Jackwillpower
JF-Expert Member
- Oct 4, 2017
- 2,467
- 3,687
Roma ndio ilianzisha Oukumene (umoja wa makanisa) na Oukumene inayaleta makanisa yote ya kikristo katika msingi mmoja na kuondoa tofauti ndogo ndogo ili wakristo wafikie umoja. Kwamba ifike mahali mkristo aweze kusali ama kuhamia kwenye kanisa lolote bila kubatizwa tena na kupokea ekaristi. Na padre aweze hata kusimama kwenye mimbari ya Waprotestant na kutoa hotuba.
Lakini kwa mujibu wa post hii ya padre Titus Amigu, Oukumene haitakaa isimame, inaonesha imeundwa kwa hila ili kumpa nguvu askofu wa Roma kwa kunyamazisha uprotestanti. Hivyo naona kuna msambaratiko huko mbele maana Wakatoliki hawapo tayari kulegeza misingi yao na msimamo wao ni ule ule kwamba "nje ya Katoliki hakuna wokovu" ingawa wao ndio wanzilishi wa mchakato huu wa umoja wa makanisa katika zama za papa Yohana wa 23 na Paulo wa 6.
Ni Waprotestant ndio wajinga, wamejiingiza wenyewe wazimawazima kwenye mtego na hivyo wameuangamiza uprotestanti kwa kufanya muhafaka na Roma, na Roma wenyewe hawawataki kulingana na padre Amigu. Labda wakanushe kuwa ni mawazo au msimamo binafsi wa Amigu nje ya msimamo wa Katoliki na Papa Fransicso. Maana padre Amigu amepinga kongamano la jumuiya ya Wakristo lililofanyika Dodoma na Dar es salaam kama usaliti juu ya Ukatoliki na kumshambulia Mwakasege ambaye ni MKKT.
Soma post hii ujionee.👇
Padre Titus Amigu Mwanza Tanzania.
MAPATO YA MWENDELEZO WA UJINGA WETU ULE ULE
Je, mmeona kilichotokea Dodoma? Mmeona? Binafsi yangu nimeona aibu, aibu kubwa. Nimeona haya ya uso, haya tele. Nimeona haya kwa niaba ya Wakatoliki, kwenye kongomano la Dodoma. Nimesikiliza mahubiri ya Mwakesege nikapata ushahidi mkamilifu wa mwendelezo ule ule wa ujinga wetu. Nimesikitika sana. Hata nyie sikilizeni mada hiyo hasa dakika thelathini za mwisho. Ameshinda! Amewateka Wakatoliki kuokoka, sijui wale mapadre wawili waliokuwa wawezeshaji wenza wameokoka nao! Wakatoliki wameokoka baada ya mada! Lakini twendeni pole pole katika mambo mawili leo: ujinga wa lugha za kale za Biblia na uovu wa kiroho.
Ujinga wa Lugha za Kale
Mada ilihusu Sauli kuwa Paulo. Kwa wanaojua lugha za kale zaa Biblia, huu ni ujinga wa wazi kwamba mtu hajui Kiebrania wala Kiyunani (Kigiriki). Niwahabarisheni. “Sauli” na “Paulo” ni matamshi ya jina moja lile lile lakini kadiri ya makabila tofauti tu, wala hakuna maana yoyote ya mabadiliko ya kitu ama mtu. Mapadre waliokuwapo pale walipaswa walau kukanusha mada hii, maana bila shaka walihudhuria vipindi vya lugha za Kiebrania na Kiyunani (Kigiriki) Seminarini. Lakini huenda walikuwa wanapenda sana kipindi cha mapumziko!
Nisikilizeni vyema. Jina “Sauli” ndiyo matamshi ya Kiebrania, yaani kwa lugha ya Wayahudi, wakati “Paulo” ni matamshi ya Kiyunani au Kigiriki kwa watu wa mataifa. Yaani kwa “SAULI” ndivyo alivyokuwa anaitwa alipokuwa anafanya uinjilishaji kati ya Wayahudi wenzake, lakini baadaye alipohamia kwa watu wa mataifa katika Asia Ndogo, Ugiriki na Roma, watu wa huko ndiyo wakawa wanamwita “PAULO.” Aidha, matamshi ya “PAULO” ni ya Kilatini vile vile. Ndiyo maana yanatumika matamshi ya “PAULO” katika nusu ya Kitabu cha Matendo ya Mitume, si vinginevyo. Hakuna suala la kiteolojia hapo.
Kwa hili, hebu niwadarasisheni kwa mifano midogo miwili. Mtu anayeitwa “CLARE” nchini Uingereza na Marekani, wanakozungumza Kiingereza, ataitwa “CIARA” nchini Italia wanakozungumza Kiitaliano, ataitwa “KLARA” hapa Tanzania maana tunatamka kwa Kiswahili, lakini huyo huyo ataitwa “KALALA” huko Songea kwani wanatamka Kingoni.
Mfano mwingine. Mtu anayeitwa “YAKOBO” huku kwetu Tanzania, ataitwa “JAMES” huko Uingereza, ataitwa “JIMMY” huko Marekani, ataitwa “DIEGO” huko Argentina wanakozungumza Kihispania na ataitwa “TIAGO” huko Ureno, Brazili, Angola na Msumbiji wanakozungumza Kireno. Hivi ni ujinga wa lugha tu kuhubiri kwamba kulikuwa na kitu katika kutoka matamshi “SAULI” kwenda “PAULO.” Kwa vyovyote hili ni jambo dogo na lenye kutibika.
