Othman Masoud Othman Sharif ateuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Othman Masoud Othman Sharif ateuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Huyu nae bado anaitwa makamu wa rais wa kwanza???
 
Hiki ni chuma
Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar leo amemteua Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais kufuatia kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad.

Uteuzi huo umefanywa na Rais kwa kuzingatia matakwa ya Kifungu cha 9(3) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, na vilevile baada ya kushauriana na Chama cha ACT-Wazalendo.

Uteuzi wa Othman Sharif unaanza leo na ataapishwa kesho Machi 02, 2021 Ikulu Zanzibar.

Pia soma

 
Hapo tupo p1 mkuu hili ni jembe
Safi Sana. Huyu jamaa ni muumini wa mamlaka kamili ya Zanzibar na wazanzibari, hatakagi ujinga huyu.

Aliitupilia mbali nafasi yake ya kuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar wakati wa mjadala wa katiba mpya kwa kusimamia anachokiamini.

Bravo ACT!
 
Safi Sana. Huyu jamaa ni muumini wa mamlaka kamili ya Zanzibar na wazanzibari, hatakagi ujinga huyu.

Aliitupilia mbali nafasi yake ya kuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar wakati wa mjadala wa katiba mpya kwa kusimamia anachokiamini.

Bravo ACT!

Ila kila siku comments za humu ndo mana CCM itatawala mpaka ichoke. Mnajiona mna akili sana mnadhani CCM Ni chama cha kubahatisha. Kila kitu kina baraka zao tena wanaona mbali sana kuliko nyie waangalia mbele ya Pua zenu.
 
wakati wa bunge la Katiba walimzingua na yeye akawazingua vile vile.
 

Makamu wa Kwanza wa Rais Mh. Othman Masoud Othman Sharif​

Moja ya interview bora kabisa kuweza kumfahamu kiongozi huyu mpya wa juu Tanzania mwenye maono makubwa

Juni 8, 2020
Othman Masoud: Zanzibar haikuanza 1964 - Part 1

Othman Masoud Othman anarejelea umuhimu wa historia na kutupeleka kwa muasisi wa mapinduzi ktk nchi za Latin Amerika, Simon Bolivar Simon Bolivar and the Spanish-American revolutions .

Nini maana ya uchaguzi ? Shujaa wa latin Amerika aliyeshiriki kuleta mapinduzi katika nchi 6 za Latin Amerika ikiwemo Bolivia na Venezuela alitoa hotuba murua mwaka 1819 mwezi February tarehe 15... ktk Bunge la Venezuela....

Othman Masoud Othman aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya SMZ , amesema kwamba ni makosa kudhani kwamba Zanzibar ilianza mwaka 1964 baada ya Mapinduzi au 1995 baada ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi na kwamba jambo ambalo haliwezi kuepukika muda wote ni mabadiliko. Msikilize kwenye sehemu hii ya kwanza ukijitayarisha kwa ajili ya sehemu ya pili ya mazungumzo aliyofanya na Radio Noor ya Mjini Unguja.

source : weyani TV

source: Meet 10 Heroes of South American Independence

Safi sana, tutafaidika sana na madini yake adhimu, huyu nikisoma maandiko yake pia kusikiliza hotuba/ mihadhara yake ya kisomi huwa najifunza mengi sana. ACT-Wazalendo imetuletea kwa Zanzibar, Tanganyika, Tanzania na Afrika kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom