Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

Saleh Jabir kutokana na uzi huu nadhani sio huyo unayemsema wewe,hapa amezungumziwa Saleh Jabir anayetambulika kama mwanzilishi wa kuimba wimbo wa kwanza au chache za mwanzoni za mtindo wa rap ambapo aliutohoa wimbo wa ice ice baby kwa kuchukua midundo (beat) naye kuweka maneno ya kiswahili,wakati huo huyo mtangazaji unayemsema alikuwa "mama nnya"
Baadhi ya mistari
"Cheza cheza kwenye dancing flow,
Wala usijali kuitwa bishoo,
Kata kata ngoma za kisasa,
Kibao ni chako sio cha kuazima

Maneno mengine nimeyasahau ilikua zamani sana
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Sasa hilo ni tatizo la waandaji tuzo

Lakini nakwambia ukweli hata SUGU angekua kwenye hiyo category bado ningeona ni upuuzi tuu kama ww unavyo shangaa Bilnass kuingia kwenye tuzo hizo wakati hafanyi HIPHOP
Bilnas anaimba mziki gan?
 
Kama ninge ..kama ningekuwa mimi star[emoji445]
Nahisi jina langu kila mtaa lingezagaa[emoji445]
Anzia ngazi Taifa, mpaka mkoa[emoji445]
Vibanda vya mamc katuni vyote ningebomoa[emoji445]


Jamaa alikuwa ananata na beats kali za majani pale bongo records


Huyu mwamba alikuwa na hits

Kama
Mnyalu
Nampenda ft nature

N.k

Huyu aliyetoa mada afungwe pingu apelekwe selo
Nembo ya taifa bongo records ingetumika,
Watoto wadogo lazima mic wajue kushika,
Lakini yote hiyo ni kama
 
Mchizi Mox anasema kuwa Majani hakupenda vile jamaa anavyoimba kwa kukoroma, akamshauri abadili na kuimba kwa sauti ya kawaida, Mchizi Mox akakataa. Majani akafanikiwa kumbadilisha Jay Moe, huyu ndio akaanza kuimba hivi tulimvyomsikia katika nyimbo zake, ila nae awali alikuwa akitoa sauti ya kukoroma kama Mox.

Hata hivyo Majani hakuwahi kusema kuwa Mox hana kipaji, ila aliona kibiashara atazingua. Mtazamo aliokuwa nao Majani hata mimi nilikuwa nao wakati naanza kumsikia Jose Chameleon na ngoma yake Mama Mia. Niliona ni msanii mwenye sauti mbovu na hawezi kutoboa kumbe sikuwa sawa. Ilikuwa ni mtazamo wangu tu na sio kuwa jamaa hakua na kipaji, sasa the same goes kwa Mox et al
Hivi hiii Style ya Jabali la Kampala. Jose inaitwajeee
 
Nimeanza kumfatilia Sugu kabla hujazaliwa, na ushahidi nimekuwekea Sasa wewe leta ushahidi popote pale palipoandikwa TOO PROUD
Huyu jamaa ni tahira wala usibishane nae yeye kambatiza 2 proud kua too proud

.Halafu anasema sugu Hana kipaji [emoji52] huyu jamaa tungeishi mtaa mmoja ningemfanya kitu kibaya Sana bahati yake tu jf hatujuani
 
Kwenye list muongeze JCB wa watengwa na Joh Makini. Jcb bwana sijui kama alichokuwa anaimba ye mwenyewe anakijua au kama unaweza okota karatasi ya wimbo alioandika ukajua kama ni wimbo
 
Yaani Unasema Soggy hana Hit Song baada ya Kibanda cha Simu?? Nilikaona Mwaka jana na Stori umeziimba wewe mpaka zikawa Hit song?? Bila Kuisahau KURWA NA DOTO nayo ilikua Hit song.

Sugu mpe Heshima yake, Ni kweli wakati wa sasa si Kama Zamani ila Heshima yake na Mashairi yake kamwe usiyabeze na kuyafananisha na hawa watoto wa 2000. Sugu Ni Msanii wa Hip Hop aliyethubutu kuikosoa serikali kuanzia enzi hajawa mbunge wala Hana matarajio ya kuwa mbunge, Kiufupi ni msanii aliyeiwakilisha mitaa (jamii) na matatizo yake.

Ni Msanii mwenye Album nyingi zilizosheheni Jumbe mbalimbali na Burudani. Kama

Ni Mimi (1995)

Ndani ya Bongo (1996)

Niite Mister II (1998)

Nje ya Bongo (1999)

Millennium (2000)

Muziki na Maisha (2001)

Itikadi (2002)

Sugu (2004)

Coming of Age-Ujio Wa Umri (2006)

VETO (2009)

Antivirus Mixtapes

Moja Kati ya wimbo wake niliokua nikiuimba sana na Kuupenda ni Mikononi mwa Polisi (1999) aliouimba kwa ajili ya Kijana mwanafunzi Michael Sikupya aliyeuawa na Polisi jijini Mbeya shuleni Iyunga Sekondari.

Kimsingi Sugu ni Legend, G.O.A.T.



Kuna Wengine umewaonea tu hapo, wale ambao walitoa Wimbo mmoja ukawa hit na hatukupata kuwasikia tena kama

°Rich One na Hatuna Kitu
°Fidovato huyu kwenye hii list sijui umemuweka wa nini hakupaswa kuwapo hapa kwa maana hakuna alichofanya katika muziki wa hip hop.
°Kr Murah Jibaba mziki mnene cd 700 njoo kichwa kichwa ule za uso.... Huyu mwamba hana chochote Kama Solo zaidi ya kazi za Kundi ulipaswa usimuweke hapa pia.


