Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

Nampa heshima kama muhasisi wa bongo fleva lakini hio haiondoi ukweli kuwa sugu hana kipaji cha muziki
Get your fact right. Sugu sio muasisi wa bongo fleva ila aliweza kuibeba bongo fleva mabegani kwake miaka hiyo na kiufupi kipaji anacho.
 
Naomba uziweke Hapa Bang zote Kama utaweza kiongozi..Mimi naikumbuka Bang ya N2N soldiers..
 
Watoto wadogo ndio hawawezi kumuelewa Sugu.
Sugu is the most successful Rap star in Tanzania. He is the G.O.AT
Watoto waliozaliwa miaka ya juzi pia kule US hawamuelewi Ice Cube, Nas na malegend wengine wa zamani.
 
Hawezi kuthubutu kusema hivo, Nature ni hazina ya taifa Top 10 ya wasanii kuwahi kutokea Nchii hii humkosi Nature yan apo unawaweka na kina Mbaraka Mwishee et al
Kuna dogo aliwahi kuja kumshindanisha humu Juma nature na G Nako eti nani mkali kwenye chorus?. Yani mtu hadi unajiuliza what the fu.ck is this?.
 
Wote wa zamani. Yaani zamani ulikua ukiingia studio tu umetoka.

Mfano kuna mwamba aliimba:

"Ni namna gani, tuta win, maishani hadi siku tutasema buriani.."

Aliimba utumbo haujawahi tokea ila alitoka kwa zama zile.
Wanaoimba utumbo alafu ukwa hit wapo wengi hata marekani wapo..
Sikiliza wimbo wa Nini mnataka mazee wa pig black anarap mambo yasiyoeleweka lakini wimbo Bora Sana kwa wakati huo..
 
Kuna dogo aliwahi kuja kumshindanisha humu Juma nature na G Nako eti nani mkali kwenye chorus?. Yani mtu hadi unajiuliza what the fu.ck is this?.
Anytime ntaenda na Nature......
Ila huo mlinganisho ulikuwa halali, Nako pia anachorous kali.
Kwa miaka ya 2010s yeye ndio mfalme.
 
Wewe Bora ume-admit kua ni shabiki Ila kwako unamuona wa kawaida, sasa ulitaka afanye nini umuone wa maana aimbe km YoungLunya au Dayoo ?
Boara young Lunya.. lakini huyu dayoo sijui platform..Ni upuuzi mtupu
 
Dogo umenitoa machozi kusema Sugu na Mike tee hana kipaji yan like serious mdogo wangu unakuja kutusi ma Legend humu.

Any way pengine nakusamehe kutokana na umri wako.

1.Sugu moto chini
2. Mambo ya Fedha
3.Jeuri
4. Hayakuwa mapenzi hii mgoma almost kila baada ya siku 3 naskiliza kuna mpenz wangu enzi hizo aliondoka tu na sikujua shida nini? Yani aliaga kama atarudi nikampa ma mazaga kibao ajabu hakurudi akasema ameolewa.

Ukija recently kama unavotaka ana ngoma inaitwa freedom na mtiti.

Vile anavoongea ndio u Mc wenyewe dogo unaliacha bit kama huna time nalo vile.

Dogo pumbavu sana wewe.
 
Akimsikiliza easy e wa west coast atakuambia hana kipaji
 
Wote wa zamani. Yaani zamani ulikua ukiingia studio tu umetoka.

Mfano kuna mwamba aliimba:

"Ni namna gani, tuta win, maishani hadi siku tutasema buriani.."

Aliimba utumbo haujawahi tokea ila alitoka kwa zama zile.
Huo wimbo ameimba Fred Saganda, jamaa ana kipaji kikubwa tu ni vile hukumuelewa.

Music ni sanaa, na mimi naamini aliimba huu wimbo kuiwakilisha sanaa yake ya kipekee.

Na kuanzia hapo utaona watu kibao walishtuka na wakaanza kuimba kwa kutumia lafudhi ya makabila yao.

It's funny.
 
Billnass Hana kipaji,
ila anaishi vzr na walioshika mziki.
 
Shida ni kwamba wengi unawajaji kwa nyakti za sasa,kitendo cha kutoa nyimbo kwa nyakati zao na kuhit ni kipaji tosha ila soko la sasa bdo limewakataa,hata marijab rajab au remmy ongala leo hii wangetoa nyimbo ungewajaji hawana vipaji,hawa unaowaona wana vipaji leo next 10 years utasema walikuwa hawana vipaji....,hao uliowataja wengi wana vipaji ila siyo mpaka vifanane kama marapa wenu wa sasa,nyimbo kama Mstari wa mbele,umoja ni nguvu ulitaka pina aimbe nn ili umpe heshima ww mtoto usiyejua mziki,heshim wazee!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…