Oscar Kambona: Mwanasiasa aliyegeuka mwiba kwa Mwalimu Nyerere

Oscar Kambona: Mwanasiasa aliyegeuka mwiba kwa Mwalimu Nyerere

Peter Stephano 809

Senior Member
Joined
Feb 29, 2020
Posts
120
Reaction score
162
FB_IMG_1583131500284.jpeg

Vijana ni nguzo ya Taifa hivyo Taifa lolote halina budi kuwa na vijana wenye weledi wa Mambo pamoja na Utashi katika kufanya Mambo, Jambo ambalo linaweza kuwapa historia kubwa hata baada ya mwisho wa uhai wao kitaifa na Kimataifa.

Tanzania kama Taifa liliasisiwa na Vijana makini kwa wakati ule, Oscar Kambona ni mmoja kati ya vijana walioandika historia ya taifa hili kabla na baada ya uhuru.

Hii ilikuwa ni kutokana na harakati zake katika kudai Uhuru na hata baada ya uhuru akiendelea kuleta changamoto ya mawazo chanya ambayo hadi leo imekuwa misingi ya Taifa hili.

Kambona alizaliwa Agosti 13, 1928 katika kijiji kidogo cha Kwambe kilichopo katika fukwe za ziwa Nyasa karibu na Mbamba Bay wilaya ya Nyasa.

Alikuwa ni mtoto wa kiume wa bwana David Kambona na Bi. Miriam Kambona. Baba yake alikuwa ni miongoni mwa waafrika wa mwanzo kupewa cheo cha uchungaji katika Kanisa la Kianglikana Tanganyika.

Oscar Mambona alipata elimu yake ya msingi chini ya mti wa mwembe ambao hadi sasa ungali umesimama huko kijijini kwao. Alisomeshwa na wazazi wake pamoja na mjomba ambaye nae alikuwa mwalimu.

Baada ya hapo alijiunga na shule ya kati ya mtakatifu Barnabas Liuli (St Barnabas Middle school) ambayo haikuwa mbali sana kutoka kijijini kwao.

Oscar Kambona alibahatika kulipiwa ada na Askofu wa Kanisa la Kianglikana Tanganyika kwani baba yake hakuwa na uwezo wa kumudu kulipa ada hiyo ambayo ilikuwa ni takribani paundi 30 za kiingereza kwa mwaka. Inasemekana Kambona alimshawishi askofu huyo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusoma sala ya Baba Mtakatifu kwa lugha ya kiingereza.

Hii ikawa hatua nyingine njema kwa Kambona kwani baada ya hapo alichaguliwa kujiunga na Shule ya wavulana ya Tabora ambapo kwa mara ya kwanza alikutana na Julius Nyerere ambaye alikuwa tayari amefundisha shule ya Mtakatifu Maria ya mjini Dodoma.

Kambona alikuwa ni kijana mwenye ushawishi na umaarufu mkubwa. Baada ya mwalimu Nyerere yeye alifuata. Mawazo yake juu ya ukombozi yalimfanya akubalike na kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa TANU huku mwalimu Nyerere akiwa mwenyekiti.

Alishirikiana kwa ukaribu sana na watanganyika wengine kupigania uhuru, mnamo mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru kutoka kwa mwingereza .

Baada ya uhuru, Kambona alibaki kuwa na ushawishi mkubwa hata baada ya muungano ambao ulizaa Tanzania na ikaaminika kuwa angekua Rais baada ya Mwalimu Nyerere kustaafu au kung’atuka madarakani kwa sababu yoyote ile.

Uwezo wake katika kuongoza ulithibitika pale alipokuwa Waziri wa Ulinzi alipowatuliza wanajeshi ambao walifura wakitaka kuipindua Serikali mwaka 1964 ambapo Rais Nyerere na Makamu wake Rashid Kawawa walipelekwa mafichoni sehemu salama kutokana wanajeshi kutaka kuwadhuru.

