Oryx Energy Rally of Tanzania

Oryx Energy Rally of Tanzania

hekimatele

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2011
Posts
9,890
Reaction score
2,795
Nimetoka kwenye press conference hapo Southern Sun wametangaza kuwa Rally of Tanzania inayodhaminiwa na ORYX inatarajiwa kuanza Ijumaa hii na kumalizika jumapili (14th - 16th June 2015) ambapo jumla ya magari 36 yataingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombea ubingwa wa Rally mwaka huu. Madereva wote wame confirm kushiriki ambapo Kenya gari mbili zitashiriki, Uganda pia 2 na Rwanda pia mbili na waliobaki wa Tanzania watashiriki.

Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ndiye atakaekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi utakaofanyika pale Tazara Ijumaa saa 9 mchana baada ya swala ya Ijumaa.

Rally map inaonesha kuna stage zifuatazo
KAZIMZUMBWE,
BANDA FOREST,
SUNGWI, na
KITANGA

Wadhamini waliojitokeza mwaka huu ni
ORYX Energy (Main Sponsors)
Southern Sun Hotel,
National Insurance Corporation of Tanzania,
Knight Support,
Radio Wave,
UTrack,
Obi,
HP,
Epidor,
DB Shapriya,
A to Z,
Red n White,
Tarmol na
Maji Poa.

Rockcity native, Salamander, BAK, MAMMAMIA, Julius Kaisari, makongo, The skipper, pig man, Root, mabesela, pierre tall, Given Edward, Jonas justin, Mphamvu, Chachu Ombara, Amavubi, Watu8, OKW BOBAN SUNZU, kichwat, zugimlole, rubaman, Polite, ndetichia, Bob Fern, Evz, magwio, Sangomwile, privacy, ChiefmTz piteni na hapa acheni kukomalia kandanda tu daily. Tehe tehe tehe
 
Utoto nilikuwa shabiki mkubwa sana wa mashindano haya ya Dar-es-salaam, nilikuwa naamka hasubuhi sana kuwahi uwanja wa taifa. Enzi za Dudu, kama mtamkumbuka. Na ile familia ya mashabiki wa Simba wakina Muchacho.
 
Kaka hii mambo enzi za kina Babu ilikuwa maarufu sana sijui kwa sasa hali ipoje...
 
Samahani mtoa mada.
Je rally inaanzia wapi?
Ningekuwa na Subaru WRX STi hakika ningejaribu hata kuwa escot.
Ipo siku nami nitakuwa hapo. Ngoja tuendeleze vigari vyetu
 
Hahahhahahahahhahahahhahha...ni kwel mkuu,ni mshabiki wa hzi mbio za magari pia..
 
Samahani mtoa mada.
Je rally inaanzia wapi?
Ningekuwa na Subaru WRX STi hakika ningejaribu hata kuwa escot.
Ipo siku nami nitakuwa hapo. Ngoja tuendeleze vigari vyetu

Usitafute balaa, kama sio familia basi JF bado wanakuhitaji.
 
ImageUploadedByJamiiForums1433864943.651048.jpg

ImageUploadedByJamiiForums1433865060.496358.jpg

Hii sitakosa.
 
Usitafute balaa, kama sio familia basi JF bado wanakuhitaji.

Mkuu usiwe na wasi wasi kabisa. Nilishawahi piga nguzo ya umeme nikaachana na hayo mambo ma sitaki kabisa. Niliona kifo mbele yangu kama ningekuwa nimefunga mkanda leo hii ningekuwa maiti.
Mana niliiona nguzo yaja machoni nikahama kiti ikachana pale pale kwa dereva.
 
hekimatele lini wataonyesha manjonjo na wapi ile pasha moto kabla ya safari
 
Last edited by a moderator:
Utoto nilikuwa shabiki mkubwa sana wa mashindano haya ya Dar-es-salaam, nilikuwa naamka hasubuhi sana kuwahi uwanja wa taifa. Enzi za Dudu, kama mtamkumbuka. Na ile familia ya mashabiki wa Simba wakina Muchacho.

Mimi pia nilikuwa mpenzi sana wa huo mchezo, nawakumbuka Kabombe na Viran aliyekuwa mpenzi mkubwa wa Yanga, sijui alikuwa ndio mmiliki wa Keko gereji au boby soap waliyekuwa wadhamini wakubwa wa Yanga miaka ile
 
Utoto nilikuwa shabiki mkubwa sana wa mashindano haya ya Dar-es-salaam, nilikuwa naamka hasubuhi sana kuwahi uwanja wa taifa. Enzi za Dudu, kama mtamkumbuka. Na ile familia ya mashabiki wa Simba wakina Muchacho.

Ni kweli kabisa usemayo mkuu.
Zamani haya mashindano yalikuwa yananoga sana.
Siku hizi naona kama yamepoa halafu hata ukiangalia mashabiki wake wachaaaacheeeeeee..
Sio kiviiiiileeeeeee
 
Kaka hii mambo enzi za kina Babu ilikuwa maarufu sana sijui kwa sasa hali ipoje...

Hujakosea mkuu ila njoo uone walau ya mwaka huu ikoje.
Wataanzia hapa town Southern Sun ila uzinduzi rasmi ni pale Tazara saa 9 mchana Ijumaa.
 
Samahani mtoa mada.
Je rally inaanzia wapi?
Ningekuwa na Subaru WRX STi hakika ningejaribu hata kuwa escot.
Ipo siku nami nitakuwa hapo. Ngoja tuendeleze vigari vyetu

Umesikiliza ushauri wa Salamander lakini?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom