Orodha ya Wakurugenzi Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) tangu Uhuru

Orodha ya Wakurugenzi Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) tangu Uhuru

ORODHA YA WAKURUGENZI WAKUU WA 'TISS' TANGU UHURU.

Idara ya usalama wa Taifa (TISS) imeundwa kwa sheria ya bunge namba 15 ya mwaka 1996 (Tanzania Intelligence and Security Service act No. 15 of 1996) iliyosainiwa na Rais Benjamin Mkapa tarehe 20 mwezi Januari mwaka 1997. Sheria hiyo ndio inayoipa mamlaka Idara hiyo kufanya kazi zake ndani na nje ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Pamoja na idara hii kusajiliwa kisheria mwaka 1996, lakini ilkuwepo tangu wakati wa utawala wa kikoloni chini ya ofisi ya Gavana wa Tanganyika. Baada ya Uhuru mwaka 1961 ilihamishiwa ofisi ya Rais.

Tangu idara hii kuanzishwa hadi sasa imeongozwa na Wakurugenzi 9 akiwemo Diwani Athumani Msuya aliyepo kwa sasa

Wa kwanza ni mzee Emilio Mzena, huyu aliongoza mwaka 1961 hadi mwaka 1975. Ndiye Mkurugenzi wa TISS aliyeongoza idara hii kwa miaka mingi zaidi kuliko wengine (miaka 14). Aliaminiwa na Mwalimu Nyerere baada ya idara yake kuzima majaribio kadhaa ya kumpindua.

Wa pili ni Dr. Lawrence Gama (PhD). Huyu alipokea kijiti kutoka kwa Mzena. Aliongoza kwa miaka mitatu tangu mwaka 1975 hadi mwaka 1978, kabla ya Mwalimu Nyerere kumuondoa katika nafasi hiyo na kumteua kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma.

Wa tatu ni Dr. Hassy Kitine (PhD) ambaye aliongoza idara hii kwa miaka miwili toka mwaka 1978 hadi 1980. Kitine alichaguliwa kuongoza idara hiyo nyeti akiwa kijana wa miaka 36 tu. Anakumbukwa kwa jinsi alivyoiwezesha TISS kushirikiana na Idara ya Usalama na Utambuzi Jeshini (MI) Chini ya Meja Jenerali Tumainieli Kiwelu, kuiteka nyara ndege ya makomandoo kutoka Libya iliyokuja kumsaidia Idd Amin katika vita ya Kagera.

Mwaka 1980 Mwalimu Nyerere alimteua kijana mwingine mwenye miaka 35 Dr. Agustine Mahiga (PhD) - (Marehemu) ambaye alikuja kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na baadaye Waziri wa Sheria chini ya Hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli - kuwa Kaimu Mkurugenzi mkuu wa TISS. Alikaimu nafasi hiyo hadi mwaka 1983, Nyerere alipomuondoa na kumteua Kaimu Balozi wa Tanzania (Minister Plenipotentiary) nchini Canada.

Baada ya Mahiga kwenda Canada, Mwalimu Nyerere alimteua Luteni Jenerali Imrani Kombe kuwa Mkurugenzi mkuu wa 5 wa TISS mwaka 1983. Nyerere alipong'atuka alimuacha Kombe kwenye idara hiyo na alidumu hadi mwaka 1995.

June 30 mwaka 1996 Jenerali Kombe aliuawa na Jeshi la polisi kwa madai kuwa walifananisha gari lake (Nissan Patrol) na gari iliyokua imeibiwa na mtuhumiwa Ernest Mushi maarufu kama "White".

Alimininiwa risasi 4 kifuani licha ya kushuka kwenye gari na kunyoosha mikono juu kama ishara ya kusurrender. Askari waliohusika na mauaji hayo walihukumiwa kunyongwa lakini Rais Kikwete aliwapunguzia adhabu mwaka 2011. Bado kifo cha Jenerali Kombe kina maswali mengi kuliko majibu.

Baada ya Kombe kuuawa alifuata Kanali Apson Mwang'onda. Huyu aliteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa 6 wa TISS ambaye aliongoza Idara hiyo hadi mwaka 2005 alipostaafu. Cornel Mwang'onda anasifiwa kwa kuifanyia marekebisho makubwa idara ya TISS ya kimfumo na kiutendaji. Ndiye aliyewezesha muswada uliounda sheria ya TISS mwaka 1996.

Mwaka 1980 Mwalimu Nyerere alifanyiwa jaribio kubwa la kutaka kupinduliwa na baadhi askari wa JWTZ (akina Tamin, McGhee na Kepteni Maganga) . Hili lilikua jaribio la 3 kubwa la kumpindua Nyerere, lakini ni jaribio la 7 katika orodha ukijumlisha na mengine madogo. Cornel Apson Mwang'onda akiwa Mkurugenzi wa ndani wa TISS (DOI) alifanikiwa kuzima jaribio hilo. Historia hii ilimuongezea sifa ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi mkuu wa TISS mwaka 1995.

