una uhakika? 😡😡🙄CP Msuya amekuwa The worst DG to be, With all resources ila still Ameruhusu amiri jeshi Mkuu kuondoka mikononi mwake, Ila pia interesting ni kuwa Vijana wa Zamani walikuwa so ambitious imagine Mahige amekaimu Ukuu wa idara nyeti kabisa at 35 Age, Njoo kwa Kitine nae at 36, Ila kwa sasa kijana wa miaka 35 kumuamini ni Ngumu sana mana Mzee alijaribu kuwaamini watu kama Makonda,Sabaya na Hapi ila matokeo yake wote tumeyashuhudia
B.W. Mkapa ndio alikuja kusaini iyo act na officially TISS ikawa identified ila kuanzia Kipindi cha kina Mzena TISS ilikuwa Chini ya ofisi ya Rais wala haikuwa identified legallyKwa miaka 35 tangu uhuru hadi mwaka 1996 hakukuwa na sheria ya TISS?
Heshima yako mkuu nimeliona jina lako idara ya usalama.Mpare pia.
Kwa maneno mengine Msuya ndiye aliyemwua rais. Amefeli majukumu yake.CP Msuya amekuwa The worst DG to be, With all resources ila still Ameruhusu Amiri jeshi Mkuu kuondoka mikononi mwake, Ila pia interesting ni kuwa Vijana wa Zamani walikuwa so ambitious imagine Mahiga amekaimu Ukuu wa idara nyeti kabisa at 35 Age, Njoo kwa Kitine nae at 36, Ila kwa sasa kijana wa miaka 35 kumuamini ni Ngumu sana mana Mzee alijaribu kuwaamini watu kama Makonda,Sabaya na Hapi ila matokeo yake wote tumeyashuhudia
Jamaa naona mnazidi msagia kunguni.. Nafikiri katika maisha ya utumishi .. hii nafasi imekuwa kaa la moto kwake. Bora angebakiaga na u DCI wake tuKwa maneno mengine Msuya ndiye aliyemwua rais. Amefeli majukumu yake.
True
Kwa wakati mmoja Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa na CDF walikuwa Viongozi wa Kanisa!
Tufanunulie mkuu kusuhu hospital ya MzenaTISS, Shukran wengine hawakujua kwann ile Hospital inaitwa Mzena hahaa....na walishangaa tu, Mzena ndo hospital gan na iko wapi?
Tufanunulie mkuu kusuhu hospital ya Mzena
Hospital hiyo ipo wapi??Ni hospitali iliyo chini ya idara ya usalama wa taifa, kama ilivyo Hospitali ya Lugalo kwa JWTZ na hospitali ya Kurasini Baracks kwa jeshi la polisi.
Imepewa jina la mzena kumuenzi mkurugenzi wake wa kwanza wa idara aliyeitwa Emilio Mzena
Kimsingi TISS imeanzishwa wakati wa Mkapa.Kwa miaka 35 tangu uhuru hadi mwaka 1996 hakukuwa na sheria ya TISS?
Rais hataki kuvaa barakoa in the middle of a pandemic wakati ana matatizo ya moyo na mpaka wasaidizi wake wa karibu wanafariki kwa Covid-19.Kwa maneno mengine Msuya ndiye aliyemwua rais. Amefeli majukumu yake.
YaaniRais hataki kuvaa barakoa in the middle of a pandemic wakati ana matatizo ya moyo na mpaka wasaidizi wake wa kqribu wanafariki kwa Covid-19.
Anawashushua wanaovaa barakoa, mpaka kanisani, hataki chanjo, hataki watu wapimwe. Hataki isolation.
Kapigwa daflao unamlaumu Msuya?
Hapa ni case ya "Mwana kulitafuta, mwana kulipata" tu.
Msuya anaweza kuwa na matatizo mengi, lakini kifo cha rais Magufuli alijitakia Magufuli mwenyewe kwa uzembe wake na ubishi wake wa kukataa sayansi, licha ya kuwa na Ph.D ya Chemistry, na kuendekeza propaganda za siasa.
Kwa kweli ukiangalia matatizo yake ya moyo, Magufuli hakutakiwa hata kugombea kazi yenye mikiki kama urais, kagombea urais kwa sababu ya uroho wake wa madaraka tu.
Sasa mtu kama huyo ambaye hashauriki wala hapangiwi, akifa, utamlaumu vipi Msuya?