kina kirefu
JF-Expert Member
- Dec 14, 2018
- 15,188
- 18,583
Lete vitu uliishia sehemu Gani ,endeleza stori za bingwa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Boss hapa ungekuwaa muungwana kama ungeongeleaaa kile kibao cha Pac na N.W.A cha "https://jamii.app/JFUserGuide the Police"KWANINI TUPAC ALIMCHUKIA SANA BIGGIE MPAKA KIFO ? (4)
_______________
Inaendelea......
Kutokana na Tupac kuhitaji bosi wa Death Row, Marion 'Suge' Knight apambane kumtoa ndani ili waweze kufanya biashara pamoja, Suge aliangaika huku na huko mpaka kufanikiwa kumchomoa Tupac jela.
Kiasi cha Dola Milioni 1.4 kilitolewa na Suge hivyo kufanikiwa kumtoa jela Tupac mwaka 1995, achilia mbali Dola 15,000 ambazo Suge alizitoa kumsaidia 'kishkaji' Tupac wakati akiwa jela.
Kimsingi Suge alikubali kujipukutisha fedha kwa sababu alijua kumwandika Tupac mkataba wa kumsimamia kupitia Death Row Records italipa. Knight alijua nini anafanya kwenye makubaliano hayo.
Makubaliano ya Tupac na Suge yakawa mazuri. Tupac akakubali kutengeneza albamu 3 chini ya Death Row Records lakini muda wote akihitaji Suge awe upande wake kwenye vita vyake dhidi ya Biggie.
Nyimbo ya kwanza ya Tupac kuitoa chini ya Death Row Records ikawa California Love. Kombinesheni ya Tupac, Dr Dre na Roger Troutman kwenye chorus ukawa unyama wa kufa mtu. Kwa hakika "The King was back from Jail''.
Ujio wa California love ulimtikisa kila mtu. Tupac alikuwa amejerea kuusimika upya ufalme wake uliotishiwa kuondoshwa kwa mtutu wa bunduki na vijana kutoka Pwani ya Mashariki (East Coast).
Marion Suge Knight na Tupac Shakur wakafanikiwa 'kuupika' mgogoro wa East Coast na West Coast ukapikika, mgogoro ambao chimbuko lake haswa ni chuki baina ya wasanii wawili, Notorious Big na Tupac Shakur.
Matatizo binafsi ya Biggie na Tupac yakajikuta yakirithiwa na hata wengine 'yasiyowahusu'. Wasanii wa East na West wakaonekana kuchukiana katika kiwango kilichotisha kabisa.
Wakati mgogoro huu ukikua na kuzidisha uhasama kwa wasanii, Serikali mwanzo ilionekana kama kupuuza, lakini kadiri hali ilivyozidi kuwa mbaya na viongozi walilazimika kusema chochote.
Lakini kabla ya kusema chochote, huko nyuma Tupac alikuwa ameshaingia kwenye mgogoro mara kadhaa na serikali kutokana na misimamo yake, harakati zake na maisha yake.
Nyimbo zake kupitia albamu yake ya 2Pacalypse ziliichefua sana serikali. Tupac alizungumzia zaidi Siasa, Ubaguzi na umasikini katika namna ambayo ilionekana kama kuchochea chuki kwa raia.
Mshtuko mkubwa ulitokea baada ya kijana mmoja mdogo kumpiga risasi polisi na kumuua kisha baada ya kukamatwa na kuhojiwa akathibitisha kufanya hivyo baada ya kusikiliza albamu ya Tupac iitwayo 2Pacalypse.
Tukio hilo lilikuwa gumzo nchini Marekani. Aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo, Bw Dan Quayle akatangaza kupigwa marufuku kwa nyimbo za Tupac kusikilizwa kwenye Jamii ya wamarekani.
Bw. Quayle alisema Tupac ni msanii asiyefaa kabisa kusikilizwa. Nyimbo zake zimejaa chuki na kuchochea uovu kwenye jamii. Akaanzisha kampeni za kuhakikisha jamii inamchukia na haipati nafasi ya kumsikiliza Tupac.
