Orodha ya Wakurugenzi Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) tangu Uhuru

Orodha ya Wakurugenzi Wakuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) tangu Uhuru

ORODHA YA WAKURUGENZI WAKUU WA 'TISS' TANGU UHURU.

Idara ya usalama wa Taifa (TISS) imeundwa kwa sheria ya bunge namba 15 ya mwaka 1996 (Tanzania Intelligence and Security Service act No. 15 of 1996) iliyosainiwa na Rais Benjamin Mkapa tarehe 20 mwezi Januari mwaka 1997. Sheria hiyo ndio inayoipa mamlaka Idara hiyo kufanya kazi zake ndani na nje ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Pamoja na idara hii kusajiliwa kisheria mwaka 1996, lakini ilkuwepo tangu wakati wa utawala wa kikoloni chini ya ofisi ya Gavana wa Tanganyika. Baada ya Uhuru mwaka 1961 ilihamishiwa ofisi ya Rais.

Tangu idara hii kuanzishwa hadi sasa imeongozwa na Wakurugenzi 9 akiwemo Diwani Athumani Msuya aliyepo kwa sasa

Wa kwanza ni mzee Emilio Mzena, huyu aliongoza mwaka 1961 hadi mwaka 1975. Ndiye Mkurugenzi wa TISS aliyeongoza idara hii kwa miaka mingi zaidi kuliko wengine (miaka 14). Aliaminiwa na Mwalimu Nyerere baada ya idara yake kuzima majaribio kadhaa ya kumpindua.

Wa pili ni Dr. Lawrence Gama (PhD). Huyu alipokea kijiti kutoka kwa Mzena. Aliongoza kwa miaka mitatu tangu mwaka 1975 hadi mwaka 1978, kabla ya Mwalimu Nyerere kumuondoa katika nafasi hiyo na kumteua kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma.

Wa tatu ni Dr. Hassy Kitine (PhD) ambaye aliongoza idara hii kwa miaka miwili toka mwaka 1978 hadi 1980. Kitine alichaguliwa kuongoza idara hiyo nyeti akiwa kijana wa miaka 36 tu. Anakumbukwa kwa jinsi alivyoiwezesha TISS kushirikiana na Idara ya Usalama na Utambuzi Jeshini (MI) Chini ya Meja Jenerali Tumainieli Kiwelu, kuiteka nyara ndege ya makomandoo kutoka Libya iliyokuja kumsaidia Idd Amin katika vita ya Kagera.

Mwaka 1980 Mwalimu Nyerere alimteua kijana mwingine mwenye miaka 35 Dr. Agustine Mahiga (PhD) - (Marehemu) ambaye alikuja kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na baadaye Waziri wa Sheria chini ya Hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli - kuwa Kaimu Mkurugenzi mkuu wa TISS. Alikaimu nafasi hiyo hadi mwaka 1983, Nyerere alipomuondoa na kumteua Kaimu Balozi wa Tanzania (Minister Plenipotentiary) nchini Canada.

Baada ya Mahiga kwenda Canada, Mwalimu Nyerere alimteua Luteni Jenerali Imrani Kombe kuwa Mkurugenzi mkuu wa 5 wa TISS mwaka 1983. Nyerere alipong'atuka alimuacha Kombe kwenye idara hiyo na alidumu hadi mwaka 1995.

June 30 mwaka 1996 Jenerali Kombe aliuawa na Jeshi la polisi kwa madai kuwa walifananisha gari lake (Nissan Patrol) na gari iliyokua imeibiwa na mtuhumiwa Ernest Mushi maarufu kama "White".

Alimininiwa risasi 4 kifuani licha ya kushuka kwenye gari na kunyoosha mikono juu kama ishara ya kusurrender. Askari waliohusika na mauaji hayo walihukumiwa kunyongwa lakini Rais Kikwete aliwapunguzia adhabu mwaka 2011. Bado kifo cha Jenerali Kombe kina maswali mengi kuliko majibu.

Baada ya Kombe kuuawa alifuata Kanali Apson Mwang'onda. Huyu aliteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa 6 wa TISS ambaye aliongoza Idara hiyo hadi mwaka 2005 alipostaafu. Cornel Mwang'onda anasifiwa kwa kuifanyia marekebisho makubwa idara ya TISS ya kimfumo na kiutendaji. Ndiye aliyewezesha muswada uliounda sheria ya TISS mwaka 1996.

Mwaka 1980 Mwalimu Nyerere alifanyiwa jaribio kubwa la kutaka kupinduliwa na baadhi askari wa JWTZ (akina Tamin, McGhee na Kepteni Maganga) . Hili lilikua jaribio la 3 kubwa la kumpindua Nyerere, lakini ni jaribio la 7 katika orodha ukijumlisha na mengine madogo. Cornel Apson Mwang'onda akiwa Mkurugenzi wa ndani wa TISS (DOI) alifanikiwa kuzima jaribio hilo. Historia hii ilimuongezea sifa ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi mkuu wa TISS mwaka 1995.