Uovu wa Kiroho – “Wakatoliki Kuokoka”
Uovu wa kusikitikiwa zaidi ni uharibifu uliofanywa na mkutano huo. Hakika haya ni madhara yatakayohitaji JIK kuoshwa. Wakatoliki wamehubiriwa waokoke licha ya kwamba kwa sakramenti ya Ubatizo walishafanyika Wakristo Wakatoliki. Wamekubalishwa kwamba walikuwa na upungufu kiroho. Wamekubali kuokoka, jambo ambalo maana yake ni kupingana na Yesu pamwe na Maandiko Matakatifu. Haya ni mapato ya ujinga ule ule niliokuwa nimeudokeza hapo mwanzo. Watu wetu hawajui “lipi ni la Kikatoliki” na “lipi si la Kikatoliki.” Wanapokea na kula vyote. Asalale! Hawana uwezo wa kupambanua “SUPU” na “SUMU.” Hawana uwezo wa kupambanua “KARIBU” na “KALIBU.” Alahaula!
Kwa hili, msishawishike kuniita nabii maana ilikuwa hatari ya wazi. Hata mlemavu wa macho aliweza kuiona. Hata mlemavu wa masikio aliweza kuisikia. Hata mlemavu wa miguu angeliweza kuikimbia.
Sikilizeni. Sisi Wakatoliki hatuthubutu kupingana na Yesu kwa kujinasibu TUMEOKOKA kwa sababu Yesu mwenyewe aliliweka jambo hilo katika wakati ujao (future tense) – ATA… na siyo wakati uliotimilika (perfect tense) – AME…. Soma alivyosema Yesu mwenyewe, “Mwenye kusaburi hata mwisho, ndiye ATAKAYEOKOKA” (Mk 13:13). Hata Mtume Paulo tumsome vizuri. Mtume Paulo ameandika, “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu UTAOKOKA.
Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa kukiri hata kupata wokovu – yaani mwishoni mwa maisha haya siyo sasa” (Rum 10:9-10). Hivi ndivyo tunavyopaswa kumwelewa Mtume Paulo na si vinginevyo. Usinikaidi. Ndiyo maana ya kusema pia, “Anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke” (1Kor 10:12).
Hivi mtu kudai “NIMEOKOKA” ni kusiganisha wakati wa kitenzi alichotumia Yesu na hiyo ndiyo maana ya “UPINGA KRISTO” na “UPINGA MAANDIKO MATAKATIFU.” Kumbe, kabla mwamini hajamaliza mapambano na ulimwengu huu si maungwana kujinasibu ameokoka. Ni majigambo hatari kabisa kiroho. Kuupata uzima wa milele, ndiyo kukaa kulia na kushoto kwa Mungu, ni tangazo la mwishoni kabisa na litafanywa na Mungu mwenyewe (Mt 25:34, Mk 10:40). Tungalipo hapa duniani chochote kinaweza kutokea wakati wowote. Ndiyo maana Yesu alisema pia, “Wa kwanza watakuwa kuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza” (Mk 10:31). Hii maana yake tuishi tukichelea “kipindupindu cha kiroho.”
Aghalabu, busara hii tunaweza kuikokotoa hata kutoka Agano la Kale, maana humo imeandikwa, “Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja. Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe, mtu mgeni wala si midomo yako mwenyewe” (Mit 27:1-2). Na YbS 11:27-28 yanasema, “Tena taabu ya saa moja huleta usahaulifu wa furaha; na mwisho wa mtu ndio ulio ufunuo wa habari zake. Usimwite mtu heri kabla ya kufa kwake; aidha mtu hujulikana kwa kuwatazama watoto wake”. Ndiposa katika busara hii, Waswahili husema, “Kabla hujafa, hujaumbika.”
Yalikuwa Matokeo Tarajiwa
Lakini mwenzenu sikushangaa matokeo hasi baada ya mada ya Mwakesege. Sikushangaa kuwaona Wakatoliki wakisimamishwa kuokoka. Wamesonga mbele “KUOKOKA.” Nilishaandika kwenye mada yangu, “NI MWENDELEZO WA UJINGA WETU ULE ULE”, “Mwamba ngoma ngozi kwake.” Si mmeona wenyewe? Mtu alipewa hadhira ya Wakatoliki, watu anaowatafuta kwa hamu kubwa, basi amewavunia kapuni mwake kilaini kabisa. Nikufikirishe.
Kigogota anayefanya kazi kubwa ya kubangua miti akitafuta funza wa kula, panzi akimtua mdomoni pake atamtema? Hii ni aibu kubwa kweli kweli! Wachungaji wa kondoo tunachunga nini? Hapa tumewauza kondoo mchana kweupe. Ni aibu kubwa! Wakatoliki wamesemeshwa “SALA YA TOBA” hadharani na hakuna mkubwa yeyote Mkatoliki aliyepinga hilo kwa mwono wa Kikatoliki.
Tazameni hiyo video. Hakuna mchungaji aliyewalinda kondoo kabisa. Kinyume chake aliyewazoa amepigiwa makofi ya kupongezwa na kushukuriwa. Jamani, Mwakesege ameshinda mbele ya watu tuliompelekea huku tukiona. Mwakasege oyeee! Amewapata watu wetu tele. Je, sasa mtaka ushahidi mwingine wa ujinga wetu?
Kumbe, heri na heko maparoko vijana na Askofu wa Iringa kwa hatua mliyochukua! Huku kwingine usingizi wa pono unaendelea kwenye vitanda vya samadari na magodogo ya QFL! Haya twende tu! Lakini ufa huu tusiotaka kuuziba sasa, tujiandae kujenga ukuta! Mwiba huu tusiotaka kuutoa leo, tujiandae miguu kutuzukia matende!
Mzee wenu Pd. Titus Amigu