"Asante Sana ahsant endugu yangu" hii ndiyo ilikuwa kauli pekee ya Rais Nyerere baada ya upepo huo wa jaribio la Mapinduzi kupita alijitokeza hadharani kumshukuru kambona kwa kazi kubwa aliyoifanya kuwatuliza wanajeshi.

Viongozi wawili hawa walianza kutofautiana miaka michache baada ya uhuru. Mgawanyiko wa kwanza ulikuwa mwaka 1964 wakati wa jaribio la mapinduzi na mgawanyiko wa pili ulikuwa mwaka 1965 Tanzania ilipoingia rasmi kwenye mfumo wa chama kimoja.

Kama mmoja wapo wa baraza la mawaziri, Oscar alipinga mabadiliko hayo akidai kuwa hakukuwa na mikakati wala mwongozo kwa Serikali kikatiba kutawaliwa na chama kimoja huku hofu yake kubwa ikiwa Katiba ilikuwa haina ulinzi kama nchi ama Serikali itageuka kuwa ya kidikteta.

Mwaka 1967 baada ya azimio la Arusha lililoazimia Ujamaa na Kujitegemea, Kambona alikuwa haamini katika Ujamaa hivyo alipingana na mfumo huu akiitaka Serikali kuanzisha sehemu chache za matazamio kama mfumo huu ungekidhi maendeleo kitaifa.

Utofauti mkubwa wa Rais Nyerere na Kambona ulikuwa kwenye masuala ya kisera ambapo Kambona alikuwa si muumini wa sera ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo Nyerere alikuwa akiiamini.

Kuna msemo wa kiswahili usemao "Fahari wawili hawakai zizi moja". Mnamo mwezi Julai 1967, Kambona aliondoka nchini akiambatana na mke wake pamoja na watoto wake kuelekea London nchini Uingereza. Kuondoka kwake kuliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo radio, magazeti na runinga.

“Mwacheni aende” hiyo ndio sauti kuu iliyotoka katika kinywa cha Mwalimu Nyerere aliposikia kuondoka kwake, pia alisisitiza kuwa Kambona aliondoka na kiasi kikubwa cha pesa ambacho hakikuendana na mshahara wake.

“Je, alipata wapi mapesa yote yale" Nyerere alihoji kwani kulikuwa na tetesi kua alijitajirisha alipokuwa ofisini kupitia pesa za Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika chini ya Umoja wa Afrika (OAU) ambapo yeye alikuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya ukombozi Kusini mwa Afrika.

Naye Kambona hakutaka kushindwa mara moja, alijibu tuhuma hizo mbele ya umma wa wanahabari huko ughaibuni akisema “Sina hatia yoyote juu ya hili, iwapo kuna mwenye ukweli basi anifanyie uchunguzi na anianike hadharani”.

Mwaka uliofuata wa 1969, Kambona alitangaza kuwa atafanya Mapinduzi mnamo mwezi wa Oktoba, lakini bado mpango wake ukakwama kwani wahisani wake wote walitiwa nguvuni na Kambona alishitakiwa kwa UHAINI licha ya kuwa ughaibuni na hukumu ikasomwa mahakamani.

Wakati wa hukumu, mmoja wa washirika wake “John Chifupa” aliulizwa: “Je, ulimaanisha nini uliposema unataka kummaliza Nyerere? Chifupa akakana akisema “la hasha hakimu mimi sikumaanisha kummaliza Nyerere kimwili bali nilimaanisha nataka kummaliza kisiasa”

Baada ya kesi hiyo kuunguruma miaka kadhaa, Kambona aliendelea kuwa mwiba kwa Serikali ya Mwalimu Nyerere akiwa huko ughaibuni mpaka pale Nyerere alipong'atuka madarakani.

Ilikuwa mwaka 1992, baada ya Tanzania kurejesha mfumo wa vyama vingi naye Kambona akaamua kurejea nyumbani Tanzania na kujiunga na chama kimojawapo cha siasa baada ya kukaa uhamishoni kwa muda mrefu zaidi ya miaka 25.

