sikuwa naupa nafasi huu wimbo kwenye masikio yangu ila kuna siku nilihudhuria harusi ya ndugu yangu ,basi kuna muda maharusi wakainuliwa kwenye viti na ndipo dj akaupiga huu wimbo maharusi waucheze lkn pia ukawa unaonekana kwenye screen za ukumbini bana weeeeeeee.....kuna hisia flani nilikuwa nazipata kutokana na ile moment kiujumla yani na ugumu wangu wote nikajikuta natabasamu kuanzia wimbo unaanza mpaka unaisha na kujiapia nitaupakua kwenye computer yangu nikirudi nyumbani,niliporudi home ajabu wimbo nilikuwa nao kumbe sikuwa naupa nafasi tu...jamaa anajua sana anachonishangaza pia lafudhi yake kama mtanzania tu kiswahili kimenyooka.