Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

Baadhi ya mistari
"Cheza cheza kwenye dancing flow,
Wala usijali kuitwa bishoo,
Kata kata ngoma za kisasa,
Kibao ni chako sio cha kuazima

Maneno mengine nimeyasahau ilikua zamani sana
 
Bilnas anaimba mziki gan?
 
Nembo ya taifa bongo records ingetumika,
Watoto wadogo lazima mic wajue kushika,
Lakini yote hiyo ni kama
 
Hivi hiii Style ya Jabali la Kampala. Jose inaitwajeee
 
Nimeanza kumfatilia Sugu kabla hujazaliwa, na ushahidi nimekuwekea Sasa wewe leta ushahidi popote pale palipoandikwa TOO PROUD
Huyu jamaa ni tahira wala usibishane nae yeye kambatiza 2 proud kua too proud

.Halafu anasema sugu Hana kipaji [emoji52] huyu jamaa tungeishi mtaa mmoja ningemfanya kitu kibaya Sana bahati yake tu jf hatujuani
 
Kwenye list muongeze JCB wa watengwa na Joh Makini. Jcb bwana sijui kama alichokuwa anaimba ye mwenyewe anakijua au kama unaweza okota karatasi ya wimbo alioandika ukajua kama ni wimbo
 
Yaani Unasema Soggy hana Hit Song baada ya Kibanda cha Simu?? Nilikaona Mwaka jana na Stori umeziimba wewe mpaka zikawa Hit song?? Bila Kuisahau KURWA NA DOTO nayo ilikua Hit song.

Sugu mpe Heshima yake, Ni kweli wakati wa sasa si Kama Zamani ila Heshima yake na Mashairi yake kamwe usiyabeze na kuyafananisha na hawa watoto wa 2000. Sugu Ni Msanii wa Hip Hop aliyethubutu kuikosoa serikali kuanzia enzi hajawa mbunge wala Hana matarajio ya kuwa mbunge, Kiufupi ni msanii aliyeiwakilisha mitaa (jamii) na matatizo yake.

Ni Msanii mwenye Album nyingi zilizosheheni Jumbe mbalimbali na Burudani. Kama

Ni Mimi (1995)

Ndani ya Bongo (1996)

Niite Mister II (1998)

Nje ya Bongo (1999)

Millennium (2000)

Muziki na Maisha (2001)

Itikadi (2002)

Sugu (2004)

Coming of Age-Ujio Wa Umri (2006)

VETO (2009)

Antivirus Mixtapes

Moja Kati ya wimbo wake niliokua nikiuimba sana na Kuupenda ni Mikononi mwa Polisi (1999) aliouimba kwa ajili ya Kijana mwanafunzi Michael Sikupya aliyeuawa na Polisi jijini Mbeya shuleni Iyunga Sekondari.

Kimsingi Sugu ni Legend, G.O.A.T.



Kuna Wengine umewaonea tu hapo, wale ambao walitoa Wimbo mmoja ukawa hit na hatukupata kuwasikia tena kama

°Rich One na Hatuna Kitu
°Fidovato huyu kwenye hii list sijui umemuweka wa nini hakupaswa kuwapo hapa kwa maana hakuna alichofanya katika muziki wa hip hop.
°Kr Murah Jibaba mziki mnene cd 700 njoo kichwa kichwa ule za uso.... Huyu mwamba hana chochote Kama Solo zaidi ya kazi za Kundi ulipaswa usimuweke hapa pia.


Mike Tee pia unamuonea, Ameacha game kwa heahima kubwa. Alitoa ma dude yaliyokua mikito ya Taifa wakati ule kama

1. Kama ft Jay moe
2. Nampenda nani ft Juma Nature
3. Ni beep baby
4. Je Utanipenda ft Mad Ice
5. Sivainogela
6. Hodi
7. Niacheni ft Banana Zoro
8. Sintobadilika ft Q Chief
 
Kwenye list muongeze JCB wa watengwa na Joh Makini. Jcb bwana sijui kama alichokuwa anaimba ye mwenyewe anakijua au kama unaweza okota karatasi ya wimbo alioandika ukajua kama ni wimbo
JcB namuelewaga sana [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] kuna hizi ngoma zake nazipenda

Ukiskia Paah Orijino na Remix
Machochoro zote [emoji3][emoji3] ft Chaka
Bongo Fleva
Wanashangaa ft Jay Moe, Nakaaya (hii ngoma kali sana)

Halafu Kuna Zile Watengwa wote, Mashairi yake nayaelewa kwenye nyimbo kama

Africa
1 2 3 4
Rap si mchezo
Sio lazima
Tabia mbaya
Tunafanya
Tathmini ft Kikosi cha Mizinga
Narizika
Full iwe laana
 
We hujui mziki aisee.
Sugu huyu huyu anaeimba verses zote 3 na korasi peke yake hana kipaji?

Na hata live anachana tu bila kuchoka unasema hajui mziki? Dah
 
Your browser is not able to play this audio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…