Licha ya kuwa mstari wa mbele katika kupigania Uhuru miaka ya 1960, Kambona alinyimwa nafasi ya kugombea uongozi katika chaguzi zote za miaka ya 90 ikidaiwa kuwa si mtanzania bali Mmalawi. Wengine walisikika wakisema ni raia wa Msumbiji. Kambona alijibu mapigo kwa kumwambia Nyerere nae si mtanzania bali Mnyarwanda.

Mnamo mwezi Julai 1997 huko London, Uingereza, Oscar Kambona aliaga dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kambona atabaki katika historia ya vijana wa wakati ule akijumuishwa na vijana wengine jasiri wa wakati huo kama Chifu Said Fundikira na wengine wengi waliokuwa mstari wa mbele katika siasa na maendeleo ya Taifa.
 
Nyerere hakuwahi kumsamehe Kambona hadi siku Oscar anaiga dunia. Mwandishi mkongwe Ahmed Rajab ambae alikua na usuhuba na Mwalimu Nyerere alisema hayo katika moja ya simulizi zake

Rajab alisema Mwalimu Nyerere alikua London kwa mwaliko wa taasisi moja ya kimataifa iliyokua inajihusisha na mambo ya Demokrasia na Maendeleo, na yeye Ahmed pia alikua amealikwa kwenye mkutano ule. Wakati wote wakikutana na Mwalimu walikua wanaongea na kutaniana, kitu ambacho kinanistaajabisha, kwani Nyerere hakua na watu wengi ambao waliweza kumtania. Wengi wakimsikiliza akiwa lecture, kuwaonya, kuwasimulia na hata wao kumuuliza maswali lakini pia akiwachekesha na wakati fulani wakivumilia kutaniwa naye na sio wao kumtania

Akiwa anajitayarisha kwenda kwenye hoteli ambayo mkutano ule ulikua unafanyika, Ahmed Rajab alipokea ujumbe kutoka kwa Mohamed Mlamali Adam(mwandishi mwingine nguli) kua Oscar Kambona amefariki dakika chache tu zilizopita

Alipofika hapo Hotelini Ahmed alifanya hima kumuona Mwalimu ili ampe habari za motomoto kuhusu kifo cha swahiba wake wa zamani. Ikumbukwe kua Nyerere alikua Best Man wa Kambona kwenye harusi yake

Ahmed anaeleza kua alipompa Mwalimu habari hizo wala hakushtuka!!! Akamwambia tu "Ok, lini? Baada ya kusema hivo Mwalimu akabadilisha mazungumzo na hakuongelea tena la heri wala la shari kumhusu Oscar Kambona. Hakika Mwalimu Nyerere hakuwahi kusamamehe aliyekua wakati fulani rafiki yake kipenzi hadi sasa hivi ambapo wote wawili wapo mbele za haki
 
Nyerere hakuwahi kumsamehe Kambona hadi siku Oscar anaiga dunia. Mwandishi mkongwe Ahmed Rajab ambae alikua na usuhuba na Mwalimu Nyerere alisema hayo katika moja ya simulizi zake

Rajab alisema Mwalimu Nyerere alikua London kwa mwaliko wa taasisi moja ya kimataifa iliyokua inajihusisha na mambo ya Demokrasia na Maendeleo, na yeye Ahmed pia alikua amealikwa kwenye mkutano ule. Wakati wote wakikutana na Mwalimu walikua wanaongea na kutaniana, kitu ambacho kinanistaajabisha, kwani Nyerere hakua na watu wengi ambao waliweza kumtania. Wengi wakimsikiliza akiwa lecture, kuwaonya, kuwasimulia na hata wao kumuuliza maswali lakini pia akiwachekesha na wakati fulani wakivumilia kutaniwa naye na sio wao kumtania

Akiwa anajitayarisha kwenda kwenye hoteli ambayo mkutano ule ulikua unafanyika, Ahmed Rajab alipokea ujumbe kutoka kwa Mohamed Mlamali Adam(mwandishi mwingine nguli) kua Oscar Kambona amefariki dakika chache tu zilizopita

