PostGE2025 Orodha ya wazee waliokuwa wanaheshimika ila wamekuja kupoteza heshima yao mwishoni kabisa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Asha Rose. Daah nilivyokua namuona kwenye kampeni akisema samuya oyee. Naishiwa ganzi kabisa.
Duu... yaani kweli ulikuwa unadhani Asha Rose ni kiongozi mzuri mpaka siku aliposema Samia hoyee? Huyu mbona ni kiazi siku zote? Kama wana tofauti na Samia basi ni ndogo sana.... may elimu yake siyo ya kuunga-unga kama Samia.
 
Azim Dewji sio baba yake MO...

Hata hivyo Azim ni mbogamboga kimdakindaki miaka yake yote tokea akiwa kijana, wafanyabiashara wa 'kaliba' ndio wafadhili wakuu wa mbogamboga...
Hawa ndugu zetu wahindi wanachojali ni maslahi tu, hawaamini kwenye itikikadi ya chama chochote. Hata leo hii chama kingine kikichukuwa nchi huwezi kuwaona wakisalia CCM, tena ndiyo watakuwa wa kwanza kukimbia.
 
Mimi hadi leo kila ninapowaza hivi mzee Kikwete ametuchukuliaje sisi watanganyika? Yaani yawezekanaje aruhusu wala urojo waje kutubagaza huku yeye akishuhudia ?

Najiuliza hivi alishindwa kuingiza ushawishi hata tu zipatikane reforms zitakazohakikisha zinatengeneza njia ya kupata wawakilishi wakutoka vyama vyote ili kutengeneza mchanganyiko wa hoja bungeni?
Najiuliza hasara ya kuwa na wabunge wa kutoka vyama vya upinzani na faida zake ,huyu faza ameshindwa kabisa kuziona?

Haikutosha ,bado anashuhudia Wana wa Taifa letu wakigongwa vyuma mchana kweupe nae akichukulia poa tu , seriously?

Huyu dingi anaushua wakis3ng3 sana 👺👺
 
Mzee Samia Suluhu
Mzee Ombeni Sefue
Mzee Prof Ibrahim Juma
Mzee Jaji Othman
Mzee Said Mwema
 
Kwani wewe ulianza lini kuwajibu na wao hizo nyuzi zao walianza kipindi gani kuzileta humu? Maana wewe naona umejiunga toka 2015, nauliza hivyo kwa sababu mada za mabishano ya kidini zina muda mrefu hazinaga mwisho.
Hizo mada zipo wapi tena siku hizi na zisizo na mwisho ni zipi nitajie mada moja wapo inayo endelezwa na waislamu...hakuna muislamu anaye leta swali la dini siku hizi au nitajie jina la huyo muislamu unaye mjua wewe.
 
Ndio maana nimekuuliza ni kipindi gani hizo mada zimeanza kukoma kuwepo? Wewe umeanza lini kujibu hoja zao humu?

Mada za dini hazinaga mwisho zinapotea na kurudi tena, mimi najua ndio ziko hivyo na kuna wakati zinazidi sana.
 
Kikwete na Mbowe . Hawa watu wamekufa kwa ajiri yao . Wapo kwa ajiri ya biashara zao .
 
Natamani niweke Orodha ndefu lakini hebu tuishi na hii kwanza..

Kuna wazee ambao tulidhani wangekuwa "dawa" hapo mwanzo lakini ghafla heshima yao waliyojitengenezea imepukutika kama barafu kwenye jua kali

10. Mzee Butiku.. huyu tulidhani angekuwa msaada kabisa lakini kuna tetesi huyu ndio alimchoma Pole pole.. aibu sana

09. Mzee Alkael Mbowe ilifika hatua akaitwa "kamanda" lakini ona heshima yake ilivyoshuka usiku mmoja tu!

08. Mzee (Mchungaji) Hananja: huyu aliheshimika mpaka akawa anaitwa Sehemu mbali mbali kuhutubia lakini akaweka njaa mbele

07. Mzee (askofu) Malasusa huyu siwezi kumsemea sana ila mnaona wenyewe

06. Mzee Rioba (wa TBC) huyu ni mmoja wa wazee ambao anaona uchawa na unafiki pekee havitoshi.. ila heshima yake imeshuka

05. Mzee Wasira: huyu angekataa tu ile nafasi ya umakamu kuliko kuendelea kukomaa wakati tayari mwili unakataa

04. Mzee Mwambegele (mzee wa Tume) hivi ataficha wapi uso wake baada ya hii 98% ? Yaani hata akistaafu akienda kucheza na wajukuu lazima watamzomea tu

03. Mzee Azim Dewji (baba Mo) huyu mzee alisema Pole pole anatafuta kiki huyu mzee anajishushia sana heshima kulinda uraia na biashara zake... Yupo radhi alambe miguu ya viongozi wa CCM

02. Mzee Tido Mhando alijijengea heshima kubwa lakini toka apambane kumsafisha Rostam na sasa anapambana kuwasafisha 'wanamtandao" heshima yake imerudi hadi "sifuri"

01. Mzee wa Msoga: binafsi huyu alikuwa Raisi wangu pendwa.. ila kumbe i was wrong.

Sote tunajionea haya yote yanatokea ni kwasababu yake na hakika amestahili kuwa namba moja kwenye hii Listi ya wazee waliokuwa wanaheshimika ila wamekuja kujishushia heshima yao mwishoni kabisa yaani dakika za jiooooni

N.b kumbuka nimejizuia kusema "wazee wa hovyo"

Sijui ni nini kiliniaminisha Kikwete " anajua" siasa za Tanzania! Imenishangaza kabisa Kikwete ameshindwa kabisa kuzisoma alama za nyakati! Nchi hii imebadilika mno! Kikwete kapigwa chenga ya mwili mchana kweupe!
 
