Hahaha, mazishi ya Tupac Shakur hayakuhudhuriwa na watu??? [emoji23]
Tupac alichomwa moto siku ya 14/09/1996 mpaka kuwa majivu kabisa kama ilivyo desturi ya wengine wanaoamua kufanyiwa Cremation, hata mama yake aliamua kuja kuchomwa
Wakati akichomwa... nje ndugu zake na masela zake wengi sana wakisubiri majivu yake
Mama yake alikuwa Mtu wa kwanza kuchukua majivu na kuondoka nayo kumwaga kwenye garden ya Nyumbani kwake asubuhi siku iliyofuata
BLACKII, ni Mshkaji wa Tupac (Mghana) aliyekuwa naye kundi moja OUTLAWS aliishi Arusha kuanzia julai 1997 mpaka 1999 yeye na GERANIMO PRATT kisha akaenda kwao Ghana, angeweza kukueleza yote unayotaka kujua kuhusu Tupac
wote wawili nao waliamua kuwa wakifa wachomwe pia na walichomwa
Kwa namna flan kuna order ya FBI ilichochea Tupac na wenzie kuuawa na kuna list ilikuwa inaendelea wakiwepo akina BLACKII
Mengine watu wanaongea tu ila hayana ukweli
Asante mkuu, wewe ndio umeongea mambo yanayoeleweka. Yani kama mtu hakukuelewa ulichoandika basi itampasa ajitafakari upya kuhusu nini anachobishania.
2pac na familia yao hawakuwa na record nzuri katika vitengo vya usalama. Mama yake na 2pac alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa black panther kwa upande wa wanawake, hivyo vyombo vya usalama bado vilimuona kuwa ni mtu hatari kwa mamlaka iliyokuwa chini ya utawala wa wazungu wenye chembe chembe za ubaguzi.
Halikadhalika 2pac nae alikuwa miongoni mwa maadui wa mamlaka na vyombo vya usalama. Ndio maana hata 2pac mwenyewe kabla ya kufa kuna muda alikuwa akihusisha kesi zake na mamlaka. Yani alikuwa anamaanisha kuwa mamlaka zilikuwa zikimtengenezea kesi mbali mbali kwa lengo la kumchafulia taaswira yake mbele ya watu waliomuheshimu na kumuamini, kwa lengo la kumvunja moyo na kumkomoa.
Lakini pamoja na yote bado walishindwa kumnyamazisha 2pac na badala yake ilikuwa kama vile wanaongeza petroli kwenye moto, 2pac hakunyamaza bali aliendelea kusema tena kwa kuwataja viongozi wakuu wa serikali majina akiwemo raisi wa nchi wa wakati huo pres Bill Clinton na makamu wake. Pia 2pac hakuishia hapo ilifikia kipindi mpaka akawapiga maafisa wa polisi risasi na kufikishwa mahakamani kisha akatoka.
Sasa unafikiri kwa aina hii ya misuguano kati ya 2pac na serikali wangemuacha salama kweli. Kama yule mmarekani George Floyd aliuwawa na polisi kwa kuwekewa goti shingoni bila kosa au sababu yoyote, je 2pac alietaka kuwauwa maofisa wa polisi ukijulimsha na historia yake ya kuwapaka viongozi wa serikali na kuwatukana polisi wangemuacha hai kweli aendelee kuichafua serikali hiyo iliyokuwa imejaa ubaguzi?
Watu wa system walipogundua kwamba 2pac ni mtu wa hasira na panic wakaamua kumtengenezea mazingira kwa kuset Orlando aibe cheni kwa rafiki yake 2pac, kisha afike katika pambano la Tyson wakiamini kwamba akifika na kukutana na 2pac ni lazima moto utawaka katika ya 2pac na Orlando. Moto ukishawaka wao wataitumia chance hiyo kufanya yao afu kuyahusisha makundi ya gangs na mauaji yale ili kupoteza ushahidi.
Na kweli mission imefanyika na kupangwa kama ilivyokuwa imetakiwa kupangwa. Ndio maana leo hii wasiofikiria nje ya box wanafikiri kuwa kijana Orlando ndio muhusika wa mauaji yale, huku waliouwa wakiendelea kufanya shughuli zao ndani ya vitengo na kupongezana kimya kimya.