Mwaka 2005 Rais Jakaya Kikwete alimteua Othman Rashid kuongoza Idara hiyo hadi mwaka 2016 alipostaafu. Othmna Rashid alikuwa Mkurugenzi wa 7 wa idara hiyo.

August 24 mwaka 2016 Rais John Magufuli alimteua Mchungaji Dr. Modestus Kipilimba (PhD) wa Kanisa la City Harvest Church la jijini Dar es Salaam kuwa Mkurugenzi Mkuu wa 8 wa TISS. Kabla ya uteuzi huo Kipilimba alikua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya taifa (NIDA).

Mchungaji Dr. Kipilimba amedumu katika nafasi hiyo hadi September 12 mwaka 2019 alipotenguliwa uteuzi wake na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna wa Polisi CP Diwani Athumani Msuya.

Kuhusu Dr Lawrence Gama, nadhani umekosea kwani mimi nilisoma na mtoto wake mwaka 1976 wakati akiwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma.
 
Unaweza ukaongelea kidogo hii misheni namna ilivyotekelezwa, kama taarifa zake siyo classified?
Bado sijaweza kuiamini hii Mada km ni ya kweli kuwa Usalama wa Taifa kwani amecopy na ku Paste kutoka kwa Malis G J (Libya walipotea wakatua Nairobi ndipo taarifa zikatua JW sio UWT) hapo hakuna ukweli wowote ila kuna sehemu humu JF pameelezewa na picha za hao viongozi
 
Hawa watu mimi nilikuwa naona ni bora zaidi wawe wanatoka Jeshini. Aidha Mkuu wake anakuwa ametoka JWTZ halafu msaidizi wake Polisi (Usalama wa raia au magereza), au the vice versa. Hii kazi kwa mtu ambaye ni raia perce na ambaye hana affliation yoyote na vyombo hivi vya ulinzi na usalama nadhani huwa inakuwa ni mzigo kidogo kwake, na ninadhani kati ya hawa waliotajwa hapa wengi wao walitokana na vyombo hivi
 
DSTV kuna mpaka Majambazi wa Silaha ambao huo ujambazi ni sehenu ya Kasi zao

Umewahi kupata kuelezwa namna Hayati Prof Nikas Mahinda aliekuwa Mbunge wa Morogoro alivyovamiwa na kuuawa nyumbani kwake?
Lete maneno mkuu, wengine tumezaliwa juzi tu.
 
Hawa watu mimi nilikuwa naona ni bora zaidi wawe wanatoka Jeshini. Aidha Mkuu wake anakuwa ametoka JWTZ halafu msaidizi wake Polisi (Usalama wa raia au magereza), au the vice versa. Hii kazi kwa mtu ambaye ni raia perce na ambaye hana affliation yoyote na vyombo hivi vya ulinzi na usalama nadhani huwa inakuwa ni mzigo kidogo kwake, na ninadhani kati ya hawa waliotajwa hapa wengi wao walitokana na vyombo hivi
Vyeo vya wale jamaa ni top secret, pia waajiriwa wote wa TISS except 'informers' wanapitia mafunzo ya kijeshi. Mafunzo yao ni ya hali ya juu.. ukichanganya na 'karate ' na ujasusi. Mafunzo yao yanaenda mpaka miezi 10 au zaidi kulingana na nafasi watakayokupa.

Mind you wakikuchukua basi wanajua utafaa kitengo kipi... Ndio maana Kuna. TISS police, JWTZ, UHAMIAJI NK. kila kwenye kundi fulani la watu na wao pia wana mtu wao.

Katiba ya nchi yetu imekibana sana hichi chombo, kazi yao kuu kwa mujibu wa katiba (TANZANIA INTELLIGENCE AND SECURITY SERVICES ACT, 1996) inawataka kutafuta taarifa zote za kiusalama, kuchuja, na kushauri juu ya hatua za kuchukua basi. Ndio maana huwezi kuona watu wa usalama wanakamata mtu au kufanya kitu chochote cha kuonekana.

Nchi za wenzetu chombo kama hiki ni huru, hakina mipaka katika kulinda, na kutunza mustakabali wa nchi... Kwetu wanasiasa wanaogopa kukipa mamlaka kamili, badala wanatumia baadhi ya maafisa kwa faida zao binafsi

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Unasahau TISS ni Taasisi ya kiraia (Civilian) Wanajeshi wachache ni broad minded ndio maana Pamoja na Jeshi kuwa na Community yao Millitary Intelligence(MI) Lakini hii ya kiraia inabaki kuwa the best kuanzia kwenye mambo ya Gathering mpaka analysis, The best analysts ni wenye mtazamo wa Kiraia, Ni siasa tu zilivuruga idara yetu ila bado iko Juu
 
Vyombo vingi vya kijasusi, vinatoaga mchoro kwa vyombo husika then hukamata, ila wao kukamata ni nadra
 
Sio kweli
Aliejenga uwanja wa Tabora
Na uwanja wa Sumbawanga..Nelson Mandela stadium alikuwa Tumainiel Kiwehlu..
 