Mike Tee pia unamuonea, Ameacha game kwa heahima kubwa. Alitoa ma dude yaliyokua mikito ya Taifa wakati ule kama

1. Kama ft Jay moe
2. Nampenda nani ft Juma Nature
3. Ni beep baby
4. Je Utanipenda ft Mad Ice
5. Sivainogela
6. Hodi
7. Niacheni ft Banana Zoro
8. Sintobadilika ft Q Chief
 
Kwenye list muongeze JCB wa watengwa na Joh Makini. Jcb bwana sijui kama alichokuwa anaimba ye mwenyewe anakijua au kama unaweza okota karatasi ya wimbo alioandika ukajua kama ni wimbo
JcB namuelewaga sana [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] kuna hizi ngoma zake nazipenda

Ukiskia Paah Orijino na Remix
Machochoro zote [emoji3][emoji3] ft Chaka
Bongo Fleva
Wanashangaa ft Jay Moe, Nakaaya (hii ngoma kali sana)

Halafu Kuna Zile Watengwa wote, Mashairi yake nayaelewa kwenye nyimbo kama

Africa
1 2 3 4
Rap si mchezo
Sio lazima
Tabia mbaya
Tunafanya
Tathmini ft Kikosi cha Mizinga
Narizika
Full iwe laana
 
Kalapina,

Huyu jamaa mbali na kuwa na harakati nyingi akiwa pamoja na kundi lake la Kikosi cha mizinga .ukweli ni kwamba hana kipaji cha music. Alipata umaarufu coz ametoka kipindi wasanii ni wachache

Sugu

Huyu jamaa ana majina kibao kama Mr two, jongwe, too proud na sasa anajiita Taita licha ya kuwa na heshima kama moja ya waasisi wa music wa hiphop tanzania , ukweli ni kwamba hana kipaji cha music

Jaffarai

Huyu ni moja ya member wa wateule alitamba na wimbo wa niko bize .lakini hakuweza kudumu kwenye game kwa muda mrefu kutokana ukweli hana kipaji

Mchizi mox

Huyu pia ni member mwingine wa wateule ngoma zake zilizowahi kupata airtime ni mambo vp na chupa nyingine . lakini uwezo wake ni wa kawaida sana

Mike tee mnyalu

Huyu jamaa alipata airtime miaka ya zamani kwa ngoma zake lakini ukimskiliza ni wazi hana uwezo kabisa. Ni moja kati ya wasanii ambao huwa wanaandikiwa

Soggydog hunter

Huyu jamaa bora angebaki kwenye u presenter tuu huku kwenye music aliforce tuu hana uwezo kabisa ana ngoma nyingi ila iliyopenya ni kibanda cha simu pekee yake

Bou nako

Huyu alikua member wa N2N lakini tangu hakua na uwezo kabisa .nafkir wana walimbeba tuu kutokana na love .ila kwenye music jamaa hana kipaji

Fido vato

Huyu member wa vatokoko soldiers ni empy kabisa , analazimisha fan tuu ila ukweli anaujua kuwa hana uwezo wowote ule zaidi ya kujikuta gangstar

Kr mulah

Huyu ndio founder wa style ya kucheza Mapanga . ameanza sanaa muda mrefu sana lakini ukimskiliza utagundua jamaa hana uwezo wowote kwenye music kwa kifupi hana kipaji

Mh temba

Huyu ni member wa TMK wanaume family mwanzoni alibahatisha ngoma kama tatu zikaenda mjini, baadaye akaja kuungana na chege wakatoa hadi album..ila ukimfuatilia vizur jamaa hana
uwezo kabisa

Rich one

Huyu pia ni member wa TMK alitamba na ngoma moja aliyomshirikisha Juma nature inaitwa hatuna kitu.baada ya hapo hajawai kutoa hitsong tena, Jamaa anasifika kwa utapeli wa kuandaa show na wasanii fake huko mkoani afu anapiga hela

Dudu baya

Huyu jamaa aliotea ngoma kama tatu tuu ambazo zilimtambulisha vyema kwenye game .lakini alipata jina kwakua kipindi anatoka hapakua na upinzani mkali kama ilivyo sasa

Dark master

Huyu ndo muhasisi wa Chamber squard Nampa heshima kubwa sana kwa kuweza kuiweka dodoma kwenye ramani ya muziki , Lakini tukiongelea uwezo binafsi .jamaa anauwezo wa kawaida sana

John mjema,

The late John mjema alitamba na wimbo wa wachumba 30. Na ngoma zingine alizofanya kwenye kundi lao aliokua na kina the late steve 2k na buibui .lakini tukimzungumzia binafsi kimuziki jamaa hana kipaji cha muziki

Maujanja suppliers

Hawa jamaa nawakubali kwa harakati zao za street lakini kwenye music watupishe hawana vipaji .lakini wao wamekua wanalalamika wanabaniwa kitu ambacho sio ukweli

Kama unafuatilia music wa bongo fleva utakua unakubaliana na mimi hawa jamaa hawana talent za music kabisa
We hujui mziki aisee.
Sugu huyu huyu anaeimba verses zote 3 na korasi peke yake hana kipaji?

Na hata live anachana tu bila kuchoka unasema hajui mziki? Dah
 
JcB namuelewaga sana [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] kuna hizi ngoma zake nazipenda

Ukiskia Paah Orijino na Remix
Machochoro zote [emoji3][emoji3] ft Chaka
Bongo Fleva
Wanashangaa ft Jay Moe, Nakaaya (hii ngoma kali sana)

Halafu Kuna Zile Watengwa wote, Mashairi yake nayaelewa kwenye nyimbo kama

Africa
1 2 3 4
Rap si mchezo
Sio lazima
Tabia mbaya
Tunafanya
Tathmini ft Kikosi cha Mizinga
Narizika
Full iwe laana
 
Back
Top Bottom