Alipofika hapo Hotelini Ahmed alifanya hima kumuona Mwalimu ili ampe habari za motomoto kuhusu kifo cha swahiba wake wa zamani. Ikumbukwe kua Nyerere alikua Best Man wa Kambona kwenye harusi yake

Ahmed anaeleza kua alipompa Mwalimu habari hizo wala hakushtuka!!! Akamwambia tu "Ok, lini? Baada ya kusema hivo Mwalimu akabadilisha mazungumzo na hakuongelea tena la heri wala la shari kumhusu Oscar Kambona. Hakika Mwalimu Nyerere hakuwahi kusamamehe aliyekua wakati fulani rafiki yake kipenzi hadi sasa hivi ambapo wote wawili wapo mbele za haki
Pamoja mkuu
 
HISTORIA FUPI YA OSCAR KAMBONA

Marehemu Oscar Kambona alizaliwa mwaka 1925 katika kijiji cha Kwambe kilichopo mwambao mwa ziwa Nyasa, karibu na Mbamba-bay, wilaya ya Mbinga, Mkoa wa Ruvuma. Alikuwa mtoto wa marehemu Rev. David Kambona na Bibi Miriam Kambona.

Rev. Kambona alikuwa ni miongoni mwa Waafrika wa kwanza kupata upadre katika kanisa la Anglikana la Tanganyika. Wakati Oscar Kambona akiwa mdogo, baba yake alikuwa akimweleza kuhusu ndoto zake juu ya uhuru wa nchi yake, hivyo Oscar alikuwa akiwa na hamu sana ya kuitumikia nchi yake. Oscar alipate elimu ya msingi nyumbani kwao, chini ya mwembe (ambao bado upo), katika kijiji chao kwa kuwatumia wazazi wake wote wawili na mjomba wake, ambao wote walikuwa walimu. Baada ya hapo alipelekwa shule ya kati ya Mt. Barnabas, Liuli, na baadaye shule ya Sekondari ya Alliance, ambako alilipiwa ada na Askofu mzungu wa Anglikana kwa vile baba yake hakuweza kumudu kulipa ada ya paundi 30 kwa mwaka.

Oscar alikuwa akisimulia jinsi alivyoweza kumshawishi Askofu huyo amlipie ada kwa kusema sala ya Baba yetu kwa kizungu. Oscar alichaguliwa kwenda ‘Tabora Boy’s Senior Government School’, ambako alionana na Julius Nyerere

kwa mara ya kwanza; wakati huo Nyerere alikuwa anafundisha katika shule ya kikatoliki. Baada ya kumaliza masomo ya sekondari alienda katika shule yake iliyopita ya Alliance kama mwalimu na baadae alichaguliwa kuwa ‘Schoolmaster’. Ilikuwa katika mkutano wa kitaifa wa walimu, mnamo mwaka 1954, ambapo Kambona na Nyerere walikutana tena. Kambona alikuwa tayari kukitumikia chama cha TANU ambacho kilikuwa kimeanzishwa muda si mrefu, lakini Nyerere akasema wasingeweza kumwajiri kwa vile chama kilikuwa hakina fedha.

Kambona akasema chama hakikuwa na fedha kwa vile hakikuwa na ‘organising secretary, na ndipo alipoamua kufanya kazi hiyo ili kujenga chama, bila ya malipo’. Aliishi kwa kutegemea akiba aliyojitunzia kwa kufanya kazi miezi 6. Katika kipindi hiki Kambona alisafiri sehemu mbalimbali za nchi na kuonana na machifu na wazee wa vijiji ili kusajili wanachama.

Katika miezi 6 alifanikiwa kusajili wanachama 10,000, na hadi kufikia mwaka mmoja alikuwa amepata wanachama hai 100,000. Kambona alitumia michango aliyopata kufungua akaunti ya kwanza ya TANU. Kisha alienda Butiama kumshawishi Nyerere achukuwe uongozi wa chama moja kwa moja. Baada ya miaka mitatu Kambona aliamua kwenda kusomea sheria katika Chuo cha Middle Temple, nchini Uingereza mwaka 1957 kwa ufadhili wa Gavana.

