Otile Brown na Sanaipendi waliua kwenye nyimbo ya chaguo la Moyo

Kila nikipata nafasi siachi kwenda YouTube kuharibu MB zangu kwenye nyimbo za huyu mtu,,, anaijua Sanaa Hadi raha
Nina hd,
imejaa ngoma zote za otile tangu akiwa underground [emoji4]
 
Kilichokupa hisia ni ile sound stage performance. Tafta mziki mzuri nyumbani kila nyimbo itakuwa nzuri.
 
Nilianza kulia kwa mara ya kwanza kwenye mapenzi mwaka 2016.

Kuna demu wangu mmoja hivi alikuwa anaupenda wimbo wa huyu jamaa aliomshirikisha Baraka Da Prince (kipindi nae anang'aa) unaitwa NISEME NAWE!

Siku nakuja kuwa mbali na huyo demu kwa mara ya kwanza toka tuanze mahusiano nililia mchana na usiku kila nikipiga au kuusikia huo wimbo au kupita maeneo ambayo tulikuwa tunapenda kukaa na manzi!

Tokea hapo nikamjua na nikawa namkubali sana Otile.

Ila wanaendana sana na Jovial... Sijawahi jutia kuhusu collaboration yao!
 
Kilichokupa hisia ni ile sound stage performance. Tafta mziki mzuri nyumbani kila nyimbo itakuwa nzuri.
Kweli kabisa mkuu.

Kuna wimbo mmoja hiv wa Chike na Flavour unaitwa HARD TO FIND nilikuwa nauona wa kawaida, ila siku nilipokuja kuusikia kwenye sound kubwa... asee! niliuelewa sana!
 
Halafu najiuliza huyu jovial ni demu wake au?
Nyimbo nyingi wanaimba wote.
 
Kweli kabisa mkuu.

Kuna wimbo mmoja hiv wa Chike na Flavour unaitwa HARD TO FIND nilikuwa nauona wa kawaida, ila siku nilipokuja kuusikia kwenye sound kubwa... asee! niliuelewa sana!
Kuna nyimbo ni za kawaida until uzisikie kwenye kinu cha maana. Mfano nyimbo ya Utaniua ua ya Jux ukiisikiliza kwenye mashine ya maana ni shida
 
Binafsi naona huyu jamaa ni overrated. Bado sana na ni wa kawaida sana. Jina kubwa kweli ila bado. Akaze buti. Hata katika nyimbo anazoimba hakuna uniqueness kiasi cha kusema unamsikia yeye. Nameless, redsan, sautsol, bahati, nk. Wakiimba unajua ni sauti ya nani. Huyu jamaa bado
 
Na hakai sana anatoa chuma.

Ile na harmonize naona video ndio walizingua kidogo ilikuwa poor ila audio ni moto.

Halafu jamaa kiswahili chake kimetuliaa sio kama yale kina Willy Paul sijui pumba tupu.
Kiswahili chake uwez mdhania Kama Ni mkenya, mi pia sikudhan Kama Ni mkenya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…