Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya

Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya

chichimizi

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2015
Posts
1,074
Reaction score
339
TANGAZO
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (OWM - TAMISEMI)
AJIRA MPYA YA MAFUNDI SANIFU WA MAABARA NA WALIMU KWA SHULE
ZA MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2014/15


A: Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya

Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za Mitaa kama ifuatavyo:-

i. walimu wa cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 11,366;

ii. walimu wa stashahada 4,151 na shahada 12,490 kwa ajili ya shule za sekondari

iii. mafundi sanifu maabara 264 kwa ajili kusimamia maabara na kuandaa masomo ya sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari

B: Utaratibu Ajira Mpya kwa Walimu na Mafundi Sanifu Maabara

Kila mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-

i. walimu wenye sifa waliohitimu mafunzo kwa mwaka wa masomo 2013/14 wamepangwa pamoja na walimu wa sekondari wa masomo ya sayansi na hisabati waliohitimu miaka ya nyuma na wameomba kuajiriwa;

ii. kuripoti kuanzia tarehe 01 Mei hadi 09 Mei 2015 kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangwa vituo vya kazi;

iii. kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma ya kuhitimu mafunzo, elimu ya sekondari, cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake;

iv. hakutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi; na

v. fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba (7) na nauli ya usafiri wa magari (ground travel) zitatolewa kwenye halmashauri husika baada ya kuripoti.

Imetolewa na
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA.


============
UPDATED LIST:
============

http://www.pmoralg.go.tz/noticeboar...aa_Biashara_2015_OWM-TAMISEMI_30April2015.pdf
 
Mi kinachoniudhi hadi presha zikanipanda ni pale ninapofungua website ya TAMISEMI kuona kama tayari alafu nakuta kile kitangazo chao kinachodai wanatoa majina tar 25 wakati naona tayari tar 26 na hawajakifuta kitangazo kile. Napata machungu wangekuwa JF wakapitia threads km hz wangefuta tu kitangazo chao.
 
Ni mtu mmoja wa tamisemi ndio ameniambia hayo,kuripoti bado ni mwezi wa5, lakini itakuwa ni tarehe za kati ili mshahara wa kwanza mupate wa mwezi wa 6 na sio wa mwezi wa 5.

Hii yote ni kwa sababu almashauri nyingi kwa sasa hazina pesa za kuwalipa walimu kama vile nauli na pesa za kujikimu,hawataki migomo na kelele kama zinavyotokeaga miaka yote pindi walimu wanapokosa stahiki zao pindi tu baada ya kujaza mikataba ya ajira na kupangiwa vituo,

Kumbukeni pesa za kujikimu,nauli na pesa za mizigo hutolewa na almashauri kutokana na vyanzo vyake vya mapato na zingine kutoka hazina,hivyo kama akaunti za almashauri za wilaya hakuna fedha za kutosha basi ajira zikitangazwa bado itakuwa ni tatizo!

Ajira zipo aidha mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa may,lakini pia wanavuta subira angalau muingie kwenye payrol ya june na sio ya may pindi mtakapo ripoti tarehe za kati za may.
 
BRAND uzi unamalengo mazuri lakini rekebisha neno ''halmashauri'' na si ''almashauri''
 
ajira akuna alikua anakufariji tu kama kuripoti mwezi wa tano ata wakitoa leo ukaripoti baada ya wiki2 itakuaje?jifariji
 
Halmashauri hazilipi pesa ya kujikimu wala nauli' pesa hizo hutolewa na TAMISEMI' aliyekupa taarifa kakupotosha..
 
Je, wakati wanatangaza kwa umma kuwa ajira zitatoka tar 25. Pia wakaongeza eti wamefanya utafiti ngazi ya halmashauri na shule kubaini uhaba wa walimu. Je, hawakugundua kuwa halmashauri hazina hela ili wasitangaze? Huyo ndugu yako wa tamisemi kakudanganya mtoa uzi
 
Je, wakati wanatangaza kwa umma kuwa ajira zitatoka tar 25. Pia wakaongeza eti wamefanya utafiti ngazi ya halmashauri na shule kubaini uhaba wa walimu. Je, hawakugundua kuwa halmashauri hazina hela ili wasitangaze? Huyo ndugu yako wa tamisemi kakudanganya mtoa uzi

Hutaki unaacha sio lazima kuamini,unaweza kuamini unavyojisikia wewe binafsi..!!
 
Kila mtu ana mtu wake tamisemi hao watu wenu au niwattunza bustan? au walinzi... mana mwaka jana mzgo kabla haujatolewa watu walikua tayar wamepata sasa mwaka huu majanga tu.
 
now days kila mtu ana ndugu au rafiki tamisemi balaaaaaaaaaa
 
ajira akuna alikua anakufariji tu kama kuripoti mwezi wa tano ata wakitoa leo ukaripoti baada ya wiki2 itakuaje?jifariji

Waswahili watu wa ajabu sana, ni rahisi kuvunja moyo na kukatisha tamaa kuliko kutia moyo
 
Back
Top Bottom