Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya

Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya

mbona kuna attachments wadau wametupia humu, na hayo majina wew unayotaka mtu atakupaje? labda kama kuna majina uangaliziwe tu mkuu MKOMBOZI1
 
wana JF anayepajua Dodoma-Kongwe DC-shule ninayoenda ni Mang'hweta sec anajuze mazingira ya huko kama koroboi ni nunue

Duuu! Hlo jina la shule sasa, ni kiashilio tosha kwamba ni interior sna!
 
Wadau nani anapafahamu iramba- singida tupeane picha

Umepangiwa shule gani Iramba ni wilaya ya Singida ni kubwa sana kuliko hata mkoa wenyewe inategemea utapangwa shule gani ila kuna baadhi ya shule ukipangwa zipo kijijini ila zipo bararan kabisa na zina umeme fight upangiwe Kinambeu sec, kizaga sec, kinampanda hizo ni shule nzuri kwa Iramba hasa kinambeu ipo njian kabisa kwenda wilayan kuna umeme wa grid ya taifa pia ni rahis kwenda kupata matibu ktk hospital ya kntc ila Singida kuna ukame maji hayatoki kila siku
 
TANGAZO
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (OWM - TAMISEMI)
AJIRA MPYA YA MAFUNDI SANIFU WA MAABARA NA WALIMU KWA SHULE
ZA MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2014/15


A: Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya

Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za Mitaa kama ifuatavyo:-

i. walimu wa cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 11,366;

ii. walimu wa stashahada 4,151 na shahada 12,490 kwa ajili ya shule za sekondari

iii. mafundi sanifu maabara 264 kwa ajili kusimamia maabara na kuandaa masomo ya sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari

B: Utaratibu Ajira Mpya kwa Walimu na Mafundi Sanifu Maabara

Kila mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-

i. walimu wenye sifa waliohitimu mafunzo kwa mwaka wa masomo 2013/14 wamepangwa pamoja na walimu wa sekondari wa masomo ya sayansi na hisabati waliohitimu miaka ya nyuma na wameomba kuajiriwa;

ii. kuripoti kuanzia tarehe 01 Mei hadi 09 Mei 2015 kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangwa vituo vya kazi;

iii. kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma ya kuhitimu mafunzo, elimu ya sekondari, cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake;

iv. hakutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi; na

v. fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba (7) na nauli ya usafiri wa magari (ground travel) zitatolewa kwenye halmashauri husika baada ya kuripoti.

Imetolewa na
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA.
Chuo cha TEKU pia ngazi ya cheti hajaajiliwa mwl hata mmoja.
Diploma na Digrii wameajiliwa wote.
Hongeleni zenu kwa kuajiliwa.
 
chondechonde walimu fikeni vituoni mwenu. Siku hizi huduma za kijamii kama maji na umeme zinafika maeneo mengi sana nchi hii. Pia usafiri sio shida sana kama zamani. Msipende kujazaja dar kufundisha tuition.
 
napenda kuulizia hizo nafasi za mafundi sanifu zipo pamoja na hao walimu wa sekondari au wao wamewekwa kwenye kundi lao.
 
napenda kuulizia hizo nafasi za mafundi sanifu zipo pamoja na hao walimu wa sekondari au wao wamewekwa kwenye kundi lao.

Zilikuwa zimechanganywa. Labda tusubiri hii update mpya watakayoitoa tuone watapangaje
 
Haiwezekani watu tumejaza form chuoni kuomba maeneo tunayoweza kupangiwa halafu ninyi mfanye tofauti kabisa na makadirio. kwa mfano mtu umetumia anuani ya dar, umeomba dar, moshi then unajikuta umepangiwa rukwa, hivi mashariki na magharibi wapi na wapi. mbona mikoa jirani na hiyo iko mingi. au zile form hazikua na maana? chakushangaza zaidi mtu mwingine ameomba upande huo huo wa rukwa una mleta mashariki tena kwa masomo hayo hayo. Hivi haya si ni makusudi kabisa. Na hii inasababisha matumizi ya kiasi kikubwa cha pesa za nauli zinazolipwa na serikali pamoja na kero za baadae za watu kubadilishana vituo kiholela bila kujali uhitaji wa wasomo husika. Naomba tatizo hili lijumuishwe kwenye marekebisho yanayoendelea ya walimu ngazi ya shahada na stashahada.
 
kabla ya ajira mlisema mpotayari kufanya kazi eneo lolote, leo ajira zimetoka mmeanza figisufigisu. Kuwaongoza wabongo lazima uwe na akili fyatu kidogo!
 
Kubali yote mkuu juzi mlikua mnalilia ajira zimetoka mnalalamika ukishachagua ualimu kubali yote haina jinsi.
 
Back
Top Bottom