Hao wote wangejua kuwa watakufa Jana, wasingesafiri, aise tujiandae maana duniani hapa tunapita, hapo tiyari hukumu imefanyika wa kwenda motoni na ambao wameenda mbinguni tiyari walishakuwa wenyeji huko!!
Waebrania 9:27
Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;
Marko 8:36
Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?
Marko 9:43
Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika; [
Marko 9:44
ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]
Marko 9:45
Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; [
Marko 9:46
ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]
Marko 9:47
Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;
Marko 9:48
ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.
Ufunuo wa Yohana 14:11
Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.
Nashauri wakuu tujiandae , tusibweteke na dunia, hii dunia inatudanganya Sana, lakini ukweli ni kwamba duniani sisi ni wapitaji!!