Masikini Quayle hakuwa amejua kuwa wakati anasema hayo, Tupac alikuwa ameshaiteka sehemu kubwa ya jamii ya wamarekani kuliko anavyodhani. Mahojiano yake na MTV ya mwaka 1993 yamlitosha kabisa kumfanya asimjibu lolote.
"Siwezi kuitawala dunia wala siwezi kuubadilisha ulimwengu, bali nichoweza kufanya ni kutema cheche zitakazofanya bongo za watu kuibadilisha dunia"..hii ndiyo kazi yetu tunayopaswa kufanya, kuamsha mtu mwingine anayetutazama".
Tupac alikiambia kituo cha televisheni cha MTV mwaka 1993 katika moja kati ya mahojiano yake yanayoendelea kukumbukwa mpaka leo. Quayle alishindwa vibaya katika kampeni ya kumaliza Tupac, lakini inaelezwa alichangia mno kupromoti mauzo ya kazi zake bila ya yeye kujua.
Watu mashuhuri mbalimbali waliyataja maneno hayo machache ya Tupac kama maneno bora zaidi kuwahi kutolewa na mtu "asiyetegemewa" na wengi kusema hivyo. Wengi waliyatumia kama rejea kwenye maeneo yao mbalimbali.
"Inawezekana baadhi yetu tusiwe watu wa kuibadilisha dunia, lakini tunapaswa kujaribu kila wakati kushawishi mtu mwingine kuchukua hatua zitakazoweza kuibadili dunia".
Maneno haya ya Tupac hata kwangu binafsi bado yanaishi sana.!
Itaendelea........[emoji3578]
#Balozi
Boss lile Song https://jamii.app/JFUserGuide the Police lililetaa Uhasama mkubwaa Mno kati ya Serikali na Wahuni wa ComptonYaani watu wanaongea pumba tupu humu. Eti Tupac aliuawa na Serikali. Really? Kwa impact gani aliyokuwa nayo kuitetemesha Serikali? You are giving him too much credit. Nataka mtu aniwekee kauli au lyrics au vitendo vya Tupac ambavyo viliitetemesha Serikali mpaka itake kumuua.
Ukute hata habari za Big mwenyewe hawazijui, yan mpaka waende kuokota mawili matatu kwenye vijiwe vya kahawa ndo waje kujaribu kutulisha matango pori kwa habari sijui za kusimuliwa na mjomba wake muuwaji wa Big 😂😂😂😂Natamani naninyi mlete stori habari za B.I.G ingependeza
Ndio maana nikasema kwamba assumptions zako ni za kijinga. Eti kwa kuwa Tupac alizaliwa na Afeni Shakur basi tayari Serikali inamchukulia kuwa ni rebel. Halafu hayo maneno aliyosema Pac mpaka Serikali ikatetemeka ni yapi? Mbona hamuyaweki hapa?Wewe huenda unabisha tu bila kujua unachobishia, au unajua ila umeamua tu kuleta ubishi ili isionekane kuwa umeshindwa.
Kitendo cha 2pac kuzaliwa na mwanamke aliekuwa member wa black panther peke yake tayari lilikuwa tishio kwa mfumo wa kibaguzi wa enzi zile. Hapo sijazungumzia yale aliyokuwa anaaongea mara kwa mara kuhusu ubaguzi wa rangi waliokuwa wanafanyiwa watu weusi kitu ambacho mamlaka hawakukipenda maana ni kama kilikuwa kinawavua nguo duniani. Na ikizingatiwa kuwa taifa hilo lilikuwa linajinasibu kuwa ni la kidemokrasia na linalopambana na ubaguzi mbali mbali.
Chuki hiyo ndio iliyopelekea kifo chake. Na sio yeye tu. Hata wale ambao wewe unaona kuwa sio tishio pia waliuwawa au kuuliwa hovyo barabarani.
