Oscar Oscar: Kwanini Polisi hawajawahi kukamata viongozi wa CCM? Je, hawakosei?

Oscar Oscar: Kwanini Polisi hawajawahi kukamata viongozi wa CCM? Je, hawakosei?

Jumapili hii taarifa za kukamatwa kwa viongozi wa CHADEMA akiwepo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, Makamu mwenyekiti Tundu Lissu na viongozi wengine zilitangazwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.Taarifa rasmi ya msemaji wa CHADEMA ilieleza pia.

Hii Siyo Mara ya kwanza, kwa viongozi Hawa kukamatwa ikumbukwe kuwa kabla ya 4R Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh Mbowe alikuwa na kesi na alikaa gerezani kwa muda mpaka alipoachiwa.

SWALI NI KUWA JE CCM WAKO JUU YA SHERIA? Sijawahi kushuhudia tokea nijitambue kuona Mwenyekiti wa CCM au katibu wake au Makamu mwenyekiti akikamatwa na polisi kwa sababu yoyote ile! HATA wakati wa Magufuli sauti zilivyovuja hakuna aliyekamatwa?

Jeshi la polisi limekuwa kinara wa kushughulika na wapinzani badala ya kushughulikia mafao ya askari wao.

CCM Kama haitaki demokrasia itangaze kuwa Tanzania ni Serikali ya chama kimoja ili tujue. Ione Kama Watanzania siyo watu wa mchezomchezo.

View attachment 3068506
Viongozi wote wa CCM ni 'Watakatifu,' ni wasafi kama 'Malaika'
 
CCM wanafuata sheria bila shuruti, tena CCM wakiambiwa mara nyingi hakuna kuandamana na Polisi, hawashindani na Polisi hata siku moja..

CCM mara nyingi tu wamekataliwa maandamano ya amani na wanatii sheria bila shuruti tena hawashindani na polisi

CHADEMA ILI WATII SHERIA, lazima SHURUTI ITUMIKE, bila KUTUMIA SHURUTI, CHADEMA HAWATII SHERIA
 
Weledi Kwa polisi ni zero.Naamini ccm hata akiamua kuanza kampeni kabla ya muda atafanya vizuri tu lakini afanye mpinzani utasikia intelijensia Imebaini viashiria vya uvunjifu wa amani.Polisi kuweni weledi,mpo Kwa matakwa ya Sheria na siyo matakwa ya watawala.
Oscar mdogo wangu.... watawala hapa TZ wanaugua Chademamonium🤣🤣🤣🤣.....
 
CCM wanafuata sheria bila shuruti, tena CCM wakiambiwa mara nyingi hakuna kuandamana na Polisi, hawashindani na Polisi hata siku moja..

CCM mara nyingi tu wamekataliwa maandamano ya amani na wanatii sheria bila shuruti tena hawashindani na polisi

CHADEMA ILI WATII SHERIA, lazima SHURUTI ITUMIKE, bila KUTUMIA SHURUTI, CHADEMA HAWATII SHERIA
😃😃😃Sheria ipi iliyovunjwa au unabwabwaja, taja kifungu!!
 
Back
Top Bottom