Bado sijaweza kuiamini hii Mada km ni ya kweli kuwa Usalama wa Taifa kwani amecopy na ku Paste kutoka kwa Malis G J (Libya walipotea wakatua Nairobi ndipo taarifa zikatua JW sio UWT) hapo hakuna ukweli wowote ila kuna sehemu humu JF pameelezewa na picha za hao viongozi

TISS Ilikuwepo muda mrefu sana inawezekana kulikuwa hakuna sheria, lakini mimi nimeelewa uwapo wa TISS tangu miaka hiyo ya sabini. Kuna ndugu yangu mmoja alikuwa ofisa wa TISS wakati wa Nyerere, na alikuwa anaishi maisha kama yuko mbinguni. Kama uliwahi kumfahamu jamaa anaitwa Walingozi, basi huyo ndiye aliyekuwa chuma cha pua wa TISS.

Mwanozni mwa miaka ya themanini ilikuwa ni almanusra tu na mimi ningeinga TISS ila nadhani hawakupenda maisha yangu ya ujana wakati huo kutokana purukushani zangu nyingi sana za wakati huo. Ila Takuru walinifanya kuwa ripota wao kwa kipindi fulani ingawa bila malipo yoyote bali malupululupu tu- ambayo yalikuwa yananitosheleza haja zangu wakati huo.
 
CP Msuya amekuwa The worst DG to be, With all resources ila still Ameruhusu Amiri jeshi Mkuu kuondoka mikononi mwake, Ila pia interesting ni kuwa Vijana wa Zamani walikuwa so ambitious imagine Mahiga amekaimu Ukuu wa idara nyeti kabisa at 35 Age, Njoo kwa Kitine nae at 36, Ila kwa sasa kijana wa miaka 35 kumuamini ni Ngumu sana mana Mzee alijaribu kuwaamini watu kama Makonda,Sabaya na Hapi ila matokeo yake wote tumeyashuhudia
Hassy kitine akili kubwa kijana wa TUNTEMEKE . Sema Deo ndo Boya kaharibu jina lao
 
Unasahau TISS ni Taasisi ya kiraia (Civilian) Wanajeshi wachache ni broad minded ndio maana Pamoja na Jeshi kuwa na Community yao Millitary Intelligence(MI) Lakini hii ya kiraia inabaki kuwa the best kuanzia kwenye mambo ya Gathering mpaka analysis, The best analysts ni wenye mtazamo wa Kiraia, Ni siasa tu zilivuruga idara yetu ila bado iko Juu
Roadmap
Msome na huyu jamaa kt the irreplaceable hapa kwenye post yake hii #69
 
Unasahau TISS ni Taasisi ya kiraia (Civilian) Wanajeshi wachache ni broad minded ndio maana Pamoja na Jeshi kuwa na Community yao Millitary Intelligence(MI) Lakini hii ya kiraia inabaki kuwa the best kuanzia kwenye mambo ya Gathering mpaka analysis, The best analysts ni wenye mtazamo wa Kiraia, Ni siasa tu zilivuruga idara yetu ila bado iko Juu
Mnataka kusema jeshini ( JWTZ ) wengi hawana kili ausio ? 😒😒
 
TISS Ilikuwepo muda mrefu sana inawezekana kulikuwa hakuna sheria, lakini mimi nimeelewa uwapo wa TISS tangu miaka hiyo ya sabini. Kuna ndugu yangu mmoja alikuwa ofisa wa TISS wakati wa Nyerere, na alikuwa anaishi maisha kama yuko mbinguni. Kama uliwahi kumfahamu jamaa anaitwa Walingozi, basi huyo ndiye aliyekuwa chuma cha pua wa TISS.

Mwanozni mwa miaka ya themanini ilikuwa ni almanusra tu na mimi ningeinga TISS ila nadhani hawakupenda maisha yangu ya ujana wakati huo kutokana purukushani zangu nyingi sana za wakati huo. Ila Takuru walinifanya kuwa ripota wao kwa kipindi fulani ingawa bila malipo yoyote bali malupululupu tu- ambayo yalikuwa yananitosheleza haja zangu wakati huo.
Huyu Walingozi wamemjadili sana hunu
 
Rais hataki kuvaa barakoa in the middle of a pandemic wakati ana matatizo ya moyo na mpaka wasaidizi wake wa karibu wanafariki kwa Covid-19.

Anawashushua wanaovaa barakoa, mpaka kanisani, hataki chanjo, hataki watu wapimwe. Hataki isolation.

Kapigwa daflao unamlaumu Msuya?

Hapa ni case ya "Mwana kulitafuta, mwana kulipata" tu.

Msuya anaweza kuwa na matatizo mengi, lakini kifo cha rais Magufuli alijitakia Magufuli mwenyewe kwa uzembe wake na ubishi wake wa kukataa sayansi, licha ya kuwa na Ph.D ya Chemistry, na kuendekeza propaganda za siasa.

Kwa kweli ukiangalia matatizo yake ya moyo, Magufuli hakutakiwa hata kugombea kazi yenye mikiki kama urais, kagombea urais kwa sababu ya uroho wake wa madaraka tu.

Sasa mtu kama huyo ambaye hashauriki wala hapangiwi, akifa, utamlaumu vipi Msuya?
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom