Othman Masoud: Tumeambiwa Bunge la Katiba linarejea septemba mwaka huu, Zanzibar yenye mamlaka kamili yanukia

Mhe Othman Masoud ameyasema hayo wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Chakwani leo 30.07.2023. Ametumia mkutano huo kuwaeleza wananchi hao ubaya wa Katiba pendekezwa almaarufu katiba ya Sitta na Chenge. Amesema wazanzibar waende wakadai Zanzibar yenye mamlaka kamili. Atayekaye waangusha watamuuliza 'wewe mwenzetu mbegu ya Kongo au ya Burundi?'

My take: wazanzibar wanajipanga kudai nchi yao sisi tunalumbana kuhusu bandari za Tanganyika, tunaingia bunge la katiba bila msimamo wa pamoja. Twendeni tukadai Tanganyika yenye mamlaka kamili.
Aliyewaangusha kwa kukataa Katiba Pendekezwa ya Tume ya Warioba ni nani kama sio Samia Katika zile Kura ?
 
Ikiwa Wazanzibari (najua sio wengi) watataka wajitenge, ni Wazanzibari wenyewe ndio watakaopata hasara. Wabara wengi wanawachochea sana Wazanzibari wajitenge kumbe hawawapendi wakinung'unika kuwa Wazanzibari wanawanyonya! Zanzibar shauri yenu!!!
Wazanzibar wao wnaadai wananyonywa. Wanataka kujifanyia maamuzi yao.
 
Unambishia Makamu wa kwanza wa Rais? Hivi akili za kiccm zimechoka kiasi hiki? Kati yake na wewe ni nani ana taarifa za ndani zaidi?
Nakwambia hivi porojo hizo,aliyetangaza kuanza Kwa mchakato ni Waziri wa Sheria anachoongea huyo act na maoni Yako ni porojo.
 
Ikiwa Wazanzibari (najua sio wengi) watataka wajitenge, ni Wazanzibari wenyewe ndio watakaopata hasara. Wabara wengi wanawachochea sana Wazanzibari wajitenge kumbe hawawapendi wakinung'unika kuwa Wazanzibari wanawanyonya! Zanzibar shauri yenu!!!
Kwani hili jeshi lenu lilijaa kila mtaa pamoja na usalama wenu wengine wanaovaa rubega Za kimasai wanafanya kitu gani ? Tumechoka kutawaliwa na Tanganyika tuwacheni tupumuwe
 
Mwambie mzee Wasira alichofanya huko Mwanza hakikubaliki. Hotuba nzima anasema Konyagi ni mbaya. Kwa kweli ametukwaza sana wapenzi wa Konyagi.
Huyo Mzee kanywa sana Gongo wakati anauza Sato pale Msasani Namanga baada ya kutoswa na Mkapa!
 
Wazanzibar wao wnaadai wananyonywa. Wanataka kujifanyia maamuzi yao.
Hizo ni hisia mbaya wanaingiziwa na Wabara wenye Nia ovu dhidi ya Wazanzibari. Mwisho wa siku ni juu yao. Lakini Wabara wenye Nia ovu ndio watakaoshangilia zaidi ikitokea na Wazanzibari watajikuta wameingizwa mkenge!
 
Kwani hili jeshi lenu lilijaa kila mtaa pamoja na usalama wenu wengine wanaovaa rubega Za kimasai wanafanya kitu gani ? Tumechoka kutawaliwa na Tanganyika tuwacheni tupumuwe
Sina hakika kama wewe ni Mzanzibari.
 
Hizo ni hisia mbaya wanaingiziwa na Wabara wenye Nia ovu dhidi ya Wazanzibari. Mwisho wa siku ni juu yao. Lakini Wabara wenye Nia ovu ndio watakaoshangilia zaidi ikitokea na Wazanzibari watajikuta wameingizwa mkenge!
Na hili linaenda kutokea soon.

Zamani wazanzibari walikuwa wakidai kwa nguvu Muungano wa serikali Tatu.

Kwa kuwa watanganyika hawakutilia maanani ndio maana jambo hili halikufanikiwa.

Kwa sasa kutokana na mfumo mbovu uliochagizwa na DPW sasa na watanganyika wanadai Tanganyika yao.

Fukuto ni kubwa kuliko awali.
 
Kwani hili jeshi lenu lilijaa kila mtaa pamoja na usalama wenu wengine wanaovaa rubega Za kimasai wanafanya kitu gani ? Tumechoka kutawaliwa na Tanganyika tuwacheni tupumuwe
😅😅😅
 
Mhe Othman Masoud ameyasema hayo wakati akihutubia mamia ya wakazi wa Chakwani leo 30.07.2023. Ametumia mkutano huo kuwaeleza wananchi hao ubaya wa Katiba pendekezwa almaarufu katiba ya Sitta na Chenge. Amesema wazanzibar waende wakadai Zanzibar yenye mamlaka kamili. Atayekaye waangusha watamuuliza 'wewe mwenzetu mbegu ya Kongo au ya Burundi?'

My take: wazanzibar wanajipanga kudai nchi yao sisi tunalumbana kuhusu bandari za Tanganyika, tunaingia bunge la katiba bila msimamo wa pamoja. Twendeni tukadai Tanganyika yenye mamlaka kamili.
Tunadai vyote..
 
Na hili linaenda kutokea soon.

Zamani wazanzibari walikuwa wakidai kwa nguvu Muungano wa serikali Tatu.

Kwa kuwa watanganyika hawakutilia maanani ndio maana jambo hili halikufanikiwa.

Kwa sasa kutokana na mfumo mbovu uliochagizwa na DPW sasa na watanganyika wanadai Tanganyika yao.

Fukuto ni kubwa kuliko awali.
Hakuna fukuto lolote la kudai Tanganyika. Narudia HALIPO! Mambo ya Utanganyika ni ya Wabara wenye nia ovu tu dhidi ya Wazanzibari. Nami nasema, Wazanzibari wakiwasikiliza; Kalaghabhao!!!
 
Yaani Mtanganyika awe na nia ovu kwa wazanzibari? Ili afaidike nini?

Acha porojo.
 
Back
Top Bottom