Mwaka 2005 Rais Jakaya Kikwete alimteua Othman Rashid kuongoza Idara hiyo hadi mwaka 2016 alipostaafu. Othmna Rashid alikuwa Mkurugenzi wa 7 wa idara hiyo.

August 24 mwaka 2016 Rais John Magufuli alimteua Mchungaji Dr. Modestus Kipilimba (PhD) wa Kanisa la City Harvest Church la jijini Dar es Salaam kuwa Mkurugenzi Mkuu wa 8 wa TISS. Kabla ya uteuzi huo Kipilimba alikua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya taifa (NIDA).

Mchungaji Dr. Kipilimba amedumu katika nafasi hiyo hadi September 12 mwaka 2019 alipotenguliwa uteuzi wake na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna wa Polisi CP Diwani Athumani Msuya.
Hivi mada kama hii inamsaidia nini mtu hasa,isn't this not feeding your mind with junk? This is distraction from real issues to be frank.People need to be careful.Na nime notice kwamba the great majority of posts za JF ni za hivyo.I think the covert secret CIA army is at work.

Shetani anajaribu kutumia kila mbinu ili kupofusha na ku- distract.
 
Acha conspiracy....Watu wa off load shida yako nini?
 
Acha conspiracy....Watu wa off load shida yako nini?
Una umwa wewe,nina shida gani.The covert army of the CIA is 24/7 in the JF,mbona tunajua.Na hata wewe inawezekana ni mmoja wao.Mbowe na Lissu si ndio comanders kwa Tanzania.Sijui Lema naye yuko Canada kwa assignment gani Kwa kuwa naye ni commander wa CIA in Tanzania.
 
Una umwa wewe,nina shida gani.The covert army of the CIA is 24/7 in the JF,mbona tunajua.Na hata wewe inawezekana ni mmoja wao.Mbowe na Lissu si ndio comanders kwa Tanzania.Sijui Lema yuko Canada kwa assignment gani.
Kumbe hongera kwakutuogopa...Tanzania ni nchi na inayojitegemea, just be confident, do your part and leave the rest to God
 
Kumbe hongera kwakutuogopa...Tanzania ni nchi na inayojitegemea, just be confident, do your part and leave the rest to God
No hatukubali vibaraka nchini mwetu,we will do all it takes to contain you/them.
 
Nashukuru kwa Clarification Mkuu BTW sidhani kama Dini ni concern kubwa kiivo kwa Mtu aliefikia Kuwa Spymaster they just use it as a Play Ground
Ni bahati na uwezo tu mkuu, wale wakurugenzi kule juu yeyote ana equal chance ya kuwa DG sema since awamu wa ya kikwete uchaguzi wa DG umekuwa wa kupewa tu...
 
Ni bahati na uwezo tu mkuu, wale wakurugenzi yeyote ana equal chance ya kuwa DG sema since awamu wa ya kikwete uchaguzi wa DG umekuwa wa kupewa tu...
JPM alikuwa Mtu wa ku outsource sana hawa top officials amefanya ivo katika Taasisi nyingi tu, at some point nilikuelewa mana laws za kawaida tu husema mabadiliko hutoka nje, japo pia hali hiyo inaondoa morali kwa Top senior officers ambao wanatarajia kupata hio position mfano Magereza alimchukua Major General mzee Na kumpa CGP ila pia njoo taasisi kama Takukuru nako aliwekwa Brigadier General mbungo na uko Tiss pia ameibuka diwani japo nadhani Alishakuwa Mwandamizi kule
 
Hata kama alishakuwa Afisa Mwandamizi kumbuka hajakulia ndani ya Idara, changamoto za idara na kukiendesha chombo kwake itakuwa ni changamoto tofouti na wale Maafisa waandamizi ambao wamo ndani ya Idara. Kuna maamuzi anaweza fanya kumbe anakosea pakubwa sana hivyo ni vyema hawa ma DG watoke ndani ya mfumo kuliko kuwatoa nje ya mfumo kuna watu wanavunjika mioyo kwelikweli.
 
Hivi watu sijui nani aliwaambia Mwang'onda alikua Kanali(Cheo cha jeshi)....yaan niliposoma hivyo tu nikajua huyu muandishi hata hajui anaowaandika

Cornel ni jina lake la kuzaliwa na Sio Colonel/Kanali
Kwani amekosea pote au hapo tu??.
 
Hivi mada kama hii inamsaidia nini mtu hasa,isn't this not feeding your mind with junk? This is distraction from real issues to be frank.People need to be careful.Na nime notice kwamba the great majority of posts za JF ni za hivyo.I think the covert secret CIA army is at work.

Shetani anajaribu kutumia kila mbinu ili kupofusha na ku- distract.
Kati ya watu wanaoandika junks hapa JF wewe ndio wa kwanza. Unaandika mada za kufikirika ambazo ziko Hollywood kwenye movie, hapa watu wanataja historia wewe hutaki ila ukitoka utaenda kuanzisha mada kama SIRI YA COVID-19, UKIMWI NI UZUSHI, FREEMASON. Yani uko YouTube channels uchwara za kibongo
 
Back
Top Bottom