Akiwa London Kambona alikuwa kiongozi wa chama cha wanafunzi wa Tanganyika na Mwenyekiti wa tawi la TANU la London. Ni wakati huo ambapo Kambona alipata fursa ya kukutana kwa mara ya kwanza na watu mashuhuri kama George Padmore, mwanaharakati wa umoja wa Afrika, ambaye alimshawishi ahudhurie mkutano wa mwaka 1958 wa waafrika wote(All Africa’s Peoples Conference), uliofanyika nchini Ghana muda mfupi baada ya kupata Uhuru.

Akiwa Ghana Kambona alipata nafasi ya kukutana na mwanaharakati mwingine maarufu wa siasa za Afrikla, Kwame Nkurumah. Akiwa uingereza Kambona alikuwa mwaafrika wa kwanza kutangaza taarifa ya habari kwa Kiswahili katika idhaa ya kiswahili ya BBC. Aliporudi nchini Tanganyika, mwaka 1959, TANU ilikuwa imeshaweka bayana madai yake ya kupewa serikali ya madaraka, vinginevyo TANU ilikuwa tayari kuanzisha mapambano kama ilivyokuwa kwa Mau Mau ya Kenya.

Wakiwa London wakisubiri kupewa madaraka ya ndani, Nyerere na Kambona walijadili hatua mbalimbali ambazo zingechukuliwa ili kuepuka kutoweka kwa amani. Wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Londoni 1991, Kambona alikumbuka matukio kama hivi, ‘’Bwana Nyerere alikuwa akiishi nami katika chumba kidogo nilichopewa chuoni. Tulijadiliana ni namna gani angeweza kurudi nyumani na kuonana na wafuasi wake bila kupewa serikali ya madaraka. Baadae nilifanikiwa kumshauri kuwa wakati atapozungumza na vyombo vya habari katika the East African Arch aseme kuwa walowezi wa kizungu ambao wapo Tanganyika wana hekima zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki.

Alikubali kusema hivyo endapo na yeye Kambona angekubali kukatisha masomo yake ya sheria huko London na kurudi Tanganyika ili ampe nguvu na kumuunga mkono katika kikao cha kamati kuu ya TANU wakati akitetea tamko lake la wenye hekima zaidi.

Katika uchaguzi wa kwanza TANU ilishinda viti vyote isipokuwa kimoja. TANU iliunda serikali ya mambo ya ndani chini ya Nyerere ambaye alikuwa Waziri kiongozi wa kwanza. Na katika harakati hizo za matayarisho ya serikali ya ndani, Kambona alimwoa Flora Moriyo wakati wakiwa kwenye msafara wa harakati za kukamilisha matayarisho ya uhuru na serikali ya Uingereza. Harusi ilifungwa katika kanisa la Mt. Paul, London, na Nyerere ndiye alikuwa msimamizi. Kambona aliteuliwa kuwa waziri wa Elimu.

Baadaye alishika nyadhifa za waziri wa Mambo ya Ndani, Mambo ya nchi za nje na Ulinzi na Tawala za Mikoa. Pia alikuwa mwenyekiti wa kwanza wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika na mwenyekiti wa utayarishaji wa AOU charter. Mwaka 1964, Kambona alifanya kazi kubwa katika kuunganisha Zanzibar na Tanganyika, akiwa pamoja na Raisi Nyerere, Raisi Karume na Waziri Kiongizi Hanga. Hii ilikuwa ni baada ya mapinduzi ya Zanzibar. Wakati wa wanajeshi wa kikosi cha Calito walipoasi mwaka 1964 Kambona alikuwa msuluhishi mkuu kati ya serikali na wanajeshi hao.