Duu... yaani kweli ulikuwa unadhani Asha Rose ni kiongozi mzuri mpaka siku aliposema Samia hoyee? Huyu mbona ni kiazi siku zote? Kama wana tofauti na Samia basi ni ndogo sana.... may elimu yake siyo ya kuunga-unga kama Samia.
Hili taifa limejaa viongozi wajinga wajinga tu wasioweza kulinda standard zao. Watu kama Salim A. Salim na Agustino Mahiga , Warioba na wengineo wa wakati ule hawa ndio mfano wa viongozi wazuri Tanzania iliwahi kupata na sio huyo mpuuzi Migiro.
 
Hananja alifurahi hadharani wakati makanisa ya Gwajima yanafungwa
Asante mkuu, alikosa hata hekima ya kukaa kimya tu! Inasikitisha! Aliyekosea (kama kuna makosa ni Gwajima) Sio waumini wake ambao wamezagaa Tanzania, wako huko mikoani hata huwa hawajui nini kinatokea Dar es Salaam! Umpende Gwajima au umchukie, huwezi kutoa adhabu ya namna hiyo! Ni aibu kwa Waumini wa madhehebu ya Kilokole. Gwajima angebeba tuhuma zake mwenyewe! Sio waumini.
 
Natamani niweke Orodha ndefu lakini hebu tuishi na hii kwanza..

Kuna wazee ambao tulidhani wangekuwa "dawa" hapo mwanzo lakini ghafla heshima yao waliyojitengenezea imepukutika kama barafu kwenye jua kali

10. Mzee Butiku.. huyu tulidhani angekuwa msaada kabisa lakini kuna tetesi huyu ndio alimchoma Pole pole.. aibu sana

09. Mzee Alkael Mbowe ilifika hatua akaitwa "kamanda" lakini ona heshima yake ilivyoshuka usiku mmoja tu!

08. Mzee (Mchungaji) Hananja: huyu aliheshimika mpaka akawa anaitwa Sehemu mbali mbali kuhutubia lakini akaweka njaa mbele

07. Mzee (askofu) Malasusa huyu siwezi kumsemea sana ila mnaona wenyewe

06. Mzee Rioba (wa TBC) huyu ni mmoja wa wazee ambao anaona uchawa na unafiki pekee havitoshi.. ila heshima yake imeshuka

05. Mzee Wasira: huyu angekataa tu ile nafasi ya umakamu kuliko kuendelea kukomaa wakati tayari mwili unakataa

04. Mzee Mwambegele (mzee wa Tume) hivi ataficha wapi uso wake baada ya hii 98% ? Yaani hata akistaafu akienda kucheza na wajukuu lazima watamzomea tu

03. Mzee Azim Dewji (baba Mo) huyu mzee alisema Pole pole anatafuta kiki huyu mzee anajishushia sana heshima kulinda uraia na biashara zake... Yupo radhi alambe miguu ya viongozi wa CCM

02. Mzee Tido Mhando alijijengea heshima kubwa lakini toka apambane kumsafisha Rostam na sasa anapambana kuwasafisha 'wanamtandao" heshima yake imerudi hadi "sifuri"

01. Mzee wa Msoga: binafsi huyu alikuwa Raisi wangu pendwa.. ila kumbe i was wrong.

Sote tunajionea haya yote yanatokea ni kwasababu yake na hakika amestahili kuwa namba moja kwenye hii Listi ya wazee waliokuwa wanaheshimika ila wamekuja kujishushia heshima yao mwishoni kabisa yaani dakika za jiooooni

N.b kumbuka nimejizuia kusema "wazee wa hovyo"
Kikwete alibagazwa sana kipindi cha JPM, nadhani nae ana-vegeance.
 
Baba yake MO anaitwa Ghulam Abbas Dewji

Screenshot_20251123_094644_Chrome.jpg
 
Ndio maana nimekuuliza ni kipindi gani hizo mada zimeanza kukoma kuwepo? Wewe umeanza lini kujibu hoja zao humu?

Mada za dini hazinaga mwisho zinapotea na kurudi tena, mimi najua ndio ziko hivyo na kuna wakati zinazidi sana.
Miaka kama 7 ...mada zimesha kufa kwa wale waislamu waliokuwa magwiji wa mijadala ya dini ...wamekimbia awathubutu kuleta mada tena ...ukiona muislamu kaleta mada ujue huyo ni mgeni hapa JF
 
Back
Top Bottom