Othman Masoud Othman Sharif ateuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Congratulations to him. Is he also a pain in the CCM's ass?
 
Hapa kazi tu watu wanaojiamini ndio anaowahitaji Mheshimiwa Magufuli ,hapa tayari yanayofurahisha yanazidi kushika kasi.
Ila cheo alichonacho hakina mashiko si ajabu mkamuona anatembea na mikasi ,CCM bana ! Nina wasiwasi ukoo wa Mwinyi unataka kuwa na ufalme pale Zanzibar,yaani hati miliki ya zanzibar hawa jamaa wanatuacha sasa, wanasema furaha yao watajenga jumba moja refu kuliko lile la uarabuni watakuwa wanatuona huku Tanganyika.
Bye bye Tanganyika ,fanyeni muwarudishe mashee ili haki itendeke,Sheni ametuletea mashee wakati awatuhusu, Magu mrudishie Sheni mashee wake. Saa mbaya tukae chonjo tujenge Tanganyika yetu na Magufuli wetu.
 
Kwa misimamo yake ninavyomjua huyu asipokuwa makini !!!!!!
Naomba niishie hapo.
 
Safi Sana. Huyu jamaa ni muumini wa mamlaka kamili ya Zanzibar na wazanzibari, hatakagi ujinga huyu.

Aliitupilia mbali nafasi yake ya kuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar wakati wa mjadala wa katiba mpya kwa kusimamia anachokiamini.

Bravo ACT!
Hiyo nafasi ni ceremonial; hatakuwa na madhara yoyote. Mamlaka anayo rais na makamu wa pili, kama Samia na Majaliwa walivyo.
 
Dah Kule Unguja hamtapata Mwamba Kama Maalimu Jamaa alikua Mwamba kweli kweli sio mchezo...Ila nae alikosea alitakiwa azae sana hasa kidume kije kubeba maono yake angeoa wake 4 dini yetu inaruhusu.
Ufalme umetokea wapi
 
Dah Kule Unguja hamtapata Mwamba Kama Maalimu Jamaa alikua Mwamba kweli kweli sio mchezo...Ila nae alikosea alitakiwa azae sana hasa kidume kije kubeba maono yake angeoa wake 4 dini yetu inaruhusu.
Jamaa haamini sana kwenye kuzaa, nakumbuka miaka ya themanini tukiwa kwenye ziara yake aliwaambia wakazi wa Mbulu waliomhoji kuhusu kupatiwa umeme; "Umeme wa nini huku? Laleni saa 12 jioni mzaane kama kuku"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…