Nyerere na Kawawa walienda mafichoni Kigamboni. Baada ya siku tatu za majadiliano Kambona aliafiki kuongeza kasi ya kuwawezesha waafrika kushika hatamu jeshini. Katika mahojiano na gazeti la Daily Telegraph la London Kambona alisema, ‘baada ya kuwatuliza wanajeshi nilikwenda kuwatafuta viongozi wengine na kuwarudisha mjini kwa kutumia Land Rover yangu’. Hatimaye maasi hayo yalidhibitiwa kabisa na majeshi ya Uingereza na Nyerere alimsifu Kambona bushara na uaminifu wake.

Tofauti kati ya Nyerere na Kambona zilianza kujitokeza baada ya maasi ya wanajeshi. Nyerere alitaka kuanzisha mfumo wa chama kimoja nchini ili kuimarisha usalama. Kambona alipinga hoja hiyo kwa maelezo kwamba mfumo huo ungezorotesha uhuru wa watu na maendeleo ya demokrasia. Hata hivyo, Kambona alishindwa bungeni; alikataa kusaini muswada (bill). Mwaka 1967, baada ya safari ya China ya mwaka 1965, Nyerere akiwa amependezwa na mfumo wa kikomonist wa Mao, alitaka kuanzisha mfumo kama huo kwa jina la ujamaa. Dhana ya msingi ya mfumo wa ujamaa ilikuwa ni kuwahamishia watu katika vijiji vya ujamaa na kutaifisha viwanda ana mali. Kambona hakukubaliana na utaratibu huo kwa maelezo kwamba ungeongeza umaskini na udhibiti wa serikali kwa watu. Alijiuzulu kutoka katika serikali na Chama na hatimaye yeye na familia yake walikimbilia Kenya na kisha Uingereza ambako walipatiwa uhifadhi wa kisiasa.

Mara baada ya kuondoka mali za Kambona zilichukuliwa. Ndugu zake wawili, waliwekwa kizuizini bila ya kufikishwa mahakamani na kufungwa kwa zaidi ya miaka kumi. Wanafamilia wengine walinyanyaswa na kuwekwa kizuizini. Wengine kati yao walibambikiziwa kesi za uhaini, wakafikishwa mahakamani na kisha kufungwa na serikali. Kati yao walikuwa Bibi Titi ambaye alipigania uhuru pamoja ana Nyerere na alikuwa kiongozi wa jumuia ya kina mama.

Alikuwepo pia Michael Kamaliza ambaye alikuwa mwanaharakati wa chama cha wafanyakazi, mwanachama wa TANU na waziri. Wengine ni pamoja na Gray Mattaka, John ana Eliya Chipaka na Prisca Chiombola. Kambona alituhumiwa kuwa kiongozi wa wahaini wakati akiwa London na alihukumiwa bila kuwapo.

Watuhumiwa hatimaye walikata rufaa katika mahakama kuu ya Afrika Mashariki na wakaachiwa huru. Hata hivyo, baadae walikamatwa na serikali na kufungwa tena. Kambona alituhumiwa kuwa aliiba pesa nyingi sana zikiwa ni mali ya umma, kitu ambacho Kambona alikataa katika taarifa yake na waandishi wa habari Septemba 6 huko London 1967. Tuhuma hizo zilisema kuwa ‘’ Kambona amekutwa na pesa nyingi sana kama karanga alipopekuliwa katika Uwanja wa ndege Embakasi Nairobi’’ Hata hivyo Kambona katika taarifa yake kwa waandishi wa habari alikanusha kuhusika na tuhuma hizi na badala yake akaipa serikali ya Tanzania kuiomba serikali ya Kenya kutoa ukweli juu ya jambo hilo- jambo halikufanyika. Akiwa Londoni Kambona aliishi maisha ya shida na dhiki. Katika mwaka 1982 ndugu zake Kambona na Otini Kambona walifunguliwa kutoka kizuizini baada ya juhudi za waziri mkuu wa New Zealand Robert Muldoon.