RIP George Floyd na wengine waliouwawa hovyo. Ingekuwa watu hawaku record au kufuatilia vifo vyao. Basi majumba mabovu wangeangushiwa kina Orlando wengine au yale magenge ya kihalifu kama ilivyokuwa desturi yao.
Yani ungetengenezwa uongo uliopangwa rangi vizuri na leo hii ingekuwa mmoja wa wanaoamini kuwa watu hao waliuwana wenyewe kwa wenyewe.
Stori gani ya Biggie unaitaka?Natamani naninyi mlete stori habari za B.I.G ingependeza
Umeshamezeshwa uongo na mjomba wake Orlando, so ni vigumu sana mtu kukuelewesha hadi ukaelewa tunachojadili.Ndio maana nikasema kwamba assumptions zako ni za kijinga. Eti kwa kuwa Tupac alizaliwa na Afeni Shakur basi tayari Serikali inamchukulia kuwa ni rebel. Halafu hayo maneno aliyosema Pac mpaka Serikali ikatetemeka ni yapi? Mbona hamuyaweki hapa?
Mnataka kumuweka Tupac kwenye level moja na MLK, Malcolm X na Fred Hamptons. Kamwe hakuwa kwenye level hiyo.
George Floyd alikuwa victim wa Police brutality. Sijui hata anahusiana kivipi na huu mjadala. Dude, you are all over the place, hata hujui unataka kuongea nini.
Mimi nazijua za makaveli uanyejua za b.i.g zilete hapa tupitieStori gani ya Biggie unaitaka?
Umeandika nini hiki?Tupac alikuwa na hasira baada ya kutokea ugomvi baina yake na BIG kuhusu utunzi wa wimbo fulani, alikwenda kwenye vyombo vya habari na kuanza kujisifu kuwa amelala na Faith Evans mke wa BIG.
BIG akaona isiwe shida ammalize tu. Kundi la Tupac likaamua nalo lilipize kisasi na vijana wawili wadogo wakaondoka kiurahisi sana.
Faith Evans akatoa wimbo mmoja mkali sana wa kumkumbuka BIG chini ya uongozi wa P Didy....
kama hujui kusoma na kuelewa siwezi kukusaidiaUmeandika nini hiki?
Diddy mjasiriamali sana.Big aligundua kwamba Diddy alikuwa anamnyonya sana, kwahiyo alikuwa amepanga akimaliza mkataba wao anaachana nae kitu ambacho Diddy hakupendezewa nacho na pengine kuamua kufanya kile anachohisi mama yake na Big.
Baada ya kifo cha Big Diddy umaarufu wake uliongezeka maradufu na pesa ikawa nyingi kutokana na kuuza nyimbo nyingi za Big ambazo bado zilikuwa studio kwake.
Pia akawahi fasta fasta kutoa ule wimbo wa 'I'll be missing you" akiwa amememshirikisha Faith Evans (ex wa Big) Nyimbo ile moja tu peke yake ilimpa pesa nyingi ambayo kama Big asingefariki basi angekaa zaidi ya miaka 5 bila kuishika.
So kifo cha Big kimemnufaisha zaidi Puff kuliko kilivyoinufaisha familia yake Big.
Pddy hawezi kumuu BIGGIE nakataa,kwenye gari alipokuwepo BIGGIE Kulikua na ndugu yake wa damu..
Eugene deal ambae ni bondia wa pddy(Mtoto wa kaka yake)
Lil cease mjomba wa B.I.G na member wa JUNIOR M.A.F.I.A wote walifia humo..
Pddy ndio power control kwenye kesi ya SUGE Na anamchomekea kweli,halafu mwezi uliopita mama yake B.I.G Alikutana na SUGE mahakamani na wakati anarudishwa jela waliondoka pamoja..
BEEF YA SUGE KNIGHT NA P.DIDDY HAIWEZI KUISHA