Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

Nimegundua kijana kinacho kuchanganya industry revolution ya mziki hasa wa hiphop hapa bongo, mziki wa hiphop unakua na kubadirika kila siku na watu kugundua namna mpya za kuufanya mziki huo kila siku, na hiyo ni kutokana na exposure kubwa ya muziki iliopo duniani kwa sasa. Tuliopata kuwaskia hao jamaa miaka ya late 90s and miaka ya 20s, hakika masikio na bongo zetu havijutii, tulienjoy sana. Yn umemuweka mpaka mtu kama jaffarai, mike t mnyaru, soggy, una utani sana
 
hapa ndiyo natambua hujui mziki hasa wa zamani
Soggy mda mwingi sana alikua upande wa production, hasa kusuka drums
kuimba ni mara moja moja, 98% kusuka drums, 2% ndiyo kuimba
Soggy ameimba sana akiwa Solo na pia akiwa na wanawe, Caz T na Suma G ( Bantu Pound & Hotpot Family).

Hebu sikilizeni hii remix ikiwa na wasanii wengi wakati wa harakati za kuikubalisha bongo fleva kwenye jamii. Dogo Hamidu ndio Nyandu Tozzy
 
Master jay mangi yule akatae hela , Sugu mwenyewe ngoma nyingi karecord mj
 
hapana, yuko vizuri sana, alizalisha hit song kali ya Afande Sele, Darubini Kali, iliyopeleka kushinda ufalme wa Rhymes 2004
Sasa si mzuri kwenye production? Me nazungumzia kwenye rap
 
Huyu jamaa ni Choko anajifanya kujua hivi hata Soggy Dog Hunter mwenyewe hata anamjua Kibanda Cha simu inatoka yeye yupo tumbon kwa mama yake mjinga mmoja
We fala una mihemko sana
 
Fatilia historia zao, mfano Mchizi mox ye mwenyewe alishawai kunukuliwa kuwa anabaniwa na majani ....lakini ukweli ni kuwa hana kipaji ana force tuu
Mchizi Mox anasema kuwa Majani hakupenda vile jamaa anavyoimba kwa kukoroma, akamshauri abadili na kuimba kwa sauti ya kawaida, Mchizi Mox akakataa. Majani akafanikiwa kumbadilisha Jay Moe, huyu ndio akaanza kuimba hivi tulimvyomsikia katika nyimbo zake, ila nae awali alikuwa akitoa sauti ya kukoroma kama Mox.

Hata hivyo Majani hakuwahi kusema kuwa Mox hana kipaji, ila aliona kibiashara atazingua. Mtazamo aliokuwa nao Majani hata mimi nilikuwa nao wakati naanza kumsikia Jose Chameleon na ngoma yake Mama Mia. Niliona ni msanii mwenye sauti mbovu na hawezi kutoboa kumbe sikuwa sawa. Ilikuwa ni mtazamo wangu tu na sio kuwa jamaa hakua na kipaji, sasa the same goes kwa Mox et al
 
Kaka nnavosema hawa nliowataja kuwa hawana vipaji ....nimezingatia Uandishi wao , flow zao n.k

Uandishi 0%
Flow 0%

Wasanii wengi hapo hata kurecord tuu producers walipata shida sana

Mfano ngoma Mh temba ft Dully sykes - Nampenda yeye
Ilikaa studio karibu mwaka coz kila majani akiiskiliza anaona bado haijitoshelezi na jamaa alirudia rudia sana kuingiza voco kutokana na uwezo wake mdogo

Hawa jamaa nkikuambia hawana uwezo ujue nimefanya utafiti sijakurupuka mkuu
 
Lazima uone hvyo kutokana na udogo wa upeo wako
 
Soggy ameimba sana akiwa Solo na pia akiwa na wanawe, Caz T na Suma G ( Bantu Pound & Hotpot Family).

Hebu sikilizeni hii remix ikiwa na wasanii wengi wakati wa harakati za kuikubalisha bongo fleva kwenye jamii. Dogo Hamidu ndio Nyandu Tozzy
Hawa jamaa tutaendelea kuwapa heshima kama legends lakini hawakua na vipaji trust me

Hata p the mc kuna ngoma yake moja anasema..

"Waasisi wa muziki bongo hawaja ni inspire/
Complex ndo kanipa ubaya /

Hapa akiwa anamaanisha wasanii wengi kama kina sugu, soggy dog mbali na ukweli kuwa walianza hizi harakati za muziki zamani lakini uhalisia wa mambo ni kuwa hawana talent..so tunawapa heshima kama brothers tuu
 
Mike T hakuwa akiandikiwa mistari, nafikiri umeona wengi wanakushangaa kumsema kuwa hana kipaji. Ni msanii aliyetokea mkoani lakini alimshangaza mpaka P Funk kwa uwezo wake kimuziki. Ni msanii aliyetoa nyimbo 4 (single) bila kutoa album na alipotoa album hizo nyimbo hazikuwepo (alikua anajiamini kuwa hategemei zile single ndio zimbebe).

Lakini pia kuandikiwa hakumfanyi msanii asiwe na kipaji, mbele (US) mastar wengi tu si walikuwa wanaandikiwa toka enzi hizo, uandishi wa nyimbo ni kipaji kama kilivyo kipaji cha uimbaji wa nyimbo.

Sister P ameandikiwa ngoma zilizomtoa ila kila mtu anajua kuwa Sista P alikuwa msanii mkali.

Anyways, kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni. Yaheshimiwe
 
Kama umefanya uchunguzi, utagundua kuwa Prof. J ana collabo chache sana alizoshirikishwa, na ni kama alikuwa selective sana katika watu wa kufanya nao kazi, yaani ni kama alikuwa anakubali kushirikishwa na msanii ambaye yeye (Profesa J) anamuona kuwa ni ana kipaji. Sasa hapo kashirikishwa na Soggy. (Prof. aliona kuwa Soggy ni msanii mwenye kipaji)

Kutoka mwaka 2000 baada ya Chemsha Bongo, Prof alikuja fanya collabo kwa kushirikishwa na Banana Zoro (bado nakuhitaji) akafanya na Bodea (Hard Core). Ingawa yeye kwenye album ya Machozi, Jasho na Damu aliwashirikisha wasanii wengi tu mpaka wachanga.
 
Hivyo vitu unavyomwambia havijui
 
Hoja Ni kitokuwa na kipaji kiwa na mazingira magumi sio excuse ya kuwa ndio una kipaji pia zamani nyimbo nyingi zilikuwa zakindezi Basi tu zamani watu wali accept ujinga mziki sasahivi unachuja quality
Bora zamani wasiokuwa na kipaji Cha kueleweka wachache Sana walipenya..
Lakini kwasasa wasiokuwa na vipaji wanapenya kiwepesi Sana Kama wameshikwa mkono na watu wenye nguvu..yaani shilole anatoa hit song na yumo kwenye tuzo za nchi..zamani isingewezekana..
 
Jina la kisanii mwanzoni kabisa alikuwa anajiita "2 proud", likafata " Mr. II", likafata "Sugu" na sasa "Taita".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…