Katika mwaka 1990 Kambona akiwa na matumaini makubwa ya mabadiliko ya kisiasa katika Tanzania hususani mabadiliko ya demokrasia, aliunda chama kiitwacho Tanzania Democratic Alliance. Wakati vyama vingi vilipoanzishwa Tanzania 1992 Kambona aliomba kurudi Tanzania. Serikali ya Tanzania ilimkatalia katakata na kudai kuwa Kambona hakuwa Mtanzania. Kambona badala yake aliomba Serikali ya Uingereza kumpa pasi ya kusafiria kurudi Tanzania. Hata hivyo Serikali ya Tanzania ilitamka kwamba pamoja na kupata pasi hiyo itamweka ndani pindi atakapoingia Tanzania. Pamoja na msimamo huo wa Serikali, Kambona alitua kwenye ardhi ya Tanzania tarehe 5 september 1992. Hakuna mamlaka iliyomkamata bwana Kambona bali alipewa miezi mitatu awe amekamilisha utata wa uraia wake.

Baada ya kurudi, Tanzania aliona kuwa harakati za kuelekea kwenye demokrasia ya kweli zilikuwa zikienda kwa mwendo wa kinyonga. Hata hivyo Kambona hakuweza kujihusisha kwa kiasi kikubwa na siasa kutokana na matatizo ya kiafya hususani shinikizo la damu. Hatimaye Oscar Kambona alifariki akiwa katika matibabu mjini London mwezi Juni 1997. Mdogo wake Otini Kambona naye alifariki katika kipindi hichohicho kutokana na magonjwa ya moyo.

Wote wawili walizikwa Tanzania, na serikali ya Tanzania iligharimia gharama zote za usafirishaji miili ya marehemu ndugu hawa. Oscar Kambona ameacha mke na watoto wawili. Mtoto wao wa kwanza Mosi Kambona aliuawa mjini London katika mazingira ya kutatanisha. Roho ya Oscar Kambona na ndugu na jamaa wote waliotangulia MWENYEZI MUNGU aziweke pema peponi, Amin.
 
Huyu jamaa natamani sana nipate historia yake kamili ila ndo vile vitabu vingi vya historia vinamgusia kwa uchache sana.
 
Oscar Kambona.
Kuna wakati ukitaka kumwangamiza mtu basi muhusishe na Kambona.

Hii ilikuwa baada ya Kambona kukimbilia Uingereza kufafuta hifadhi.
Namweleza Oscar Kambona:

MASAHIHISHO
Katika video nasema Mwalimu Nyerere aliondoka Dar es Salaam kwenda Butiama baada ya kuundwa kwa TANU.

Ulimi umeteleza.

Mwalimu aliondoka Dar es Salaam kwenda Butiama baada ya kuacha kazi.

Kambona akatumwa kwenda kumrudisha President wa TANU New Street.


View: https://youtu.be/u4dHCqHCbPI
 
Shekhe umekuja tena na hekaya zako

USSR
USSR,
Mimi si Sheikh.
Tatizo hili hapa tulilimaliza miaka mingi iliyopita.

Wengi hapa wananiita Mzee Mohamed.
Kwani ndugu yangu kalamu yangu inakubughudhi?

Huu uwanja kila mtu anaandika akipendacho.

Ikiwa labda kuna sheria inayozuia kuandika kwa namna fulani tafadhali nifahamishe.
 
Bagamoyo,

Ahsante sana kwa kutuwekea hazina hii.

"Ten Africans," nimekisoma na kipo katika Bibliography ya kitabu cha Sykes.

Martin Kayambo yupo pia katika, "Modern Tanzanians," nacho pia kipo katika Bibliography ya kitabu cha Sykes.

Katika "Modern Tanzanians," Martin Kayamba anasifiwa kwa makubwa aliyofanya na halikadhalika anashutumiwa kwa kuwa kibaraka wa Waingereza.

Kitabu hiki kimekusanya Biography kadhaa za Waafrika maarufu wa karne ya 20 mwanzoni lakini mimi zilizonivutia ni ya Kleist Sykes, Martin Kayamba na ya Ali Juma Ponda na Hassan Suleiman.
 
Back
Top Bottom