Oukumene yaleta sintofahamu ndani ya Katoliki

"Nje ya ukatoliki hakuna wokovu" Hii umeitoa wapi kwenye mafundisho ya kanisa katoliki ?
Hayo ni mapokeo ya wazee roma wanavituko kwa kweli😁😁
 
Papa atabaki kuwa kiongozi wa wakatoliki
Yesu kristo ataendelea kuwa kiongozi wa wakristo
 

Yohana 6:44​

Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka...
 
Umoja ni nguvu..sio mbaya kuungana kwa lengo moja..huu utengano wa kidini sio mzuri unaleta mipasuko mingi kwenye jamii zetu.
 
Aendelee kukaza fuvu, azidi kujitia ujinga huyo Padri
 
Msomi Padri Titus Amigu. Ni hazina ya Kanisa. Mungu amuweke miaka mingi ili atupe hekima yake. Karismatiki imeingia kiuhuni ndani ya Kanisa Katoliki, inatuletea mafundisho ya ovyo kama laana, uchawi n.k. Unamualika mchungaji hata teolojia hajasoma anakuja kukuhubiria nini? Hayo ndo matokeo yake, hajui sauli na paulo 😂
 
Tulia mjumamosi. We umeshikwa akili na kale kamama kenye schizophrenia.
 
Wasabato watauvamia huu uzi na kuanza porojo zao 😂😂 mara papa, mara kanisa kahaba. Akili za wasabato kumfuata nabii wa kike Ellen Gould White ambae aliumwa ukichaa ni tatizo
 
Shetani hana shida na hizi aina ya imani hata kama mtaungana kuwa dini moja dunia nzima, shetani anachopambana nacho ni wewe usiwe na imani inayokupa uzima wa milele..........yaani kujua, kusadiki na kuwa na hakika ya kwamba Yesu Kristo ndiye Bwana wa kutupeleka kwa baba.

Ukichukulia mfano wa kanisa la Perigamo ambamo palikuwa na kiti cha enzi cha shetani, utaona kwamba hao watu walikuwa wanaendelea na taratibu zao za ibada ya kikristo kama kawaida lakini haikumpa shida shetani aliyekuwa kaweka kiti chake cha enzi hapo, kwa sababu aina ya imani waliyokuwa nayo haikuwa ile inayowapa uzima ule wa Mungu.
Kwa hiyo kuweni makini na hizi sarakasi zinazoendelea duniani za kuunganisha madhehebu kwa kivuli cha kujenga mapatano (harmony), kuna mtego mkubwa ndani yake, tujitahidi sana kutafakari mambo kwa kina.​
 
Sijawahi kuwaelewa Charismatic Catholics. Hawajakaa Kikatoliki kabisa.
 
Sijawahi kuwaelewa Charismatic Catholics. Hawajakaa Kikatoliki kabisa.
Ni wakatoliki ambao wanadhani style za walokole ndio dili. Yani badala wao wawafundishe walokole ukristo wao ndio wanawaiga, kituko. Mbaya zaidi hawataki kuhama kanisa. Hawa ni mwiba. Wahame watuache na kanisa letu, sisi miujiza na majibu tunayaona kila siku kwenye maisha yetu bila fujo za kelele na kufokafoka.
 
kwakweli nimeso bila kuchoka namkubali sana,anayoyafundisha si yake binafsi na hakurupuki kwenda kwenye kipindi mana kanisa katoliki hata uwe na elimu kubwa husemi ya kiimani kwa kujiamulia ukiwa kiongozi.Yapo matatizo na mapungufu ya baadhi ya mapadre kuingia ktk upadre kwa fashen hawaendelei kujibidiisha wanakuwa wazembe.Pdr amigu anafundisha kwa facts na yupo chini ya kanisa katoliki si kama hao wanaomiliki kanisa binafsi uhuni tu.Mwisho papo mahala padogo sijamuelewa ameandika usimwite mtu heri kabla hajafa.Kwanini wakatoliki tunamuita papa baba mtakatifu?Kuna tofauti yeyote na kumuita mwenye heri?
 
Mwisho papo mahala padogo sijamuelewa ameandika usimwite mtu heri kabla hajafa.Kwanini wakatoliki tunamuita papa baba mtakatifu?Kuna tofauti yeyote na kumuita mwenye heri?
Baba mtakatifu.. Ikimaanisha kiti chake alichokalia anachokiongoza ndio kitakatifu.
Hapo haimaanishwi personality yake kama kiongozi.
 
Akili yako ikiwa nyepesi huwezi kumwelewa Amigu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…